Pages

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Thursday, January 31, 2013

DIAMOND AMKAMATA MMOJA WA WACHAWI WAKE

 
Zikiwa zimepita siku 29 tangu alipofanyiwa vurugu za kutosha msanii anayetamba na kazi yake ya Kesho si mwingine Diamond wakati wa show yake aliyokuwa akiifanya ndani ya Maisha Club na kusababisha watu kadhaa kuumia na  chupa kurushwa pamoja na mayai viza.
 
Huku akiachwa bila ya cheni ,saa wala miwani aliyokuwa amezivaa na kuambulia boooooo kibao siku ya jumamosi Diamond alipokuwa akielekea Kigamboni kwenye show aliyokuwa anaifanya huko akiwa na msanii Z Anto alifanikiwa kumkamata mmoja wa walioanzisha vurugu hizo akiwa ndani ya pantoni nae akielekea kigamboni

msikilize Diamond hapo chini, akiwa na Gossip Cop Sudy Brown kwenye UUUUUU HEEEAAARRD

CHRIS BROWN AJITOA INSTAGRAM

 
Msanii Chris Brown, ameamua kujitoa katika mtandao wa instagram, siku ya jana, baada ya kuona mambo hayaendi sawa, inawezekana ni kutokana na comment za mashabiki  kwa kile alichokua anakituma na kukiandika, kabla ya kujtoa aliamua kuandika ujumbe huo hapo juu.

Rapper na Producer Timbaland amesaini mkataba na Record lebel ya Jayz `Roc Nation'

http://api.ning.com/files/W-cvbOicaVXfNoWx1lbtOjQo5qTEd67eYXeGWbq2PUxrXLFSUF-WVcUdVZhg1XWsGPwRgrogOh4G5OgzsRbe5nYv0GmVHz67/jayz.jpg 
Rapper na Producer Timbaland amesaini mkataba na Record lebel ya Jayz `Roc Nation' unaomtambulisha kama msanii chini ya lebel hio.

Jay-Z ametangaza habari hizi kwenye mtandao wake wa Life + Times kuwa Timbaland yupo chini ya Roc Nation na wanamkaribisha sana.

 Jayz na Timbaland wamefanya kazi Pamoja kwa Muda Mrefu, kama unakumbuka mwaka 1998 Timbaland alitengeneza wimbo wa Nigga What ,Nigga Who , Wakaja tena kufanya Big Pimpin ,Dirt Off Your Should na Off That ft Drake.

Kazi ya Mwisho Timbaland amefanya na Jay z ni Wimbo wa Justin Timberlake ft Jay z – Suit And Tie. Mpaka sasa wasanii kama M.I.A ,Meek Mill, Elijah Blake na Jahlil Beats.

Jenga Picha Jay z na Timbaland wakiwa Studio wanatengeneza Beat Kwa ajili ya Timbaland.Nomaa. 

Wednesday, January 30, 2013

HII NDIZO TOP 10 ZA REDIO KITULO FM [25 JANUARY 2013]

10:-Ngoma Moja - Team Racerz
09:-Utamu - Dully ftn Diamond & Dimpoz
08:-Sina Noma naye - Koba MC
07:-Mtu wa watu - PNC ftn  Janjaro,Z anto,Pingu & Kassim
06:-Kinyulinyuli - Samir
05:-Listen - Belle 9
04:-Jambo jambo - Steve RnB
03:-Bonge la Bwana - Shetta ftn Linnah
02:-Kesho - Diamond
01:-Wazo la leo - StaminA ftn Fid Q

Monday, January 28, 2013

Video Ya PRESS PLAY Kutoka Mwisho Wa Mwezi Huu...

     Hivi karibuni tuliona picha za Director Nisher kutoka Nisher Entertainment kutoka A-Town akishuka Bongo, DSM kwa ajili ya kurekodi video ya ngoma mpya ya DJ Choka a.k.a Mr. ApetitePRESS PLAY. Nisher alitua na mzigo ukafanyika, sasa mpya ni kwamba video hiyo itatoka mwisho wa mwezi huu... inayofahamika kama
    
 Ujumbe huo kuhusu video hiyo iliyomuweka Nisher hapa Bongo zaidi ya wiki, ulitoka katika uongozi wa BHitz music Group kupitia ukurasa wao wa Twitter ikiandikwa, "Press Play Video Official Release 31.1.13" yaani mwisho wa mwezi huu wa kwanza wa mwaka....
Track hiyo inayoshirikisha wasanii wakali kutoka BHitz, kama Deddy, M-Rap, Vanessa Mdee, Mabeste na Gosby inataraji kudosha kichupa hicho tarehe hiyo... Tusubiri tuone.

