Pages

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Friday, December 28, 2012

ANGALIA PICHA JINSI EMPOWERMENT MUSIC GROUP WALIVYO FUNIKA KATIKA SHOW YAO SIKU YA KRISMASI

 Empowerment Music Group kwa Stage na dancers wao
 Mr Red moja ya member wa kundi hilo akituzwa na Mdau wa muziki



 Ergon Elly katika Willz of Chuma

 Ergon Elly [kushoto] na Y - Jay member wa kundi

 Mashabiki wakifuatilia kinachoendelea Ukumbini kupitia Big Screen
 Y - Jay member wa EMG
 Mr Red [kushoto] na  Y - Jay



Show ilifanyika katika viunga vya Makete mjini ilikuwa ni moto wa kuotea mbali.
 
Show Hiyo ilidhaminiwa na General Supplies Limited[Francis Sheli],Luvanda Photo & Video Studio,BM Salon,B Pub pamoja na Stopper Inc.

[NSong] Brand New - Joh Makini - Sijutii

Hii ni audio ya wimbo wa Joh Makini 'Sijutii' ambayo video yake ilishatoka. Kwa mujibu wa JOh wimbo huu ulirekodiwa mwaka 2007 na umekuwa released mwaka huu 2012. 
 
Unaweza kuusikiliza na kudownload hapa.

[SONG] BRAND NEW - R.O.M.A - 2030 Intro

      

Hii ni Intro ya ngoma mpya ya ROMA Mkatoliki inayo kwenda kwa jina la 2030 ambapo ametoa story kamili dhidi ya maisha ya mwanae na maana nzima ya 2030. 

Top 20 ya wasanii waliojitolea zaidi kusaidia jamii mwaka 2012...Taylor Swift aongoza, list yamtema Rihanna.


Taylor Swift
Japokuwa jamii ndiyo inayomuweka juu mtu yeyote lakini pia hutegemea kitu kutoka kwake baadae kulingana na moyo wake mwenyewe na anavyoiona jamii ya wahitaji mbalimbali, kwa kujitolea kuisaidia jamii hiyo tunaita 'kuirudishia jamii" ama kwa lugha ya kigeni tunaweza kusema 'giving back to the society'

Kwa mujibu wa mtandao wa shirika la kusaidia jamii "DoSomething.org.' mwaka 2012 mwimbaji wa kike wa Pop na Country Taylor Swift ndiye ameshika nafasi ya kwanza akifatiwa na mwimbaji mkongwe wa pop na rock Miley Cyrus.


Taylor Swift alitumia mkwanja mrefu sana kwa ajili ya kutoa misaada ya kibinadamu kwa mwaka 2012 kiasi cha $ 4million, kiasi ambacho hakikufikiwa na celeb yeyote.

Miley Cyrus aliyeshika nafasi ya pili yeye aliitumikia jamii zaidi kwa kusaidi kuelimisha watu wengi zaidi kuhusu utunzaji wa wanyama, lakini pia sapoti yake katika kuinua muziki kupitia kampeni ya "Save The Music Foundation" na "Make-A-Wish Foundation", na hizi ni baadhi tu.

Celebs wengine ambao wameingia kwenye list hiyo ni Lady Gaga, Justin Bieber, Selena Gomez, Demi Lovato, Carrie Underwood, Sofia Vergara, Beyonce Knowles, Jay-Z, Ian Somerhalder, Pink, Ben Afleck na wengine wengi.

Jay Z & Beyonce
Lady Gaga
Unfortunately, Rihanna ambae mwaka huu umekuwa mwaka wake wa mafanikio sana, kiasi cha kuingia kwa mara ya kwanza kwenye Billboard Chat Top 200 na album yake ya 'Unapologetic', na kununua jumba la kifahari la dola million 12. Hata hivyo haimaanishi kuwa hatoi misaada, hata hivi karibuni aliisaidia sana hospitali ya kwao Barbados kiasi cha dola million 1.75 ili kuanzisha kitengo maalum cha kansa.
Justin Bieber
 
Hii ndio list ya top 20 ya celebs waliojitolea zaidi kusaidia jamii:

