Pages

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Wednesday, August 28, 2013

LYRICS | MRS SUPERSTAR - YOUNG KILLER

Kila mwanadamu anaupendo.

mwingne anawaza., vp atampataje,amtakaye..

sio kwamba na act..no niko real...

japo msodoki ni mdogo.,ila nauwezo waku feal...

fikra zangu zinani2ma nidate kwa maunda zoro.

najua ntaleta jiras kwa brother.,banana zoro

xaxa vp ningekua na penny,.iv ntakua free...

au kama ni ngekua na mwasit wa t.h.t..

ila penny na his diamond atanisumbua.,

hata mwasiti najua pendo  langu ata livua...

kwanza long time agoo.,

nishazimikaga na wema ila skendo za magazet daaa..

moyo wangu ukamtema,...

nikachukia mapapalazi niakahis wameharibu bahat.. moyo wangu nikauweka bondi..kwa chiku mwanaharakati...

ila wote 2nachana hatuta dumu magetoni,..

nklipozimika na besta..marlow akapiga honi,..

madam Lita na salama nikaogopa mcharuko wa b.s.s....

nimemove mpaka dar wolper ni mchane face 2 face....

ila roho inakataa inaogopa waigizaji...

macho yalisha2ua kwa frola h..baba akamuitaji...      

CHORS..BRIGHT & NE-MO..


Wapo weng nataman kuwa nao in my life..
muda mwingi natumia kuwaza nani atae nifaaa.
mrs super star nani ni mwite love..x2..

VERSE..2
Hiz hisia zangu..sidhan kama nakufuru...

akili inanituma niende sambamba na lulu...

ila naogopa yasinitokee ya kanumba 

nikasukumwa nikafa wengne wakang'oa mchumba..

ama ray c.. Nikimcheki machoni haish...

kile kiuno bila mfupa kingenipikia mapish..

ila ghafla nikaogopa niliposikia ana mchizi...

baada ya kuuliza ni nani..kumbe mnako lordyeä...

love kwa pipi atanipa upendo wa kina...

au tuta achana njia panda kama amini na linah...

kwenye love staki kukosea.,kua na mrembo mwene visa...

niwe na teya.,au nimuache ni date kwa mona lisa....

nikadata na diva..ile sauti ni soo...

ye ndo mgonjwa kwa raha zangu atanifia itakua soo...

sura ya pesa aunt ezekiel..young xna hela..

vanesa mdee najua hawezi kush kisela....

mara jokate kichwani akanitawala mpaka basi, 

nikajua ata nikisema nahisi hatonipa nafasi...

namuomba mungu ili anipe jift..special ....

isingekua kizungu zungu basi...

ningekua na recho....

.CHORS.. BRIGHT & NE.MO

Wapo wengi natamani kuwa nao in my life.. muda mwingi natumia kuwaza nani atae nifaa..
mrs superstar nani nimwite love..:x 2

VERSE..3

Usiku silali.. usingizi autokei...namuwaza johari...

ila ule ukaribu na ray....unanipa wasiwasi...

na mi sitaki  nijute...

basi nikahamia kwa daina baada ya kusema nimvute....

shilole naogopa...kumwambia yanayo nisibu,...

kwa khadija nikakope kopa....

nije nimpe taratiibu...nahisi ataniadhibu pedesheee...

wanafitina maana atahitaji matunzo chaa ajabu mi uwezo 

sinaa...nampenda uwoya mtoto wake ataniitajee.,..

kaka .,baba..ndikumana atanionaje...

hizi hisia zangu wala siitaji aswali....mi napend. 

Kuitwa babu bibi cheka ata kubali....

Tuesday, August 27, 2013

DIAMOND AIBA WIMBO WA DAYNA ANATAKA KUACHIA HIVI KARIBUNI ''NAMBA 1''


Baada ya tuhuma za kuiba wimbo wa H.Baba na Pasha, nataka kulewa. 