BREAKING: PICHA 8 ZA LULU MAHAKAMANI LEO JAN 28 PAMOJA NA MAELEZO YA MASHARTI YA DHAMANA YAKE.


Lulu akiwa anaingia Mahakamani leo january 28 2013 akiwa na shauku ya kupata dhamana.
Mahakama kuu leo imetangaza dhamana ya mwigizaji Lulu lakini iwapo atatimiza masharti aliyopangiwa ambayo ni pamoja na kuwasilisha hati yake ya kusafiria, kutosafiri nje ya Dar es salaam, kujiwakilisha au kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza ya kila mwezi pamoja na wadhamini wake wawili ambao kila mmoja adhamini kwa shilingi milioni 20 za kitanzania.
Upande wa familia ya Lulu umesema masharti yote yaliyotajwa wanaweza kuyatimiza leo leo hivyo wanasubiri tu jibu la msajili ambae ndio anatakiwa kuhakikisha hayo masharti yametimia kisha ruhusa ya kumkabidhi Lulu kwa familia yake itolewe.
Taarifa za ndani ni kwamba uwezekano wa Lulu kuachiwa upo kuanzia january 29 2013 ambayo ni kesho kwa sababu kuna watumishi wawili wa serikali ambao wapo kikazi mkoani Pwani na ndio walitakiwa kutia saini dhamana ya Lulu wakiwa ni sehemu ya masharti.
.
.
.
.
Hapa ni wakati alipocheka sana pale mwandishi mmoja wa kike ambae pia alikua akimpiga picha alipokua akimlainisha Lulu kwa maneno baada ya mwigizaji huyo kuficha uso wake alipokua akipigwa picha, alisema alikua anaumizwa macho na mwanga wa kamera.
.
.
Mama mzazi wa Lulu ni mwenye nguo nyeupe na nyeusi.
Unaweza kumsikiliza mwigizaji Dr Cheni hapo chini, ni mmoja ya watu waliokaribu na familia ya Lulu na ameshirikiana nayo kwa muda mrefu sana kwenye hii kesi ikiwemo kufatilia mawakili, kushughulikia dhamana na mengineyo.

DR CHENI;NIKO TAYARI KUMTOLEA LULU DHAMANA YA SHILINGI MILIONI 20


cheni
Muigizaji wa Bongo Movie Dr. Cheni amesema yeye ni miongoni mwa watu walio tayari kumdhamini muigizaji mwenzie Elizabeth Michael maarufu kama Lulu ambaye leo hii mahakama kuu ya Tanzania imempa nafasi ya dhamana.
Lulu ambaye kwa zaidi ya miezi saba yupo mahabusu katika gereza la Segerea anakabiliwa na kesi ya mauaji dhidi ya marehemu Steven Kanumba.

Akiongea na Clouds FM leo katika mahakama kuu ya Tanzania ambapo kesi hiyo inasikilizwa, Dr Cheni ambaye yupo karibu na familia ya Lulu katika kipindi chote cha kesi hiyo amesema masharti yote ya dhamana hiyo yanatekelezeka.

“Kwa mfano kama hiyo wamesema kwamba kuna dhamana ya milioni 20 na mtu mwingine milioni 20 mimi ninaweza nikajitoa katika mmoja wapo katika upande huo,” alisema Cheni.

“Masharti mengine sidhani kama ni magumu kwasababu kila kitu kiko okay sidhani kama kitashindikana sasa hatujajua msajili atakapopata anatoa leo ama atamtoa lini sababu na yeye lazima apate muda wa kupitia yawezekana ana mafaili mengi juu ya meza.”

Cheni amesema masharti hayo yaliyowekwa wanaweza kuyatimiza leo hii. Masharti mengine ya dhamana hiyo ni pamoja na Lulu kurudisha hati yake ya kusafiria, haruhusiwi kutoka nje ya Dar es Salaam na atatakuwa kuripoti mahakamani kila siku ya kwanza ya mwezI

Wednesday, January 23, 2013

[AUDIO] IZZO B ftn QUICK ROCKER,NGWEA & RUTH - BALL PLAYER

PROMISE NI UJIO MPYA WA MSANII WA KIKE TZ SHAA

       
Staa Sara Kaisi Msanii wa Bongo Flava  Shaa anayewakilisha vizuri Tanzania Kupitia Muziki baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu Baada ya kuachia single yake ya Mwisho Siri Ya Penzi na nyingine nyingi Siku Ya tarehe 28.01.2013 Ataachia single yake mpya inayokwenda kwa jina la ''PROMISE''.