1. Taylor Swift
2. Miley Cyrus
3. Channing Tatum
4. Lady GaGa
5. Justin Bieber
6. Robin Roberts
7. Pink
8. LeBron James
9. Selena Gomez
10. Ian Somerhalder
11. Jay-Z & Beyonce Knowles
12. George Takei
13. Ben Affleck
14. Andrew Garfield & Emma Stone
15. Ryan Seacrest
16. Demi Lovato
17. Carrie Underwood
18. Olivia Munn
19. Sofia Vergara
20. Drew Brees

Hizi Ndio Sababu Zinazolifanya Kundi La P-Unit Lisivunjike

       
Kundi la P-Unit kutokea nchini Kenya ambalo lionaundwa na wasanii watatu yaani Frasha, Gabu na Bon Eye limeweza kutoa sababu ya wao kutotengana au kuwa pamoja hadi leo. 

Akiongea kwa niaba ya kundi zima la P-Unit, Gabu amesema kuwa P-Unit ni kama familia na wanaheshimiana sana, na sababu kubwa inayo wafanya waendelee kuwa na umoja katika kundi hilo ni mipango thabiti ambayo wamejiwekea, wanatambua tofauti kati ya kazi na urafiki. 

P-Unit kwasasa wanatamba na ngoma yao mpya ya You Guy ambayo wamemshirikisha Collo.

VANESSA MDEE a.k.a V KUUTAMBULISHA WIMBO WAKE MPYA MWAKANI 2013

Baada ya kufanya vizuri katika collabo mbili kati ya A.Y na Ommy Dimpoz aliweza kufahamika  na kupelekea mashabiki wengi kumkubali katika muziki wa Bongo Fleva,Sasa kama unakumbuka siku ziliyopita alifunguka katika ukurasa wake wa twitter na akasema kwamba anatarajia kuachia ngoma yake mpya siku ya tarehe 26 mwezi huu lakini mpaka sasa kimya ni tatizo.

  
Leo kupitia Double XXL aliamua kufunguka na kusema kwamba amekuwa na mambo mengi sana na ndiyo maana akuwa na time ya kuitambulisha lakini ameamua kuchukua uamuzi wa kuitambulisha ngoma yake mpya siku ya tarehe 12 mwakani.Kwa hiyo kama wewe ni shabiki wa Vanessa Mdee kaa tayari kwa ujio mpya kutoka kwake.
 

Uliiona hii!! Chris Brown asema anataka kuondoka kwenye hii dunia baada ya kutoa album yake, je anataka kujiua? soma undani wa habari hii.

'Don't work me up hit maker' ambae amekuwa gumzo kwenye media mwaka huu katika maswala mbalimbali ikiwemo mapenzi yanayotatanisha kati yake na warembo wawili Karruache Tran na Rihanna, ugomvi wake na Drake na mafanikio yake makubwa katika Muziki, alitoa tamko ambalo liliwashtua wengi siku kadhaa kabla ya kusherehekea sikukuu ya Christmas.
 
Chris Brown aliandika kupitia Instagram ujumbe unaoonesha ana machungu sana na hili game la muziki, na kwamba anataka kuondoka katika sayari hii baada ya kuachia album yake ijayo.
Chris Brown aliandika kupitia instagram, "Baada ya hii album nataka kuondoka katika hii sayari."

"Wasanii wa kweli ni viumbe waliojiweka hatarini!" Baada ya hapo aliendelea na maneno yenye ukakasi na yanayoonesha hasira, "This gimmick age is f*cking corny as f*ck! Be you but f*cking get credit for the work u do. Not becuz someone cosigns who knows absolutely nothing about music and culture!"

Chris Brown ambae album yake ya Fortune ilipendekezwa kushindania tuzo za grammy za 55 katika kipengele cha Best Urban Contemporary Album, anatarajia kuachia album yake mpya mwaka 2013 inayoitwa 'Carpe Diem'.