Msanii  Naseeb Abdul Diamond Platnum, ameingia tena ndani ya tuhuma baada ya kusadikiwa wimbo anaotaka kuuachia wa No.1 ni wa Dayna.

Inasemekana awali Dayna alimtaka Diamond wakafanye wimbo kwa Shedy, Diamond akakubali, akaskiliza mdundo na kumuahidi Dayna kwamba wangefanya wote. 

Lakini baadae Diamond akamrubuni Shedy na kumwambia ile bit ampe na aachane na kazi ya Dayna.

hii ni demo ya wimbo wa Dayna ambao unafanana kila kitu na wimbo wa Diamond anaotaka kuachia. skiliza na pia waweza ku share na wenzio.

CHANZO:-CHUMA BLOG

HUU NDIO WIMBO MPYA WA DOGO D F| YOUNG KILLER - MUNGU NIPE

Msanii anaeiwakilisha Mwanza, kutoka Super Nyota 2012, "Young Killer"  amefanya collable na msanii mdogo wa hip hop (11) anaeiwakilisha Mwanza pia "Dogo D" 
 
Collable hiyo waliyoipa jina la "Bora tu nipate Bora tu nipate maadui" inategemewa kutoka wiki ijayo.
 
Dogo D ni msanii wa hip hop ambae licha ya kuwa na umri mdogo kiasi hicho ameshafanya collable na Roma (haijatoka) na tayari ana single ambayo inafanya vizuri  pande za Mwanza "Mungu Nipe" feat Abuu Mkali.
 

Wednesday, August 21, 2013

FEZA,O'NEIL WAPONDA RAHA BOTSWANA, KUSHUHUDIA FAINALI ZA BBA


SUGU KUACHIA NGOMA MPYA

Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi ‘Mr ii Sugu ‘anatarajia kutoa ngoma yake mpya hivi karibuni iitwayo barua kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete Waraka 2.
Akiandika kupitia page yake ya facebook alisema kuwa yuko kwenye maandalizi ya kuandaa ngoma hiyo mpya ambayo inakuja ikiwa ni muendelezo wa ngoma ya kwanza iitwayo waraka Kwa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa Miaka kadhaa iliyopita, kwa sasa ni Rekodi mpya ambayo ni barua Kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waraka No 2.
‘Niko kwenye maandalizi ya kurekodi track yangu mpya inaitwa barua kwa rais-waraka 2’alisema Sungu.

HIVI NDIVYO MSHINDI WA GARI LA FIESTA KIGOMA ALIVYOKABIDHIWA ZAWADI YAKE


Meneja Masoko na Mauzo wa kampuni ya push Push Media Mobile Rugambo Rodney akimkabidhi namba ya gari/funguo mshindi wa kwanza wa gari aina ya Vitz iliyoendeshwa na kampuni hiyo kwa mashabikwa fiesta wa Kigoma. 

Rugambo alisema kuwa baada ya kugawa zawadi hiyo Kigoma, sasa wanaelekeza nguvu zao zote Tabora ambapo watatoa fedha taslim na pikipiki. 

Ili kushinda unatakiwa kutuma neno fiesta kwenda namba 15678.

MKAZI wa Kigoma, Abdallah Aly Ngagari (51) ameshinda gari aina ya Vitz iliyoendeshwa na kampuni ya Push Mobile Media ya kunogesha tamasha la Fiesta.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Kigoma, Meneja Masoko na Mauzo wa Push Mobile Media, Rugambo Rodney alisema kuwa tayari Ngagari amekabiziwa gari yake katika hafla fupi iliyofanyika huko huku Kigoma.

Rugambo alisema kuwa baada ya kukamilisha bahati nasibu hiyo, kwa sasa nguvu zao wanazielekeza mkoani Tabora katika tamasha la Fiesta ambalo litafanyika Ijumaa.