Ngoma hiyo ambayo mashahiri yake yameandikwa na Barnaba na kutayarishwa na ProducerManeck wa Am Records. Shaa ametupia cover ya ngoma hiyo kupitia ukurasa wake wa Facebook "#Promise #NewSingle By Shaa Official release date is 28/01/2013...
will provide a link for both the audio and video #Photography by Slide VisualsGongaMX ilipata nafasi ya kushiriki kwenye uchukuaji video wa single iyo ambayo imefanywa na Adam Visuals LAB. Endelea kuwa nasi ili uweze kuona picha the behind a scene.

NISHER:NASHUKURU MUNGU NIMEMALIZA KUTENGENEZA VIDEO MPYA"PRESS PLAY"

Baada ya kuwasili hapa Dar kwa ajili ya kutengeneza video mpya ya Dj choka kutoka B hits inayofahamika kwa jina la Press Play,sasa leo kupitia katika akaunti ya Nisher aliandika ujumbe na kusema kwamba wamemaliza jana ku shooting video mpya ya "Press play"
Huu ndiyo ujumbe kutoka katika ukurasa wake wa Facebook

[LYRICS] BELLE 9 - LISTEN

Verse 1:                                                     
 
wakufunzi wengi manguli wa mapenzi
ila mi sitaki nataka kwako
wakufunzi wengi manguli wa mapenzi
girl eeeh eeeh oooh
nitaridhika baby na penzi lako wewe nataka kwako ooooh
nitaridhika baby na penzi  lako wewe nataka kwako oooh
 
listen up listen up
ma baby
listen up listen up
nieleweeeee *2
 
Chorus:
 
nimefal in love baby fal in love
nimefal in love baby fal in love
 
listen up listen up
ma baby
listen up listen up
nieleweeeee *2
 
Verse 2:

huu sio wimbo ila hii ni zawadi yako zawadi zawadi kwako
safari yangu ya mapenzi naomba iishie kwakoooo
nitaridhika baby niwe wako uwe wangu
me sitaki kuwa kama yule i i i i want to give you true love
 
listen up listen up
ma baby
listen up listen up
nieleweeeee *2
 
nimefal in love baby fal in love
nimefal in love baby fal in love
nimefal in love baby fal in love
nimefal in love baby fal in love

Tuesday, January 22, 2013

Manager wa Rapper Game amesema yupo kwenye mchakato wa kurudisha kundi la G-Unit kama wasanii, 50 Cent na Game wata weka tofauti zao pembeni na kutengeneza pesa kwa pamoja .

Manager wa Rapper Game amesema yupo kwenye mchakato wa kurudisha kundi la G-Unit kama wasanii, 50 Cent na Game wata weka tofauti zao pembeni na kutengeneza pesa kwa pamoja .
 
Fahamu Ni takribani miaka kumi toka umemuona 50 Cent na Game waki share mic na Manager Dontay "Taydoe" Kidd amesema  50 Cent anajua hakuna G Unit bila game na Game anajua G Unit haiwezi kufanya vizuri bila yeye kwa sasa.
 
Dontay anategemea kutengeneza pesa nyingi kama G Unit litarudi tena kufanya kazi pamoja kwani walikuwa na mashabiki sana . 
 
Dontay alisema wakirudiana tu atahamisha jitiada zake kwenye bidha za G Unit kama T Shirt , viatu ,kofia , na mpaka simu za G Unit.

Rapper Izzo Bizness amesema Ball Player Inaanza Audio na ni mara ya kwanza kufanya wimbo na watu watatu.


Rapper Izzo Bizness amesema Ball Player Inaanza Audio na ni mara ya kwanza kufanya wimbo na watu watatu.

Izzo amesema ameamua kubadilisha style kidogo kwani ingekuwa ni  marudio ya kazi alizozifanya mwaka jana .

Wimbo unatoka kesho na WaTanzania ndio wataamua kama ni ujio mzuri wa Izzo au Akajipange tena .

