
Pages
▼
Thursday, September 04, 2014
Wednesday, September 03, 2014
Habari na Picha: Jumba la Big Brother lateketea kwa moto | Uzinduzi umesogezwa Mbele
Habari ya kusikitisha kwa mashabiki wa shindano la Big
Brother Africa, Jumba linalotumika kufanyia shindano hilo lililoko
Johannesburg, Afrika Kusini limeteketea kwa moto September 2.

Kutokana na tukio hilo, M-Net na Endemol South Africa
wameeleza kuwa wamelazimika kubadili ratiba ya shindano hilo msimu huu
lililopewa jina la ‘Big Brother Hotshots’ na halitaanza September 7 kama
ilivyotarajiwa hapo awali.
Chanzo cha moto huo hadi sasa hakijajulikana na makampuni
hayo yameeleza kuwa uchunguzi wa kina utaanza mara moja.
Makampuni hayo yamepata changamoto kubwa kutokana na tatizo
hilo kwa kuwa vifaa vinavyotumika kufanyia uzalishaji ni vya aghali na adimu
sana hivyo wameeleza kuwa ni vigumu kupata vifaa mbadala hivi punde.

“Kila juhudi itafanywa kutafuta ufumbuzi wa tatizo haraka
iwezekanavyo kuhakikisha kuwa reality show hii kubwa zaidi Afrika inaendelea.”
Wameeleza katika tamko lao.
Hakuna mtu aliyejuruhiwa katika tukio hilo.
M-Net and Endemol SA advise that due to a devastating fire at the Big Brother house on 2 September 2014, Big Brother Hotshots will not launch this Sunday (7 September) as schedule.
The cause of the fire at this stage is unknown and investigations will commence as soon as it is safe to do so.
At this stage M-Net and Endemol are urgently looking for an alternative Big Brother house in which to film the production, however as this production has highly technical infrastructure, camera and edit requirements an alternative is not immediately available. Every effort will be made to find a solution as quickly as possible to ensure that Africa’s biggest reality show will continue.
CHANZO:-www.timesfm.co.tz
Weestar ajiondoa Navy Kenzo na kusaini na Ngoma Entertainment | sikiliza kionjo
Kwa mujibu wa maelezo ya Ngoma Entertainment kwa Bongo5, Msanii huyo ameamua kufanya muziki na watu wamfahamu kama Weestar na sio kama member wa tatu wa kundi la Navy Kenzo.
Hivi sasa Navy Kenzo imebaki na wasanii wawili ambao ni wapenzi, Nahreel na Aika.
“Ameamua kuwa huu ni muda wa watu kumfahamu kama Weestar na sio kama member wa tatu wa Navy Kenzo. Anaamini kila msanii ana sauti yake na wajibu wake wa kuwapa watu kile Mungu alichompatia. Single yake ya kwanza kama msanii anayejitegemea inaitwa ‘Naiye’ na inatoka Ijumaa hii kwenye vituo vya redio.” Wamesema Ngoma Entertainment kwenye maelezo yao.
Tuesday, September 02, 2014
NEW SONG | CHANDE - Feat - Belle9 - USICHELEWE
Singer Name;-Chande ft Belle 9
Song Name:-Usichelewe
Country;-Tanzania
Genre;-Bongo Fleva
Producer;-Amiga tiger
Hi,
I hope you're doing well.
This is brandy new song from Teylano Music Classic by
Artist;-Chande ft Belle 9
track;-Usichelewe
We thanks for promoting us everyday..
God bless you...Call me 0658747424 For More Information...by Lawize Music Entertainment..
Kim Kardashian kuitosa familia yake kwa ajili ya Kanye West

Mwanamitindo Kim Kardashian
anaripotiwa kufikiria kuchukua uamuzi mgumu ili kumfurahisha mumewe Kanye West,
uamuzi ambao utaiangusha biashara kubwa ya familia yake ‘The Kardashians’.
Kwa mujibu wa The Sunday
People, Kim Kardashian anapanga kuitosa reality show ya familia yake ‘Keeping
Up With the Kardashians’ kwa sababu Kanye West hapendi kabisa jinsi ambavyo
anayaanika maisha yake kwenye kipindi cha runinga.
Kanye West anataka maisha yake
na mkewe kuwa ‘binafsi’ kwa kuwa hivi sasa ni tofauti na alivyokuwa awali.
Endapo Kim K atafuata matakwa
ya Kanye West, ni dhahiri kuwa Keeping Up With The Kardashian itashuka sana
umaarufu kwa kuwa uwepo wake una mchango mkubwa kutokana na umaarufu alionao.
“Lakini ni vigumu kwake kwa
sababu kwa kiasi kikubwa familia yake inamtegemea awe pale kuuza maisha yake
kwenye kamera. Inawezekana akajitoa hivi karibuni, japokuwa series bado ina hit
sana.” Chanzo kiliieleza The Sunday People.
Huenda Kim Kardashian akajikita
katika masuala ya mitindo kwa sababu tayari alizindua ‘The Kardashian
Kollection’ akiwa na ndugu zake Khole Kardashian na Koutney Kardashian.
CHANZO:-www.timesfm.co.tz
Diamond Platnumz kutumbuiza kwenye uzinduzi wa Big Brother Africa, Jumamosi

Diamond Platnumz atakuwa
miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye uzinduzi wa msimu mpya wa shindano
la Big
Brother Africa utakaofanyika Jumamosi hii, September 7 nchini Afrika
Kusini.
Meneja wa staa huyo, Babu Tale
amesema Diamond atarejea leo akitokea nchini Ujerumani ili kujianda ya na show
hiyo.
“Diamond anarudi leo saa tano
usiku atakuwa kasharudi bongo kwa sababu weekend hii tunaperform kwenye Big
Brother launch kwahiyo tunaenda South Africa.
Tukitoka South Africa Tutaenda
Nairobi kwenye Coke Studio kurekodi. Tukitoka Nairobi tunakwenda Ungereza
kwenye show ya African Unplugged, kwaHiyo ratiba yetu ipo tight,” amesema Tale.
MAJINA YA WASANII WA KUWANIA TUZO ZA CHOAMVA 2014 KUTANGAZWA ALHAMIS YA SEPTEMBA 4,2014
Majina ya Kuwania Tuzo za
CHOAMVA(Channel
O Africa Music Video Awards) 2014 yanatarajiwa kutangazwa Alhamis September 4 ,2014 ya Wiki hii,Swali ni Je, Ni Msanii Yupi wa Tanzania Ataiwakilisha/Wataiwakilisha Nchi Mwaka Huu?

Mwaka jana Msanii A.Y alikuwa Ni msanii pekee aliyeiwakilisha Tanzania katika Tuzo Hizo,Mwaka
huu kuna uwezekano mkubwa Diamond Platnumz akatajwa kwenye vipengele kadhaa Kutokana Kuwa ni Msanii anayefanya Poa Kimuziki na Kuwa-Nominated katika Tuzo Mbalimbali mwaka Huu.