Alisema kuwa watatoa pikipiki kwa wapenzi wa muziki wa Tabora ambapo ili kushinda, mashabiki wanatakiwa kutuma neno Fiesta kwenda namba 15678 ili kushinda pikipiki au fedha taslim shs 100,000.

Alisema kuwa wamejipanga kufanya zoezi hilo na lengo kubwa ni kuwazawadia mashabiki wao ambao na kufaidika na tamasha hilo. Kwa mujibu wa Rugambo, zawadi zote zipo katika mikoa ambayo fiesta imefanyika na ndiyo maana wameweza kutoa zawadi mkoani Kigoma mara baada ya kuchezesha droo.

Tuma FIESTA kwenda 15678 nawe waweza kufaidika na FIESTA

JOKATE NA LUCCI "KAKA NA DADA"

The two are coming with something massive, this is Day 3 photo....stay tuned

BABA YAKE BOB JUNIOR AFANYA SHOO YA KUFA MTU NCHINI FINLAND



 
Bob Junior ni mwanamuziki maarufu wa Bongofleva lakini kipaji hicho ni kama amerithi kutoka kwa baba yake mzazi Mr. B Rummy Nanji ambaye pia ni mwanamuziki maarufu akifanya kazi zake ulaya.
 
Weekend iliyopita mdingi wa Bob Junior ali-perform nchini Finland kama anavyoonekana pichani hapo chini akifanya makamuzi ya kufa mtu.

MSANII MAVADO AGOMA KUSAFIRI KWA NDEGE TOFAUTI NA ALIYO AHIDIWA NA WAANDAJI WA SHOW HUKO JAMAICA

Mavado Msanii mkali wa miondoko ya Dancehall kutoka huko Jamaica, amekuwa gumzo hasa baada ya kukataa kwenda kufanya show huko Guyana baada ya waandaaji wa show hiyo kumtumia usafiri wa kandege kadogo badala ya Jet ambayo walimuahidi.

Msanii huyu na timu yake ya watu 17, waliipotezea show hii kubwa na kurudisha hasara yote kwa muandaaji ambaye mpaka sasa hajasema chochote katika vyombo vya habari kuhusiana na tukio hili.

Jitihada pia zinaendelea kumtafuta msanii huyu ama uongozi wake kufahamu zaidi mustakabali wa tukio hili na issue nzima ya kulipana fidia kama itakuwepo.

PRODUCER SCOT STORCH AIBIWA NA WAHUNI



Scot Storch Producer mkali wa muziki ambaye amekuwa ni mtu wa matukio sana  amekumbwa na maswahiba makubwa hasa baada ya kubananishwa na wahuni na kuibiwa pesa pamoja na vito vya dhahabu vyote alivyokuwa amevaa wakati alipokuwa akitoka katika hoteli ya New York Palace Madison Avenue.

Producer huyu amedai kuwa alifuatwa akiwa katika gari na watu waliokuwa na bunduki na kumuamrisha atoe kila alichonacho ama wangemwua,na producer huyu hakuwa na pingamizi zaidi ya kuwakabidhi briefcase iliyokuwa na dola zipatazo 5000 cash pamoja na vito alivyokuwa amevaa vyenye thamani inayofikia dola 100000, na jumla ya vitu alivyopigwa staa huyu vinafikia thamani ya shilingi 169,522,500/- za kitanzania.

Kwa sasa polisi wanaendelea kufuatilia issue hii baada ya kupata taarifa rasmi kutoka kwa Scot mwenyewe ambapo pia kwa sasa anakabiliwa na kesi mahakamani baada ya kushindwa kusimamia jukumu la kumlea mtoto wake inavyotakiwa.


KAULI YA MSANII DIAMOND BAAADA YA KUHUSISHWA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA




 
Msanii Wa Muziki wa Bongofleva mwenye jina kubwa Town na mwenye Mkwanja mkubwa hapa nchini Nasseeb Abdulmaliki “Diamond” amejitokeza na kukanusha kuwa hahusiki na biashara ya madawa ya kulevya.