Kwenye wimbo huu ataskika kwa mara ya Kwanza Msanii Ruth aliyefanya Chorus,Izzo amesema kuwa beat ya Ball Player imetengenezwa na Nahreel huku vocal na final mixing ikafanywa na Lamar wa Fish Crub.

Amesema wazo la kuja na wimbo wenye jina la ‘Ball Player’ ni kulinganisha juhudi za mchezaji mpira awapo uwanjani ambaye huwa na pilila pilika muda wote na jinsi ya kutumia mfano huo katika maisha ya kawaida. 

Amejitolea mfano yeye wakati anakuja Dar es Salaam kutokea Mbeya alifikia kwa washkaji lakini kwa sasa anaishi kwake mwenyewe kutokana na juhudi zake katika kutafuta maisha.

BEN POL ATENGUA MSIMAMO WAKE WAKUTOTAKA FANYA COLLABO NA WASANII WENGINE



Kama unakumbuka vizuri mwaka jana Ben Paul alisitisha kufanya Collabo na msaani yoyote mpaka February 3, 2013, Lakini hapa katikati tumeskia Yatakwisha ft Linnah, Lord Eyes ft Ben Paul - No More Drama na Mama Yoyo Aliyoshirikishwa na G Nako.
Leo Ben Paul ametengua kaulia yake kuhusu kusitisha kufanya collabo na kusema atakuwa akifanya collabo kwenye Ngoma nzuri .
Ataangalia Potential ya Msanii ,Wimbo wenyewe na Production. Ben alisema ata International artist wanafanya collabo nyingi ila hawashuki kwa sababu wanazingatia Mambo hayo.

Kuhusu wimbo wake wa kwanza kutoka mwaka huu Ben amesema `Jikubali' Inamuhusu mtu anaye Weka Tofauti kati yake na watu wenye mafanikio, watu maarufu na ata wanasiasa. 
Hii ngoma itamuhamasisha afanye vizuri kwenye jambo analolifanya ,kama ni kazi , elimu ,sanaa au chochote. 
Huu wimbo unampa nafasi yakujiona ni mtu mwenye uwezo wakufanya kazi nzuri na akafanikiwa na kusaidi familia yake. Mtu huyo atuone sisi kama watu wa kawaida. Wimbo unatoka Kupitia Video kwanza alafu audio ndio itafata.

Monday, January 21, 2013

Lady Gaga Kupiga Show Kwenye Tamasha La Kumpongeza Rais Barack Obama

       
Tamasha la Barack Obama lililokuwa limepangwa kufanyika january 19 lilisogezwa mbele hadi january 22 na badala yake likafanyika tamasha la family friends wa familia ya Obama.

The pop star Lady gaga amepata shavu la kupiga show kwenye tamasha la january 22 ambalo litakua linamhusu Barack Obama na timu yake ya kampeni ikiwa ni kumuintroduce tena Ikulu.

The Mother Monster amefuata nyayo za Jay-Z ambae alifanya tamasha kama hili mwaka 2009 baada ya ushindi wa Obama kwa awamu ile ya kwanza, ambapo Roc Nation president Jigga alibadilisha wimbo wake wa 99 Problems hasa kwenye chorus na ikasikika akimalizia kuwa but Geoge Bush Aint One. 
 
Wimbo aliubadilisha hata kipindi cha kampeni za kumsapoti Obama mwaka jana na aliibadili chorus hii na kusema but Romney Aint One.

Gaga alikua anamsapoti sana Obama katika concert kibao alizokua anapiga licha ya kuwa kuna wakati baadhi ya watu walisusia concert na kuondoka baada ya yeye kuanza kumpigia debe Obama.

Atafanya nini katika tamasha la kesho, The Mother Monster anajulikana kwa surprise kibao akiwa stage na ya kesho haijulikani itakuaje mbele ya Barack Obama.

Justin Bieber ashusha boxer na kuonesha makalio yake,ni bangi au hajazoea utu uzima?! Iangalie hapa



Pop and R& B star Justin Bieber amewashangaza fans wake walioshindwa kutafsiri nini chanzo cha haya yote, baada ya kupost picha inayomuonesha kwa nyuma akiwa ameshusha boxer kama sio chup* akiwa na lengo la kuonesha makalio.

Bieber amepost picha hiyo kwenye Instagram na baada ya muda mfupi akaamua kuifuta, lakini tayari watu kibao walikuwa wameshaidownload na imezagaa kwenye mitandao kibao. Mwimbaji huyo ambae ndo kwanza amefikisha umri wa kiutu uzima (18) hakuandika chochote kwenye picha hiyo na ni kama aliwaachia watu waseme.