Wengi wanajiuliza inakuaje, Chris ameamua kujimaliza ama anataka kuihama vipi hii dunia, ama ametumia maneno ya kisanii na hana maana ya moja kwa moja ya kuihama hii sayari yenye oxygen inayomsaidia binadamu kupumua.

Hata hivyo Chris Brown aliifuta message yake muda mfupi baada ya kuipost.

Sunday, December 23, 2012

SERIKALI YABEBA JUKUMU LA KUMSAIDIA SAJUKI HADI KUPONA


 
Serikali imechukua jukumu la kumhudumia msanii na muongozaji wa filamu Sadick Juma Kilowolo ambaye anatarajia kuondoka wiki ijayo kuelekea India kwa matibabu.

Katibu wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Wilson Makubi, alisema Sajuki ambaye kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, amegundulika kuwa ana tatizo la kufeli kwa figo na kwamba yuko chini ya uangalizi na uchunguzi zaidi.

Alisema kutokana na hali hiyo, serikali imejitolea kumsafirisha msanii huyo kwa gharama zake na kusaidia katika gharama za matibabu akiwa nchini India.

“Sajuki anatarajiwa kusafiri wiki ijayo baada ya taratibu zote kukamilika, hivyo sisi kama TAFF tunathibitisha kuwa hali yake bado haijatengemaa kama ilivyojulikana hapo awali,” alisema Makubi.

Msanii huyo amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu ambapo mwaka jana alianza na uvimbe ulioanzia mikononi na baadaye ndani ya mwili kwenye ini na sehemu tofauti za tumbo.

Msanii huyo alipelekwa India kwa ajili ya kutibiwa, kisha akarejea nchini baada ya kupata nafuu, ambapo kwa sasa ameugua tena na anahitaji matibabu ya haraka ikiwamo upasuaji.
 

TOP 20 ZA REDIO KITULO FM 23 DESEMBA 2012

20;-Leka Dutigite - Kigoma Allstars(12)
19;-Darasa Huru - MeccaCheka ftn Nakaaya(Ingizo Jipya)
18;-Utamu - Dully Sykes ftn Diamond & Ommy Dimpoz(2 weeks)
17 ;-Bonge la Bwana - Shetta ftn Linnah(19)
16;-Mama Yeyo - G nako ftn Ben Pol(20)
15;-Riziki Tip Top Connection(06)
14;-Let me Go - Keko(17)
13;-Ameen - Mwana FA ftn AY & Dully Sykes(11)
12;-Si kosa Lake - Empowerment Music [EMG](16)
11;-Niache Kido - Nick II,Gnako & Joh Makini(07)
10;-Utarudishwa - Izzo B ftn Belle 9(08)
09;-My everythin' - Ali kiba(15)
08;-Nasemanao rmx - Ney (05)
07;-Nataka kulewa - Diamond(14)
06;-Watasubiri - Mtanashati Ent(04)
05;-Kuwa na subira - Rama Dee ftn Mapacha(02)
04;-Me & U - Ommy Dimpoz ftn Vanessa Mdee 'V'(13)
03;-Nipende - Mr Blue ftn Walter Chilambo(10)
02;-Dear God - Kala Jeremiah(2weeks)
Bonus;-Kesho - Diamond
01;-Kelele - Baucha ftn Ali kiba (2weeks)

Zimeandaliwa na;Ergon Elly
Bye Bye 2012 welcome 2013

Saturday, December 22, 2012

[SONG] BRAND NEW;-KOBA MC - SINA NOMA NAE


Artist;- Koba Mc 

Song ;-Sina Noma Nae

Prod;- GQ

Studio;- DIGITAL VIBES

Special Thanx SAB Multimedia

Morogoro

Contact +255717996666


CLOSER NI NGOMA MPYA YA VANESSA MDEE a.k.a V

   
Baada ya kupiga  collable na wasanii mbalimbali hapa bongo mwanadada Vanessa Mdee ameamuakuja na ngoma yake mwenyewe pina ikumbukwe licha ya kuwa mtangazaji lakini wengi wetu tunamfahamu kutokana na collabo kadhaa alizofanya hivi karibuni kama Money featured by AY, Ommy Dimpoz's Me N You 

Vanessa Mdee a.k.a V. Zaidi au naweza kusema mpya kutoka kwa mwanamuziki huyu ambae pia ni mtangazaji wa kituo cha Redio cha Choice FM cha Dar Es Salaam ni kwamba anafanya ngoma yake ambayoanategemea kuirelease tarehe 28 mwezi huu siku ya ijumaa 2012.