Ni kwa muda mrefu sasa kumekuwa na taarifa za Diamond kujihusisha na biashara hiyo hasa kutokana na ukaribu wake na wfanya biashara wakubwa wa dawa za kulevya wenye maskani yao nchini Afrika Kusini.

Taarifa zaidi zinasema ni wafanyabiashara hao waliohusika kwa karibu kuusafirisha mwili wa marehemu Albert Mangwair, aliyefia huko huko Afrika Kusini ambaye taarifa za kifo chake ziligubikwa na matumizi ya madawa ya kulevya.

Akikanusha taarifa hizo Diamond alisema “ni kweli mimi nina pesa za kutosha kuniwezesha kuishi maisha ninayotaka lakini sijawahi kujihusisha na biashara hiyo. Kufanya kazi kwa bidii kunalipa na kazi yangu inaonekana na ndiyo inayoniwezesha kuwa na fedha ambazo leo watu wameanza kuzitilia shaka.

Sielewi nia ya watu hawa ni nini?”

Taarifa za Diamond kuhusishwa na mtandao huu zimeanza kushika kasi kufuatia miongoni mwa watu wake wa karibu kuonekana wakiwa karibu sana na akina Agnes Gerald “Masogange” (25) na Melisa Edward (24) kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa Mwalimu JK Nyerere wa Dar es Salaam kabla hawajapanda ndege kuelekea Afrika Kusini ambako walikamatwa.

Picha Za Utengenezwaji Wa Video Ya TNG - Crazy Man



 Kutoka Kwa Chiwa Man Wa Tng, Wako busy wakikamilisha project yao mpya ya Crazy Man Na Video imefanyiwa shoot week iliyopita. Picha alizo nitumia hizi hapa.




KANYE WEST AKATAA KUWA JUGDE WA AMERICAN IDOL.

Vyanzo vya habari vumereport kuwa Kanye West amekataa nafasi ya kuwa judge kwenye season mpya ya show ya kutafuta vipaji vya uimbaji (American Idol).

Vyanzo hivyo vimeendelea kusema kuwa Kanye amekataa ofa hiyo ya kuwa judge katika season ijayo (Season 13) kutokana na kuwa show ya kisasa sana "mainstream"
 
Producers wa American Idol walitarajia kuwa na Will.i.am Sean Diddy Combs na Rodney Jenkins katika meza ya majugde ,lakini mwisho wasiku inaonekana na watakuwa na songwriter and record producer Dr. Luke, ambaye ataungana na Keith Urban pamoja na Jennifer Lopez..

DIAMOND ATAJWA SAKATA LA UNGA.

*Utajiri, safari zake nje ya nchi vyatiliwa shaka
*Ahusishwa na mtandao hatari wa Masogange
KWA mara ya kwanza tangu lilipoibuka sakata la watu maarufu kujihusisha ama na utumiaji au usafirishaji wa dawa za kulevya, jina la mwanamuziki anayeaminika kuwa na ukwasi mkubwa kwa sasa hapa nchini, Nasseeb Abdulmaliki, maarufu zaidi kwa jina la Diamond, limeanza kutajwa kuwa ni miongoni mwa vigogo wa ‘unga.’

Tayari mjadala mkubwa wa chini chini umeibuka kwa watu mbalimbali wakiwemo mashabiki wake, na taarifa ambazo zimelifikia MTANZANIA Jumatano kutoka vyanzo mbalimbali zimedai kuwa, mwenendo wa maisha ya Diamond sasa unachunguzwa na baadhi ya maofisa wa vyombo vya dola vya ulinzi na usalama.