Picha hii ambayo imesambaa kwenye mitandao inawashtua zaidi watu ambao walikuwa bado wanashangaa picha ya Bieber akiwa anachoma majani a.k.a marijuana kwenye chumba cha hotel akiwa na washikaji zake akiwemo rapper mwenye umri mdogo "Lil Twist".

Kwa haya matukio mawili ya haraka haraka unaweza kujiuliza ni bangi, kama kweli anavuta, ama ndo vile he is young and wild and free!!

Lakini Bieber sio peke yake aliyepost picha ya aina hii, mwaka jana Justine Timbalake nae alipost picha kama hii alipokuwa ameenda tour kwa ajili ya Bachelor party kabla ya ndoa yake na mkewe wa sasa Jesica Biel.

BALL PLAYER NI UJIO MPYA WA HIP HOP ICON KUTOKA MBEYA "IZZO B" JUMATANO HII

 
Jumatano hii mashabiki wa Izzo Bizness wategemee kitu kipya kutoka kwake. 

Rapper huyo ambaye jina lake halisi ni Emmanuel Simwinga anatarajia kauchia single yake mpya iitwayo ‘Ball Player’ aliowashirikisha Quick Rocka na Ngwair.

Izzo amesema kuwa beat ya Ball Player imetengenezwa na Nahreel huku vocal na final mixing ikafanywa na Lamar wa Fish Crub.

Amesema wazo la kuja na wimbo wenye jina la ‘Ball Player’ ni kulinganisha juhudi za mchezaji mpira awapo uwanjani ambaye huwa na pilila pilika muda wote na jinsi ya kutumia mfano huo katika maisha ya kawaida. 

Amejitolea mfano yeye wakati anakuja Dar es Salaam kutokea Mbeya alifikia kwa washkaji lakini kwa sasa anaishi kwake mwenyewe kutokana na juhudi zake katika kutafuta maisha.

Sunday, January 20, 2013

SARAH LENORE ASAINI KATIKA LEBEL YA CASH MONEY RECORD LEBEL


YMCMB ni group linaloendelea kukuwa kila siku ,hivi sasa Birdman na Slim maboss wa kundi hilo kum-sign mshiriki wa shindano la  'America's Got Talent' Sarah Lenore katika label  yao ya Cash Money record label. 


Sarah Lenore,ni muimbaji kutoka Detroit ambaye alishiriki katika kipindi cha America's Got Talent' kinachorushwa na television ya  NBC hiki ni kipindi cha tv cha kutafuta vipaji vya waimbaji , ameshakubaliana kujiunga na YMCMB  

sarah anasema kwa miaka kadhaa amekuwa akipata nafasi yaku-sign na record labels tofauti tofauti lakini hakuwa tayari ,lakini nafasi hii alioipata anazani ni njia muafaka kutambulishwa katika music industry chini  Cash Money Records. 

Hakuna  njia nzuri ya kunitambulisha kwenye music industry zaidi ya ku-sign kwenye label kubwa ,na nafasi ya kufanya kazi na  Birdman ,Slim na team nzima ya YMCMB nifaida kubwa

Baada ya maneno hayo kutoka kwa sarah ,Birdman hakukaa kimya amemzungumzia kwa kusema, "Sarah ni star kwa kila neno ,ni mtumbuizaji wenye nguvu na anasauti nzuri   . My brother Slim na mimi tunamipango mikubwa sana juu yake ‘’amesema birdman.

PICHA:-RIVER CAMP MASKANI KWA WASANII JOH MAKINI,NIKI WA2,BONTA ARUSHA

Kwenye picha ni Ras Omega ambaye ni moja ya waanzilishi wa River Camp na msanii Nikki Wa pili(Mdogo wa Joh Makini)wakiwa sehemu ya kuingilia ya maskani hiyo iliyopo maeneo ya Uzunguni Arusha.
humo ndani kuna matunda ya kila aina
Kuna aina ya mboga tofauti tofauti kama unavyoona pichani hizo ni moja ya mboga ambazo nazipenda sana 'Salad' na niliambiwa kuwa kabla ya Joh Makini kuingia kwenye muziki alikuwa na vitalu vyake kadhaa yaani analima hizo mboga.