 V ali-tweet kwenye ukurasa wake wa twitter kuhusu wimbo huo ambao utaitwa Closer. Well Vanessa is good at singing... i bet we can all agree on that. Tusubirie hii afu tuone Stay close.

MAANDALIZI YA TOP 50 ZA REDIO KITULO FM 2012/2013

Kwa mdau wa muziki wa kizazi kipya hii inakuhushu kwa kupendekeza ni ngoma/wimbo upi uhusike kwenye Top 50 ya kufunga mwaka 2012 na kuukaribisha mwana 2013 kwa kuandika katika sehemu ya comment au Tuma Ujumbe mfupi wa maandishi yaani SMS kwa simu namba 
0755 894 663. Hizi ni Top 50 za Redio Kitulo Fm na Track hizo zitahesabiwa na Mtangazaji  Ergon Elly pia Matukio mbalimbali yaliyotokea yanayohusu wasanii yatahusika siku ya tarehe  31 Desemba 2012 kuanzia saa tatu kamili usiku mpaka new year 2013

ZIFAHAMU NYIMBO ZILIZOPO KWENYE ALBUM YA KALA JEREMIAH IITWAYO PASAKA

  1.  INRODUCTION
  2. PASAKA
  3. KALA WA MWANZA ft LANGA,SUPLISE & CHANGAS
  4. HALLOW
  5. WAAMBIENI ft ROMA,STIVE RNB & BELLA KOMBO
  6. STREET DANGER ft NEMO,BLACK WA USWAZI, & JOSE MTAMBO
  7. AZIMIO LA ARUSHA ft DOGO SHEBY
  8. MTOTO WA MAMA ft MASTER DO
  9. SABAYA REMIX ft BASHARY
  10. USHAMJU ft NOORAH
  11. ACHANA NAO
  12. MISS FLANI ft LEAH MUDDY
  13. DEAR GOD ft BABY SOFI
  14. VIPII?
  15. NINGEKUWA RAIS ft JOKATE MWENGELO
  16. DEDICATION
  17. WIMBO WA TAIFA ft NAKAAYA SUMARI
  18. NDOTO ft DULLY SYKES
  19. MISS UG ft BIG TYM
  20. DEAR GOD REMIX ft MASHABIKI
  21. WIZI MTUPU
  22. MAMA ALISEMA ft G.SOLLO,FRESH K & QJ
  23. READY TO DIE
  24. MR DJ ft MAGE & SAMIA MSHASHA
KAMA UNAHITAJI HII ULBUM UNAWEZA KUWASILIANA KWA KUPIGA HIZI NO
                +255 659553776 na +255 756799877


Mwanamuziki kutoka Nigeria, Goldie Harvey ashinda tuzo kubwa za Nigeria Music Video Awards [NMVA]

       
 Mwanamuziki kutoka Nigeria, Goldie Harvey ashinda tuzo kubwa za Nigeria Music Video Awards [NMVA] huko Nigeria.  

Goldie ameshinda tuzo hiyo ambapo alikuwa kwenye kipengele cha Utumiaji mzuri wa mavazi [Best Use Of Costumes] kupitia ngoma yake ya Say My Name.

Katika tuzo hizo, Goldie ambae pia ni alikuwa ni mshiriki wa Big Brother Africa [Star Game] iliyopita, alikuwa anashindanishwa kwenye tuzo hiyo na wasanii wengine watatu kutoka hapo hapo Nigeria.

HII NI COVER YA MOVIE YA MAREHEMU SHARO MILIONEA

Hii ndiyo movie mpya ambayo Marehemu Hussein a.k.a Sharo Millionea alikuwa yuko mbioni kuitoa kabla ya kifo kumkuta.