Kutajwa kwa jina la Diamond katika sakata hili, kunatiwa nguvu zaidi na mwenendo binafsi wa maisha wa msanii huyo maarufu wa muziki wa kizazi kipya, unaokwenda sambamba na ukwasi mkubwa alioupata katika kipindi kifupi.
Kama hiyo haitoshi, safari za nje ya nchi za mwanamuziki huyo unaohusisha ziara zake nchini Afrika Kusini na Uingereza, pia ni mambo ambayo yamechochea wingu la mashaka lililofikia hatua ya jina lake kuingizwa katika mtandao huo ambao katika siku za karibuni, umewagusa pia baadhi ya watu wenye majina makubwa katika jamii.

Kuhusu ziara hizo, kilicholeta mshtuko na dukuduku dhidi yake ni kuwapo kwa taarifa kwamba, katika moja ya ziara hizo za nje ya nchi, Diamond alifikia hatua ya kusafiri akitumia chumba kinachotumiwa na wageni mashuhuri (VIP), badala ya njia ya wasafiri wa kawaida.

Mbali na hilo, taarifa nyingine zinaeleza kwamba, mizigo ya msanii huyo ambaye mara kadhaa amekuwa akisafiri na kundi la wacheza shoo wake, imekuwa ikipita pasipo kupitishwa katika hatua za ukaguzi kwa namna ile ile ilivyokuwa kwa mabinti wawili wa Kitanzania walionaswa nchini Afrika Kusini baada ya kuruka mfumo wa ukaguzi wa JNIA.

Aidha, ukaribu wa kimahusiano kati ya Diamond na baadhi ya Watanzania wanaoishi nchini Afrika Kusini na ambao majina yao pia yameanza kuhusishwa na biashara hiyo ya mihadarati, ni jambo jingine ambalo limechochea harakati za kufuatiliwa kwa karibu kwa nyendo za Diamond.

Taarifa zaidi kutoka JNIA zinaeleza kwamba, miongoni mwa watu wanaoweza wakawa wamemponza Diamond ni wale ambao walionekana kuwa karibu na Agness Gerald ‘Masogange’ (25) na Melisa Edward (24), siku walipokuwa wakisafiri kwenda Afrika Kusini kabla hawajanaswa katika uwanja wa Ndege wa Oliver Thambo jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini, wakiwa na shehena ya dawa za kulevya.

Mwenendo wa watu hao unatiliwa shaka kuwa huenda ni miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya wenye maskani yao nchini Afrika Kusini, kwa sababu mbali na ukaribu na wasichana hao, pia walihusika kwa karibu kuusafirisha mwili wa mwanamuziki Albert Mangwair, aliyefia huko huko Afrika Kusini ambaye taarifa za kufa kwake ziligumbikwa na matumizi ya dawa za kulevya.

Alipoulizwa jana na MTANZANIA Jumatano kupitia simu yake ya kiganjani kuhusu taarifa hizo na iwapo amekwishahojiwa na vyombo vya dola baada ya jina lake kuanza kutajwa kuwa miongoni mwa orodha ya wasanii wa muziki wanaosafirisha dawa za kulevya, Diamond alikiri kuwa na pesa za kutosha kuishi maisha anayoyataka, lakini akakana kujihusisha na biashara hiyo.

Akifafanua tuhuma moja baada ya nyingine kwa mpangilio aliokuwa akiulizwa na gazeti hili, Diamond alisema katika maisha yake, hajawahi kujihusisha na utumiaji au usafirishaji dawa za kulevya, lakini madai hayo yamekuwa yakitolewa dhidi yake na watu ambao hawajui siri ya mafanikio yake.

“Kazi ngumu siku zote inalipa, sasa napata matunda ambayo yanatokana na kile nilichokifanya, iweje watu wanitilie mashaka, Watanzania ni mashahidi wangu wananiona navyochumia juani, nitaendelea kulia kivulini tu kwani nakula kwa jasho langu.

“Siyo kweli kwamba mizigo yangu haikukaguliwa na kama haikukaguliwa na ingekuwa na kasoro, basi Uingereza wangenitia hatiani, nilipita na nilikaguliwa.” Alisema Diamond.

