Pages

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Friday, April 18, 2014

(New Audio) Ezdee ft. Mau & Mabov – BORN TODAY

IMG_20140414_165937-3
Nilirekodi juzi tarehe 16 kama zawadi to all the fans kwa siku yangu ya kuzaliwa. Inaitwa “BORN TODAY” pia ni special dedication kwa waliozaliwa April (Team Aries) zaidi it talks about the concept of us being alive. Nini maana ya kuzaliwa? What’s the purpose of living…? Vitu kama hivyo zaidi ukisikiliza  utapata mengi.

Enjoy ujio mwingine wa EZDEE!!! Pia shukrani sana kwa wote walionitakia mema on my birthday. One love
Its an everyday song.
Please support Hiphop
Artist: EZDEE Ft. MAU & MABOV
Song:  BORN TODAY
Producer: Bunduki AK47
Kaju (Gofu Rec

MASAI NYOTAMBOFU AITEMA KAMPUNI YA AL-RIYAMY.

MCHEKESHAJI maarufu hapa nchini katika swaga za kimasai ambaye pia ni mmiliki wa masainyotambofu.info Gilliady Severine Kahema 'Masai Nyotambofu' Ameamua kuitema kampuni aliyokuwa na mkataba nayo ya Al-Riyamy Pro ambayo hurusha kipindi chake cha VITUKO SHOW kwenye runinga ya CHANNEL TEN. 

Akizungumza na babamzazi.com leo, Masai Nyotambofu alisema kuwa ameamua kuachana na kampuni hio baada kugundua kuwa kuendelea kuwepo pale kwa muda mrefu ni sawasawa na kuididimiza sanaa yake kwani hamna mafanikio yeyote zaidi ya kuahidiwa kwamba baada ya kipindi fulani mambo yatakuwa mazuri huku siku zinazidi kwenda,
 
''Kiukweli nimeamua kuachana na Al-Riyamy Pro maana naona muda wote wa miaka mitano sijafikia malengo yangu niliotarajia na ahadi za kampuni hazionekani, 
Pia kikubwa zaidi kilichoniondoa ni pamoja na kuchezeshwa na wasanii wasio na vipaji halisi wanaishia kuigaiga stile za watu tu hatima yake tunaonekana wote wabovu. 
 
Hapo mwanzo tulivyokuwa timu kamili tulifanya vizuri na kupokelewa vizuri lakini walivyoondoka baadhi ya wasanii wenye uwezo mkurugenzi akasema analeta wasanii wengine, 
 
Basi mimi nikaendelea kusubiri maana kila msanii alikuwa na mkataba wake hivyo kila aliyeondoka aliondoka kwa sababu zake binafsi mimi nikaendelea kukomaa nikihisi mbele ya safari kutakuwa na mabadiliko, Mara mkurugenzi akaaza kuwaleta watu tu from no whwre wasio na vipaji vya sanaa tucheze nao, 
 
Kila nikimuuliza kuwa mbona wengine wakisimama mbele ya Camera wakiambiwa Action hawajui itakuwaje? Jibu lake alinijibu nawasaidia maisha yao magumu. 
 
Nikamwambia huoni kuwa kazi ikiwa mbovu tutapoteza mashabiki? Akajibu we fanya kazi ntapitisha mchujo wasio na vipaji ntawaondoa watabaki wenye vipaji wachache tu niwatengenezee maisha ili muuone umuhimu wa kukaa kwenu hapa miaka mingi mimi nauona uvumilivu wenu, 
 
Cha ajabu mkurugenzi aliendea kujaza watu wasio na vipaji uongozi hakuna nidhamu kambini mbovu mimi siheshimiwi na mimi simuheshimu mtu basi tafrani kama kilabu cha komoni. Lakini nikaendelea kukomaa nikitarajia mabadiliko mwaka 2014, 
 
Kuna siku nikajaribu kumwambia mkurugenzi kuwa aniazime kiasi fulani cha fedha nikamilishe Video ya wimbo wangu alafu anikate akasema sina hela huoni mko wengi? kwanza kampuni hainilipi wewe unataka upate promo ili uzidi kuitwa kwenye Show utashuti saa ngapi na kwenye Show utaenda saa ngapi? Dah! Hapo ndipo nilipoona kuwa napoteza muda ukizingatia mwanzoni tulivyokuwa wakali watupu kipindi kikiruka hewani simu za wasanii zinaita mpaka kero lakini sasahivi kipindi kinaruka mwanzo mwisho hata hubipiwi..! Ni ishara tosha kwamba watazamaji wameanza kuingia mitini. 
 
Ni bora nikae pembeni nikinusuru kipaji changu kwani kama riziki yangu mwenyezi mungu hakuniandikia kuipata hapo hata nikomae vipi kamwe sitofanikiwa hapo. 
 