Apumzika kwa Amani.

FAT JOE KWENDA JELA KWA KUKWEPA KULIPA KODI

       
Kiongozi wa kundi la Terror Squad maarufu kama Fat Joe ama Joe Crack ambae hapo nyuma alitamba na baadhi ya ngoma zake kama Lean Back, What's Love, Aint say Nothing na nyingine nyingi.

Sasa latest news kutoka kwa rapper huyo ni kuwa yuko matatani kutokana na kukumbwa na mashtaka ya kudaiwa kodi ya kiasi cha dola za kimarekani $1 Million ambazo ameshindwa kulipa katika pato la taifa la mwaka 2007 na 2008

Fat Joe kwa sasa yupo huru kwa dhamana ya dola za kimarekani $250 hadi hapo atakapo kuja kusomewa tena hukumu yake hapo April mwakani.

KOIKOI NI UJIO MPYA WA MSANII OMMY DIMPOZ

   

Msanii anaefanya vizuri na kazi zake kama "Me & Una zingine si mwingine ni Ommy Dimpoz akaribia kuachia ngoma yake nyingine kwa fans na inawezekana ikawa funga mwaka 2012.
       
Ommy ambae kwa sasa anatamba na wimbo wake wa 'Me N You' ambao amemshirikisha Vanessa Mdee a.k.a V hivi amesema yupo karibu kuachia kamba hiyo inayokwenda kwa jina la Koikoi

Hivyo kama we ni shabiki mkubwa wa Ommy Dimpoz basi kaa tayari kwa kuisubiria ngoma yake hiyo inayofuata na kama kawaida jamaa huwa hakosei katika kazi zake.
     
Ommy Dimpoz ni msanii mwenye chimbuko la Kigoma aliyeanza kuvuma kwa kasi alipo-release ngoma yake ya kwanza inayofahamika kama Nai Nai ikimshirikisha AliKiba na baada ya hapo akaachia Baadae  ambayo pia ilifanya na inafanya vyema redioni na kwenye TV

KESI YA ELIZABETH 'LULU' MICHAEL IMEHAMISHIWA MAHAKAMA KUU NA HIVYO HAJATOKA KWA DHAMANA KAMA ILIVYO RIPOTIWA HAPO AWALI



Awali habari zilizoandikwa kuwa lulu atasherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka akiwa nje lakini mambo yamekuwa sivyo kama ilivyoandikwa na hivi ndivyo  mambo yamekuwa.

 Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu ya jijini Dar es Salam leo imefunga jalada la kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili msanii wa Filamu nchini ELIZABETH MICHAEL maarufu kama LULU tayari kwa kulipeleka mahakama Kuu ya Tanzania ili kesi hiyo ianze kusikilizwa.

Kabla ya kuanza kusomwa kwa maelezo ya kesi hiyo ambapo LULU hakutakiwa kujibu lolote kutokana na mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, Hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu AUGUSTINA MMBANDO amemtaka wakili wa Serikali kutaja idadi ya mashahidi watakaotoa ushahidi wao wakati kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa.

Wakisoma kwa awamu maelezo ya mashahidi wa kesi hiyo Mawakili wa Serikali katika kesi hiyo wamesema kuwa wanao mashahidi Tisa wanaotarajia kuwatumia kwenye kesi hiyo na kubainisha kuwa shahidi namba moja katika Kesi hiyo ni SETH BOSCO kijana aliyekuwa akiishi na marehemu STEVEN KANUMBA.


 Katika maelezo ya SETH yaliyosomwa mahakamani hapo imeelezwa kwamba siku ya tukio KANUMBA alimtaka asitoke ili watoke pamoja lakini ilipofika majira ya saa tano usiku alisikia vurugu chumbani kwa KANUMBA ambako alikuwa na mpenzi wake ELIZABETH MICHAEL na baada ya muda alibaini kulikuwa na ugomvi baina ya wawili hao huku mlango ukiwa umefungwa.