Alipoulizwa kuhusu taarifa za kuwa mwanamtandao wa kundi la Masogange, pia alikanusha kwa kueleza kuwa hata siku aliyosafiri kwenda Afrika Kusini alikwenda peke yake uwanja wa ndege na kuongeza kuwa alikwenda huko kwa shughuli za kimuziki, ambapo safari nzima iligharimu zaidi ya Dola 30,000 za Kimarekani.

“Afrika Kusini nimekwenda kufanya kazi zangu na safari hiyo imenigharimu zaidi ya Dola 30,000, nilikwenda kurekodi nyimbo yangu mpya inayoitwa namba moja ambayo itaanza kusikika hivi karibuni.

“Unajua Watanzania sasa hivi wanajua mtu hawezi kufanikiwa au kupata maendeleo bila kuuza ‘unga’, hili si sawa juhudi za mtu ndizo zinamfikisha alipo, na mimi juhudi zangu ndio zinanifikisha hapa, watu waache kunijadili vibaya.” Alisema Diamond.

Kuibuka kwa taarifa hizi kumekuja ikiwa ni takribani miezi miwili sasa tangu Watanzania wawili, Agness Gerald ‘Masogange’ (25) na Melisa Edward (24), waliokuwa na uhusiano wa karibu na baadhi ya wanamuziki maarufu hapa nchini, kukamatwa nchini Afrika Kusini wakiwa na dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani ya Sh bilioni 6.8.

Mbali na kuwa na uhusiano wa karibu na wanamuziki, Edward anadaiwa kuwa alikuwa mfanyakazi katika mgahawa mmoja maarufu jijini Dar es Salaam, unaomilikiwa na mmoja wa vijana matajiri hapa nchini ambaye hata hivyo gazeti hili halijafanikiwa kumpata ili kufanya naye mahojiano.

Wakati huo huo, tayari hatua za kinidhamu zimekwishaanza kuchukuliwa dhidi ya wafanyakazi wa JNIA waliohusika kupitisha kilo 150 za dawa za kulevya, ambao Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ametaja majina yao hivi karibuni na kuonyesha kwa waandishi wa habari ushahidi wa kuhusika kwao.

Tuesday, August 20, 2013

FAHAMU KUHUSU RAPPER RICK ROSS NA KAMPUNI YA REBOOK

Je Rick Ross Bado Anafanya Kazi Na Reebok.. Ni swali linalo ulizwa na mashabiki wengi wa MMG Na Wa Rapper Rick Ross na kazi zake. 

Fahamu kuwa kwa sasa Rapper huyo anatangaza ujio wa album yake mpya ya Self Made 3 na kwenye mkusanyiko wa picha alizo toa kwenye promo ya album hio ni hii picha inayo onyesha bidha za Reebok pembeni ya gari

JAY Z KUFANYA SHOW UARABUNI NOVEMBA O1 2013

Kwa mara ya kwanza kabisa katika historia yake ya muziki, Rapper Jay Z anatarajia kufanya onyesho huko Uarabuni Abu Dhabi, Tarehe 1 mwezi November mwaka huu. Onyesho hili litakuwa ni katika kusindikiza mashindano maarufu ya magari ya Abu Dhabi Grand Prix, na kwa mujibu wa taarifa za chini chini, Mpunga wa kutosha tu umetumika kumchukua staa huyu kwaajili ya kupanda jukwaani siku hiyo.

Wasanii wengine ambao watakuwepo katika kufanya onyesho katika tukio hili ni pamoja na Amr Diab, Elissa, Hussain Al Jassmi, Bendi ya Muse kutoka Uingereza na kundi la Depeche Mode kutoka Uingereza pia.

