MSANII maarufu wa Hiphop nchini, Khamis Mwinjuma au maarufu Mwana FA,amesema muziki kwake ni kazi na sababu inayomfanya kila siku azidi kung’ara ni ubunifu alionao ambao humfanya kuwa tofauti na wenzake.
Akizungumza na mwandishi wa makala hii alisema,muziki ni kazi
hivyo inabidi kila siku kufikiria vitu mbalimbali ambavyo atawaletea
mashabiki wako ili wazidi kumpenda na kumfanya kutochuja katika
muziki”muziki ni kazi hivyo mara nyingi nimekuwa najaribu kubuni aina
mbalimbali zaa maneno ili niwe tofauti,kama Unanitega,Bado niponipo na
mengine mengi tu,ilio tu yawe mapya kwa mashabiki”.
Akielezea historia yake alisema,muziki alianza toka mwaka 1993
ambapo alifanikiwa kuanzisha kundi ambalo lilikuwa linaitwa,Crew Black
Skin na katika kundi hilo alikuwa na marafiki zake wawili ambao ni
Robilus na Getheerics.
Mwana FA alikutana na marafiki zake hao kipindi wakiwa katika
shule ya Umumio Islami High School,kwani wote kwa pamoja walikua
wanachukua masomo ya Sience.
Mnamo mwaka 2000 alifanikiwa kutoa nyimbo yake ya kwanza
iitwayo”Ingekuwa vipi”ambayo alimshirikisha Juma Mchopanga”Jay
Moe”ambayo ilifanikiwa kufanya vizuri kwa kiasi kikubwa.
Baada ya
nyimbo hiyo alifanikiwa kutoa nyingine kama “Mi na mabinti””Show
time”,aliyomshirikisha Ambwene Yessaya”AY,Alikufa kwa ngoma,ambayo
alikuwa amemshirikisha Judith Wambura”Lady jay Dee”.
Mwana falsafa
kwa mara ya kwanza alifanikiwa kupata tuzo ya Kilimanjaro Music Awards
mwaka 2003 kupitia wimbo wake wa,Alikufa kwa ngoma,ambao ulichaguliwa
kuwa wimbo bora.
Baada ya kupata tuzo hiyo alitoa albamu ya
kwanza iitwayo Mwanafalsafani,ambayo alisema ilifanikiwa kufanya vizuri
na hivyo kupata hamasa ya kuendelea kufanya Albamu nyingine ambapo mwaka
uliofuata mwishoni alitoa Albamu ya Unanitega,ambayo pia mwaka 2006
ilimpatia tuzo ya Albamu bora ya Hiphop.
Mnamo mwaka 2007 pia
mwana FA akiwa ameshirikiana vizuri na AY,walifanikiwa kupata tuzo
kupitia wimbo wao wa “Habari ndio hiyo”kuchaguliwa kuwa wimbo bora wa
mwaka”nilifurahi sana baada ya kupata tuzo,kwani naamini kila kazi
mwisho huwa na mshahara,tuzo ni heshima na ilinipa hamasa kwa kiasi
kikubwa sana ya kuzidi kuongeza juhudi katika fani hii na kuzidi kuwa
mbunifu”.
Mwana FA ambaye alizaliwa mwaka 1984,kwa kushirikianna
na rafiki yake wa karibu,Ambwene Yessaya walifanikiwa kutoa Albamu moja
iitwayo”Habari ndio hiyo”,ambayo ndani yake kulikuwa na nyimbo kama“Kula
kwa macho”waliyomshirikisha msanii kutoka nchini
Uganga”Talia”,”Asubuhi”ambayo walimshirikisha Abubakar Katwila “Q
chief”,”Fungua champagne”,”Nangoja ageuke”,”Bounce”,na “Umejuaje”.
Mwana
FA hadi sasa tayari ana albamu nne ambazo tayari ameshazitoa,ila kwa
sasa amesema albamu hazina faida hivyo yeye atakuwa anatoa nyimbo tu na
kufanya maonyesho,kwani anaamini kipato kikubwa kipo katika
maonyesho”Kwa sasa sina mpango wa kutoa Albamu kwa sababu unajua
hailipi,tumekuwa tunaibiwa sana kiasi kwamba mtu unafanya kazi kubwa ila
mwisho wa siku faida haionekani”Albamu hizo ni Mwanafalsafani,Toleo
lijalo,Unanitega,Habari ndio hiyo.
Akizungumzia mafanikio ambayo
ameyapata hadi sasa anasema ni makubwa sana kiasi kwamba hana budi
kumshukuru sana mungu kwa alipofikia kwani hakutaraji kama atafika ila
pia bado anazidi kumuomba mungu,kila siku azidi kumpandisha juu zaidi ya
hapo”Namshukuru sana mungu na wazazi wangu ambao wamenilea ila kwa
kweli nawapongeza na kuwashukuru pia mashabiki kwa kuwa bila wao mimi
nisingekuwa hapa nilipo”
Akizungumzia kuhusu watu wachache ambao
wamekuwa wakihusisha mafanikio yake na kundi la FreemaSon,alisema
umefika muda sasa wa Tanzania kuamka na si kwamba kila mtu anayefanikiwa
ni kumhusisha na kundi hilo ”nawaomba wa Tanzania wenzangu
wabadilike,si kwamba kila mtu anayefanikiwa basi ameingia katika kundi
hilo,mimi ni msanii wa zamani sana hivyo mafanikio nastahili,pia
ukizingatia kuwa ni msanii ambaye ninakubalika katika jamii”.
Mwana
FA alipoulizwa kuwa anaisaidia vipi jamii inayomzunguka hasa wajane na
wale watoto wenye ulemavu alisema,huwa anasaidia kupitia mfuko wa
Sawasawa Foundation,ambapo hupeleka misaada yake kwa ajili ya kusaidia
watoto yatima na wajane”Unajua imani ya dini yangu huwa hainuruhusu
kutangaza pale ninapotoa msaada,sababu hiyo ndio maana huwa nakuwa kimya
tu,ila nasaidia kupitia mfuko wa Sawasawa Foundation”
“Na malengo makubwa sana,hasa mwaka huu,kwani nimejipanga vya kutosha
kuhakikisha nitafanya mambo makubwa kuliko mwanzo,amini nimejipanga vya
kutosha ili nizidi kuwa juu zaidi”