Nilifurahia mazingira ya asili ya maskani hiyo ambayo katika maskani zote Arusha nilizotembelea hii imetisha zaidi kwa mazingira mazuri.S/O kwa Nikki wa pili na Ras Omega mmetisha sana

PICHA:DIAMOND AKITANGAZA LIVE KIPINDI CHA COUNTDOWN NDANI YA CHOICE FM


Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa msanii wa Bongo Fleva maarufu kama Diamond Platinumz kwa kuwasha kipaza sauti na kuendesha show ya redio kwa masaa mawili live ndani ya choice Fm 102.5 Fm.


[Coming Soon] Video Ya ''KI-UTU UZIMA'' Ya Joh Makini Kuachiwa Hivi Karibuni.

      
Msanii wa Rap/Hip-Hop Joh Makini ambaye anatokea kwenye kundi la Weusi, na kufanya vizuri na baadhi ya ngoma zake kama Bye Bye, Stimu Zimelipiwa na nyingine nyingi, hivi karibuni ataachia video yake mpya inayokwenda kwa jina la ''KI-UTU UZIMA'' ambapo mzigo mzima umesimamiwa na kampuni ya I-View Studios.

R.O.M.A Aeleza Maana Ya Mistari Hii Ya 2030


    Mida flani ya leo mchana, msanii maarufu anaetamba na track yake mpya ya 2030, Roma Mkatoliki amefanya kutoka maana ya ya baadhi ya lines zilizo katika ngoma yake mpya hiyo kupitia ukurasa wake wa facebook.
ROMA mwenye mistari mikali iliyokaa kimapinduzi, alianza na ule unaouuhusu mji wa Tanga, akiwaambia wana Tanga "TANGA MMEKOSA NINI, AMKENI ACHENI UMWINYI, HAWA WACHAGA HAWATUWEZI ONA MANKA BARA 20"
  R.O.M.A aliendelea kuachia maana hizi, na kuhamia kwenye huu "UNAPEWA CONTENA LA CONDOMS UIHONGE DHAHABU, MV SPICE ILIPOZAMA TV INAONESHA TAARAB" na kuelezea maana yake hapo chini,..

AMAZONI AJITOA KATIKA KUNDI LA MTANASHATI ENT

         
Msanii wa muziki wa kizazi kipya maarufu kama Amazon ameweka wazi kuwa amejitoa Watanashati Entertainment, kwa kile alichodai kuwa Bosi wa kundi hilo ambae ni Hustadhi Juma Na Musoma, alikuwa anataka kumpa mkataba wa milele kitu ambacho kimemfanya Amazoni aone kama ni lengo la kummaliza kimziki.
         
Amazon alisema kujitoa kwake ni kwa roho safi lakini amesikitishwa sana na Bosi huyo kutaka kumpa mkataba wa milele ambao utambana yeye kutokufanya kazi nyingine. Pia aliongeza kwa kusema kuwa kutokana na hilo kwa sasa atakuwa akifanya muziki kivyake hadi pale atakapo pata meneja mpya wa kuweza kusimamia kazi zake.

TOP TWENTY ZA REDIO KITULO FM 20/01/2013

20:-Kesho - Diamond Platnumz(Ingizo Jipya)
19:-Wazo la Leo - Stamina ftn Fid Q(Ingizo Jipya)
18:- 2030 - Roma ftn Story(Ingizo Jipya)
17:-Mapenzi - Rich Mavoko (20)
16:-Zilipendwa - Matonya (14)
15:-Kidela - Abdul kiba(17)
14:Let me Go - Keko (12)
13:-Mtima wangu - Amin ftn Linnah (10)
12:-kunatatizo kwenye nafasi hii wadau
11:-Nimerudi - Chid Beenz ftn Dully 
10:-Darasa Huru - Meccacheka ftn Nakaaya (06)
09:-Kelele - Baucha ftn Alikiba (08)
08:-Utamu - Dully ftn Diamond & Ommy (11)
07:-Kinyulinyuli - Samir (03)
06:-Si kosa Lake - EMG (09)
05:-Mama yeyo - G nako ftn Ben Pol (05)
04:-My everythin' - Alikiba (02)
03:-Me & U - Ommy Dimpoz ftn Vanessa Mdee "v"(07)
02:-Dear God - Kala Jeremiah (01)
Bonus:-Ngoma Moja - Team Racerz
01:-Bonge La Bwana - Shetta Ftn Linnah (03)

Jumapili njema!!!

Labels