Pages

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Sunday, May 06, 2012

Diamond afunguka! Nimejiajiri, nimeajiri kupitia muziki


 MSANII anayeongoza nchini Tanzania kwa ubunifu wa kufanya shoo nzuri na zenye mvuto mkubwa kwa mashabiki wake amesema kuwa kwake muziki ni ajira na ni kazi kama ilivyo kwa mfanyakazi anayeingia ofisini.

Mshindi huyo wa tuzo tatu za Kilimanjaro kwa mwaka huu na mwaka 2010, alisema kuwa anafanya kazi hiyo kwa malengo zaidi na ndio maana anaweza kuwateka mashabiki wake na kuufanya muziki wa kizazi kipya uzidi kupendwa ndani na nje ya nchi.

"Nafanya muziki kama kazi, sifanyi muziki kujifurahisha mimi na kutafuta pesa pekee huku nikiwaacha mashabiki zangu hawajakata kiu ya burudani," alisema Diamond.

Alisema kikubwa hasa anachokifanya ni kushirikiana na watu na siku zote anaamini kuwa hawezi kufanya kazi peke yake pasipo kuwa na wacheza shoo wake kwani ndio wanaompa sapoti kubwa na kubadilishana mawazo ili kuleta vionjo vipya.

"Unajua mimi sina ubahili hasa ninapofanya kazi, na hili ndilo lililonifanya nizidi kusonga mbele katika kazi ya muziki ili upate ni lazima utoe, ili nifurahishe mashabiki ni lazima nizingatie kanuni kama hizi," alisema.

Diamond aliongeza kuwa maandalizi ni silaha nyingine ambayo inamfanya kila siku mashabiki wamwone mpya. "Siwezi kutokeza machoni mwa mashabiki nikiwa hivyo hivyo kila siku hata nikiwa na wimbo mpya sidhani kama watanifurahia kila siku staili hizo hizo, pia namtanguliza Mungu katika kila jambo," alisema.

Hata hivyo amewashukuru mashabiki na kuahidi kutowaangusha "nawashkuru sana na nawaahidi kuwa sitowaangusha na wategemee vitu vipya".

Wikiendi iliyopita msanii huyo alifanya shoo katika sehemu ya kiburudani ya Dar Live iliyopo jijini Dar es Salaam na kuvunja rekodi kwa kuingiza mashabiki wengi zaidi kuliko shoo zote zilizowahi kufanyika sehemu hiyo

Diamond ambaye alivaa mavazi ya kibaharia aliwasili eneo hilo kwa usafiri wa helikopta na hatimaye kuingia katika gari aina ya benzi ambalo lilimsogeza mpaka jukwaani.

Licha ya mvua kubwa iliyonyesha mashabiki walionekana kujifunika viti vyao kichwani ili waweze kuona utumbuizaji wa msanii huyo.

Lady Jaydee apanga kutengenezewa beat na Dr Dre!

 


Ameshafanya kazi na wasanii wakubwa Afrika kama Oliver Mtukuzi na wengine lakini kwake Judith Wambura aka Lady Jaydee anaona haitoshi.

Sasa anatamani kufanya kazi na producer mkubwa kabisa duniani na ambaye kwa mujibu wa orodha ya wafalme wa Hip Hop wenye mshiko zaidi duniani (Forbes) mwaka huu amekamata nafasi ya tatu, Andre Romelle Young ama Dr Dre, whaaaaaat! Jaydee you must be kidding right?

Mapema Jumapili hii Jaydee ametweeet, "Mwaka huu unaisha tena kabla Dr.Dre hajanitengenezea Beat, inabidi nijipange upya"

Anaposema mwaka huu unaisha bila kupata mdundo mzito kutoka kwa mchawi huyo wa beats Dr Dre anamaanisha kuwa amejiwekea mpango huo kwa muda mrefu bila shaka!

Bad news kwa Jaydee ni kwamba kama akitaka kufanikisha mpango huo ni lazima akusanye kuanzia dola 100,000 hivi kwa beat moja ambazo ni karibu shilingi milioni 150 za Tanzania! Kama akifanikisha atakuwa msanii wa kwanza anayeishi Afrika bila shaka kuwahi kufanya kazi na Dr Dre!