November 2013, Utaona Hii Filamu Kuhusu Maisha Ya Nelson Mandela, Hawa Ndio Wamepewa Heshima Ya Kuigiza Filamu Hio

Star kutoka Marekani Idris Elba amepewa heshima kubwa ya kuigiza kama Nelson Mandela kwenye filamu ya maisha ya Mandela iliyopewa jina la Mandela: Long Walk To Freedom. Kwenye filamu hii tunaona harakati za Mandela za kuondoa na kutokomeza mfumo wa Apartheid nchini South Africa.

Huyu Star umemuona kwenye filamu kama Takers, Thor, 28 Weeks Later Na The Unborn
 
Kwenye filamu hii pia tunaona maisha ya Nelsom mpaka alivyo kuja kumuoa Mke wake wa Pili Winnie Mandela ambaye husika wake umechezwa na Naomie Harris uliyemuona kwenye filamu kama Sky Fall.


 

CHEKI TRAILER YA FILAMU KALI YA BONGO ITAKATOKA HIVI KARIBUNI 'GOING BONGO'

HALI YA KIAFYA YA MEMBER WA B2K ''RAZ B YAENDELEA VIZURI HII NI MARA BAADA YA KUPIGWA NA CHUPA KICHWANI



 Alhamisi ya wiki iliyopita (August 15), aliekuwa mwimbaji wa kundi la B2K Raz-B, alijikuta katika chumba cha watu mahututi baada ya kupigwa na chupa kichwani katika moja ya show alizokuwa akifanya nchini China.
Raz-b (28) alikuwa akifanya show kwenye moja ya kumbi za starehe Zhejiang, China wakati ugomvi ulipotokea upande wa mashabiki wameripoti TMZ.
 
Inasemekana Raz alienda kusuluhisha huo ugomvi wakati jamaa mmoja alipo vurumusha chupa iliyompata kichwani na kupelekea kukatwa sehem mbali mbali na kumchana sana kwenye mdomo wake na kusababisha kufanyiwa operation ya saa  moja kurekebisha shimo kwenye mdomo wake  iliyokuwa pia ikihitaji nyuzi 4.

siku moja baada ya kufanyiwa upasuaji hali haikuwa nzuri, hakuweza kuamka na mmoja wa ma dancers wake alimkimbiza hospitali ya karibu na hali yake kusemekana kuwa mbaya kiasi cha kufikia kupumulia mashine.
Raz-b amekua akiishi China kwa miaka 3 sasa na ana plan za kurudi marekani 
UPDATE: Hali ya Raz kwa sasa inaendelea vizuri, anapumua mwenyewe bila kutumia mashine na anaongea na kucheka la bado hajaruhusiwa kutoka hoospitali.. amesema mmoja wa watu wake wa karibu.
muwakilishi wa Raz amesema "Doc amesema ni maajabu ame-survive"

Wasanii waungana kutokomeza zero mashuleni FA, Stamina,Roma, Kalla Jeremiah Mwasiti, Linex,Petter Msechu.

Wasanii wa hiphop na bongo fleva wakutana na kutengeneza wimbo maalumu "Tokomeza zero" kwa ajili ya kyhamasisha wanafunzi mashuleni kupenda shule, kuithamini elimu, mwisho wa siku kuitokomeza zero.
Wimbo huo umeandikwa na Ditto na kutayarishwa na producer Tudd Thomas na kufanywa na wasanii kama, Lina, stamina, Mwasiti, FA, Linex, Roma, Diamond, Maunda Zorro, Petter Msechu, Keisher na Kalla Jeremiah.

FIESTA ROAD TRIP KIGOMA TO TABORA NA SINGIDA


Timu ya Clouds Media Group njiani kuelekea Tabora na Singida kwa ajili ya Fiesta 2013, Tabora itafanyika tarehe Ijumaa 23 August 2013 ndani ya Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi na Singida ni Jumapili tarehe 25 August 2013 Singida Motel.Adam Mchomvu.
Team on the move to Tabora and Singida.
Adam Mchomvu.
Haroun Driver akibadilisha tairi.

Labels