Maelezo hayo yamesema kuwa baada ya muda LULU alitoka chumbani kwa KANUMBA na kumtaarifu kuwa KANUMBA ameanguka ndipo aliingia chumbani na kumkuta akiwa ameegemea ukuta pembezoni mwa mlango huku povu likimtoka mdomoni na kuamua kumlaza chini kabla ya kuomba msaada.


Mashahidi wengine wanaotarajia kutoa ushahidi wao wakati kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa ni SOPHIA KASSIM mmiliki wa nyumba aliyokuwa akiishi KANUMBA, Madaktari watatu, maofisa wa polisi watatu, afisa uhamiaji ambaye ni shemeji wa KANUMBA na MORIS SEKWAO kijana aliyempakia LULU kwenye gari yake muda mfupi kabla ya kukamatwa.


Baada ya kusomwa kwa maelezo ya mashahidi wote wakili huyo wa Serikali amesoma maelezo ya LULU na kubainisha kuwa walianza uhusiano wa kimapenzi Januari mwaka huu ambapo walikuwa na kutokuelewana katika baadhi ya nyakati hasa pale mmoja anapompigia mwenzake simu na kutopokelewa kwa wakati.


 Baada ya maelezo yote kutolewa na kukamilika Hakimu wa Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu AUGUSTINA MMBANDO amezishukuru pande zote na kumkata LULU atoe maelezo ya nyongeza kama anayo ambapo LULU alisema hana maelezo yoyote.


Hakimu MMBANDO amemtaka LULU kuendelea kubaki Lumande mpaka hapo tarehe ya kesi itakapotajwa na mahakama Kuu ya Tanzania.

Friday, December 21, 2012

Hawa ni Waigizaji wa Bongo Movie waliofanya vizuri mwaka 2012


 

TAZAMA BAADA YA MH. GODBLESS LEMA KUSHINDA RUFAA NA KURUDISHIWA UBUNGE WAKE


Mbunge wa Arusha Mjini-CHADEMA,Mh Godbless Lema akiondoka kwa staili ya maandamano Mahakamani leo baada ya kushinda katika rufaa ya kesi yake ya kupinga matokeo, iliyosomwa jijini Dar es Salaam leo kushoto kwake ni katibu wa Chadema mkoa wa kinondoni na katibu wa kuteuliwa wa kanda maalum ya Dar es salaam Henry Kilewo
  
Mwekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai, Mh Freeman Mbowe(wa pili kulia)akiteta jambo na Mbunge wa Arusha Mjini(CHADEMA)MH GODBLESS Lema ndani ya mahakama leo asubuhi muda mfupi kabla ya rufaa ya kesi yake ya kupinga matokeo iliyosomwa jijini Dar es Salaam leo kutolea hukumu na kuamuru lema kuwa ni mbunge Halali wa Arusha Mjini wa Pili kushoto ni Mbunge wa Arumeru Mashariki(CHADEMA)Mh Joshua Nasari na wa kwanza kushoto ni katibu wa Chadema mkoa wa kinondoni na katibu wa kuteuliwa wa kanda maalum ya Dar es salaam Henry Kilewo
  
Kutoka kushoto ni Mke wa Mbunge wa Arusha Mjini(CHADEMA)Godbless Lema,katibu wa kuteuliwa wa kanda maalum ya Dar es salaam Henry Kilewo,Mbunge wa Arumeru masharii Joshua Nasari,Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe wakiwa mahakama ya rufaa leo asubuhi muda mfupi kabla ya hukumu ya kesi ya kutolea
Mawaikili wakiwa kwenye viti vyao leo muda mfupi kabla ya hukumu ya kesi ya lema kutolewa asubuhi hii
Baadhi ya watu mbalimbali waliofurika mahakamni leo kusikiliza hukumu ya Lema
 Wakili Machachari na Mbunge wa Singida Vijijini(CHADEMA) Tundu Lissu ambae alikuwa mtetezi wa Mbunge wa Arusha Mjini(CHADEMA)Godbless Lema ambae aliingia kwenye kesi upande wa utetezi baada ya kesi kufika mahakama ya rufaa akiongea machache baada ya hukumu hiyo.watu mbalimbali walimshangiliwa sana leo

Labels