Hii ni Rmx ya ngoma ya Joto, Hasira ya Malkia wa muzki Tanzania maarufu
kama Lady JayDee ambayo amefanya na Songa, Mkoloni pamoja na Nikki
Mbishi.
Pages
▼
Monday, September 30, 2013
CHEREKO CHEREKO YA CPWAA KUACHIWA RASMI OCTOBER MOSI 2013
"Chereko Chereko" ni ngoma mpya ya mwanamuziki maaufu kwa jina la Ilunga Khalifa a.k.a Cpwaa "The King Of Bongo Crank", ambayo inatarajiwa kuachiwa siku ya kesho ambayo ni itakuwa October 1.
Cpwaa anatarajia kuachia ngoma hiyo katika radio stations tofauti za hapa nchini pamoja na kwenye Social medias.
Ngoma hii ya Chereko Chereko ambayo imebeba mahadhi ya Afro Dance imefanywa ndani ya Studio ya De Fetality Music chini ya Producer Mensen Selector.
Cpwaa anatarajia kuachia ngoma hiyo katika radio stations tofauti za hapa nchini pamoja na kwenye Social medias.
Ngoma hii ya Chereko Chereko ambayo imebeba mahadhi ya Afro Dance imefanywa ndani ya Studio ya De Fetality Music chini ya Producer Mensen Selector.
Sunday, September 29, 2013
PICHA SHOW YA DIAMOND ZANZIBAR PICHA,DIAMOND PLATNUM ALIVYOACHA HISTORIA ZANZIBAR,AFANYA SHOW KUBWA SANA
Akizungumza na watu wa zanzibar ndani ya kituo kikubwa kabisa cha Radio Zanzibar Coconut Radio
Baadae nikakutana na waandishi wa habari ndani ya hotel ya kisasa kabisa,Zanzibar beach lesort
Wanahabari kazini
ROSE NDAUKA KUJIFUNGUA BILA NDOA
Staa wa filamu za Bongowood, Rose Ndauka
ambaye ni mjamzito anadaiwa kuwa atazaa kabla ndoa mwezi Aprili,
mwakani.
Akizungumza na mwanahabari wetu, mchumbaa’ke, Malick Bandawe
ambaye ni memba wa kundi la muziki la TNG alianika aya za Kurani kuwa
katika Dini ya Kiislamu si ruhusa kufunga ndoa na mwanamke ambaye ni
mjamzito kwani ni sawa na kufunga ndoa na watu wawili hivyo anamsubiri
ajifungue kwanza.
“Ni kweli mchumbaa’ngu hivi sasa ni mjamzito na
anatarajia kujifungua mapema mwezi wanne, mwakani.
“Kuhusu kufunga naye
ndoa kwa sasa ni ngumu hadi ajifungue kwani kwa dini yetu (Uislam) si
ruhusa kufanya hivyo lakini atakapojifungua tu tutafunga ndoa,” alisema
Malick.
Malick ambaye hivi sasa anatamba na Wimbo wa ‘Crazy Man’ alisema
kuwa ana furaha kubwa kuitwa baba mtarajiwa na anamuomba Mwenyezi Mungu
Rose ajifungue salama kwani anampenda kupita maelezo.
Baada ya
kuzungumza na Malick, gazeti hili lilimtafuta mama wa Rose Ndauka,
Batuli kufungukia ishu ya mwanaye kubeba ujauzito kabla ya ndoa ambapo
aligoma kuzungumza kwani hakubaliani na suala hilo.
PICHA YA RECHO YA NUSU UCHI ALIYOWEKA INSTAGRAM YAZUA MANENO MANENO
Stori: Gladness Mallya
MSANII wa filamu za kibongo, Rachel
Haule ‘Recho’ hivi karibuni aligeuka kituko baada ya kutupia picha ya
nusu utupu katika mtandao wa kijamii.
Picha hiyo ambayo Recho amevaa shati tupu (inayoonesha ndani) bila kuvaa kitu kingine chochote, aliitupia kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo mashabiki na marafiki zake walichangia huku wakimlaumu kuwa hakufanya vizuri kuiweka picha hiyo ya aibu mtandaoni.
Paparazi wetu alimuuliza Recho kulikoni? Akajibu hivi:
“Nawapenda sana marafiki zangu lakini mimi sijaona tatizo la hii picha kwa sababu ni ya kawaida sana sioni ubaya wake.”
GPL
PICHA ZA UTENGENEZAJI WA VIDEO MPYA YA BABAJONII
BABAJONII AKIWA KATIKA MOJA YA SHOT ZA VIDEO YAKE MPYA AMBAYO ITAKUJA KUKICK MJINI MUDA SI MREFU

BABAJONII AKIWA NA MBWA WALIOTUMIKA KWENYE VIDEO YAKE MPYA

BABAJONII KATIKA KAZI

Miss Philippines avishwa taji la Miss World na miss kutoka Ghana awa mshindi tatu. Angalia picha ya tukio jinsi lilivyokuwa
Miss Philippines Megan Young mwenye umri wa miaka 23 amevishwa taji
la Miss World ambalo limefanyika leo hii huko Indonesia. Megan ni
mzaliwa wa Marekani na ana umri wa miaka 23 anasomea mambo ya digital
film. Mshindi wa pili ametoka France na watatu kutoka Ghana.
Megan akitoa hotuba ya shukrani baada ya kuvishwa taji na Wenxia Yu
wa China ambaye ndiyo Miss World aliyemaliza muda wake leo, Megan
ameahidi kuwa miss world bora zaidi ya waliowahi kutokea.















PICHA NA:-DJ CHOKA