All the best Jide japo kwa gharama hiyo ni kweli huna budi kujipanga upya!
 
Na daily entertainment take away

Mayweather awapa raha wana Hiphop!

 


Ukimtoa Mike Tyson, hakuna boxer mwingine duniani kipenzi cha wanamuziki hasa wa Hiphop kama Floyd Mayweather Jr.

Usiku wa kuamkia leo amedhihirisha kuwa hatakuja kushindwa ulingoni na boxer yoyote wa uzito wake kwa kumshinda Miguel Cotto kwa pointi na kuchukua mkanda wa WBA junior middleweight.





















Boxer pekee aliyebakia na ambaye anadhaniwa pengine anaweza kuivunja rekodi yake ya kutopigwa ni Manny Pacquiao wa Ufilipino.

Baada ya ushindi huo, wanamuziki na watu wengine maarufu duniani waliushambulia mtandao wa twitter kuonesha furaha yao juu ya ushindi huo uliompa dola milioni 32 za kuweka benki ama kula bata!


YALIYOJIRI KWENYE KILI MUSIC AWARD WINNERS MWANZA

 

 Show ya hapa Mwanza ilifunguliwa na msanii wa taarabu Isha Mashauzi, shangwe zilikuwa zakutosha kabisa na wapenzi wa burudani ya taarabu walipata chakula cha ubongo.


 Akafuatia msanii aliyechukuwa tuzo ya RnB anajulikana kama Ben Pol

 Misago, Hellen & Dullah

Barnaba, Hellen & Sam Misago 

Kaka mkubwa ndio aliyekuwa akiangalia ulinzi wa wasanii wote wakiwa salama 

 Ikafikia zamu ya Ommy Dimpozi kupanda kwa steji, na show ilikuwa bab kubwa 

 Barnaba aka Baba Steve kwa steji

 Wacheza show wa msanii Diamond

 Ikafika zamu ya mtoto wa Zanzibar AT kupanda kwa steji

 Ikafika zamu ya msanii mwenye tuzo 3 kupanda kwa steji, hapa namzungumzia Diamond 

 Mtoto wa Tanga Roma ndio aliyefunga show kwa upande huu wa Mwanza

Ommy Dimpoz katikati
Na Dj Choka

Wanamuziki wa Kenya kufanya maandamano ya amani



Wanamuziki wa Kenya kesho May 6 watashiriki katika maandamano ya amani katikati ya jiji la Nairobi.

Wasanii hao kwa pamoja wakijiita Kenya One, wataungana kusisitiza amani na mshikamano nchini humo katika kuelekea kipindi cha uchaguzi.

Wataungwa mkono na watu wazito akiwemo mwenyekiti mtendaji wa Safaricom Bob Collymore na Jimnah Mbaru na Chris Kirubi.


Bob Collymore


"Tutatembea kutoka KICC na kuzunguka mitaa yote mikubwa. Tunawaomba wakenya wenzetu kuangana nasi katika jambo hili” alisema mwanadada  Size Eight.





Size 8

Beyonce apewa tuzo ya uandishi wa habari!

 


Beyonce Knowles – mwanamke mrembo zaidi duniani  (kwa mujibu wa People Magazine) mke wa rapper wa pili kwa hela duniani, Mama wa mtoto mrembo na mshindi wa tuzo kibao za Grammy na sasa ameongeza heshima nyingine ambayo si rahisi kuifikiria .

















Mwanamuziki huyo ameshinda tuzo kutoka kwenye umoja wa waandishi wa habari weusi wa New York kwa makala yake aliyoiandika kwenye jarida la Essence iitwayo "Eat, Play, Love”.

Katika makala hiyo Beyonce anahalalisha uamuzi wake wa kuchukua miezi tisa nje ya shughuli za muziki kwa kusafiri na kujitambua. Sentesi zilizoshinda ni pamoja na ile aliyoandika “, “In Capri I ate pizza and drank red wine every Sunday. I discovered I love artichokes and that a salad and fresh fish are not only healthy choices but incredibly delicious.”

Hata hivyo uamuzi wa Beyonce kupewa tuzo ya uandishi wa habari umekosolewa vikali.

“Tuzo kama hizi huwasahau wana habari wa kweli ambao huandika mada za maana na za hatari” alikosoa mwandishi mmoja wa Mused Magazine.

Ripoti ya mwandishi huyo ilionesha mashaka iwapo kweli Beyonce aliandika kipande hicho mwenyewe. Hata hivyo mhariri wa burudani wa Essence Cori Murray ameliambia gazeti la New York Daily News, “Ni mwandishi wa kweli. Tulihariri alichokiandika lakini kila mmoja huhaririwa isipokuwa Toni Morrison”.

Wakati Beyonce akijiongezea heshima nyingine ya uandishi wa habari, ameamua kuuonesha uzuri wake kiduchu akiwa bila nguo kwa kusambaza picha hii!










Damn!!!
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Na daily entertainment

Simu za Jose Chameleone zawa kimbilio la wanyonge

 


Wanasema ukiwa na hela unaweza kufanya lolote utakalo! Yaweza yasiwe mambo yote katika dunia hii kama vile kununua pumzi, lakini wazo la biashara lolote linaweza kutekelezwa kama pesa ikiwepo.

Kibongobongo wazo rahisi kabisa la msanii wa muziki apatapo vijisenti ni duka la nguo? Hakuna idea zingine? 

Ni tofauti kidogo kwa nguli wa muziki nchini Uganda Jose Chameleone.

Yeye anafikiria mambo makubwa zaidi! Tayari wiki iliyopita amezindua simu zake za mkononi ziitwazo Chameleone Mobile!

Katika uzinduzi huo wa nguvu watu maarufu, wawakilishi wa makampuni ya simu na wadau wa mawasiliano ya simu nchini Uganda walihudhuria.

Bobi Wine alikuwepo kwenye uzinduzi kumpa shavu mwenzie
Simu hizo za bei bwelele kabisa zitakuwa na rangi mbalimbali za “Kinyonga”.  Pamoja na bei yake kuwa ndogo jambo ambalo litazifanya zinunuliwe kama njugu na hasa wananchi wa kawaida, simu hizo zina memory card, flashlight, FM radio,MP4 player na vingine.

Zilianza kuuzwa muda mfupi tu baada ya kuzinduliwa huku zingine zikitolewa bure kwa wageni waalikwa. 

Simu hizi za Chameleone zinauzwa kwa shilingi 60, 000 ya Uganda sawa na shilingi 35,000 hivi za Tanzania.

Chameleone atatumia duka la kaka yake Humphrey Mayanja lililipo Ivory Plaza jijini Kampala kama makao makuu ya simu hizo.

Uhakika ni mkubwa kuwa maelfu ya watumiaji wa simu nchini Uganda watataka kuimiliki kutokana na bei yake ndogo na jina la mwanamuziki huyo.  Hiyo ni sababu makampuni mengi ya simu yamekuwa karibu naye yakitaka kuingia ubia wa kibiashara naye.


Nini kilitokea kwa maji ya Lady Jaydee aliyekuwa na mawazo makubwa kama ya Chameleone!!!!
Na daily entertainment take away.

Saturday, May 05, 2012

ASLAY ALIPO KUWA MAKETE

Aslay kwa Stage

KILI MUSIC AWARD WINNERS SASA NI ZAMU YA MWANZA KUPATA LADHA YA UBONGO.

 

Tukiwa Airport ya Dar pichani ni Dullah wa Planet Bongo na Barnaba 

Wakati tupo uwanja wa ndege tukakutana na rafiki zetu Arthur na Salama Jabir na walikuwa wanaelekea Mwanza ila kwenye kazi yao ambayo haiusiani kabisa na tour ya Kili 

Ommy Dimpozi & AY wakiwa tayari kuingia kwenye ndege, AY alikuwa na Salama so AY yeye anashow kesho jumapili hapa hapa Mwanza

Baada ya kufika Mwanza salama tukapata nafasi yakwenda Radio Free Africa kufanya interview kidogo 

Barnaba Boy
 

Labels