Nimeamua kurudi Nyumbani Jijini Dar kutuliza kichwa sina mkataba na kampuni yeyote kwa sasa najiandaa kuachia ngoma mpya baada ile niliyomshirikisha Rich Mavoko na Kitokololo (Yero Masai) Watu wangu kaeni mkao wa kula Uchekeshaji siachi mpaka mwisho wa uhai wangu, Kuondoka Al-Riyamy Pro Sio mwisho wa kampuni kufanya kazi wataendea wengine na wala sio mwisho wangu wa kuchekesha bado mtaendela kuzipata ladha zangu kupitia filamu zangu ambazo nipo katika mikakati ya kuanzisha Project. Namshukuru mwenyezi mungu kwa kunipa kipaji hiki kilichonifanya niwe na ukaribu wa hali ya juu na watu mbali mbali na katika show zangu napokelewa vizuri hicho kinanifanya nimuheshimu kila mtu wa kila rika, 
 
Nawapenda Mashabiki wangu One Love.

HUYU NDIYE MTANZANIA NA MWANAMITINDO WA KWANZA AKAUNTI YAKE YA FACEBOOK KUWA VERIFIED NA KUWA OFFICIAL.

Flaviana Matata ni jina linalofahamika zaidi hapa Tanzania na hata nje ya Tanzania, Flaviana ambaye alizaliwa June 9, 1987 (age 26), Shinyanga, Tanzania Amekuwa ndiye mtanzania wa kwanza kwa akaunti yake ye facebook kuwa Verified na kuwa official kwa kuwepo alama ya Tiki katika akaunti yake inavoonekana hapa chini.
 Kampuni ya Tigo Tanzania  ilikuwa ndiyo ya kwanza kuwa Verified katika mtandao wa kijamii wa facebook, Twitter msanii wa kwanza kukubaliwa na kuwa verified ni Ay.

MARTINE KADINDA AMUITA LULU MICHAEL NYAU.


Mwanamitindo maarufu Bongo, Martin Kadinda amempongeza Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa kumuita nyau.

Martin alifanya ishu hiyo wakati akimtakia Lulu Happy Birthday Aprili 16 ambapo mwanadada huyo alikuwa akitimiza umri wa miaka 19. Mwandishi wetu alipomhoji kuhusiana na kumuita nyau, Martin alifunguka:

“Yule kwangu ni mdogo, nimemlea tangu akiwa
anasoma sekondari pale Perfect Vision Ubungo, nimetumia neno nyau kama utani lakini nikimaanisha mdogo kwangu.”

Mrisho Mpoto aelezea sababu kutovaa viatu kwenye matembezi binafsi na ata akiwa safari za Kimataifa

Msanii wa muziki wa asili Mrisho Mpoto amedai kuwa ajisikii vizuri pindi anapo vaa viatu kutokana kudai kuvaa viatu kuna athiri utendaji wa kazi zake
 Mpoto akiwa na gari ambalo alikataa kuzungumzi chochote
Mpoto akiwa na gari ambalo alikataa kuzungumzi chochote

Mpoto ameiambia bongo5 kuwa amesemwa sana kuhusu tabia ya kuto vaa viatu lakini ameshindwa kubadilika.

“Beauty yoyote ipo kwenye jicho,unapozungumzi Mrisho Mpoto kuwa peku ,sehemu nyingi sana,mara nyingi sana watu wananiona peku, ni kwa sababu ya kutafuta energy ,unajua energy ya mimi kuendelea kuishi inapatikana
kwenye udongo,yani ngozi yangu inapokutana na ardhi nakuwa so (confident) na nakuwa Mpoto, zaidi na nguvu na nakuwa na akili ,sasa sipendi wakati mwingine kuwa fake,najitaidi sana kuwa wakisasa ila nakuwa nasahau,kwamfano naweza nikanunu kiatu cha gharama alafu nikakisahau kwenye ndege au kwenye basi kwasababu siyo kawaida yangu kuvaa viatu, nisha jaribu lakini nimeshapoteza vingi,kwasababu siyo culture yangu kuvaa viatu ,viatu navaaga kwasababu watu wananisema.


kwaiyo nikivaa ninakuwa kama inanisumbua, nikaona kama bora niache,alafu nakuwa siko huru,ukinikuta nimevaa viatu alafu tukaanza kufanya mazungumzo nakuwa siko huru kwasababu nakuwa nipo kama naelea hewani,yani kama sina chaji,kwaiyo kwangu mimi ardhi ni kama plug ya
mwili wangu,nikikanyaga chini wewe niulize chochote nitakujibu niambie niandike shairi la haina yoyote,mimi ata nikiandika nyumbani kwangu lazima niweke miguu kwenye mchanga,ata nyumbani kwangu hakuna mchanga mimi ninabeseni kabisa la michanga,kwajili tu yakukanyaga yani
nikiandika nakuwa confidant ata nikiandika nakuwa na amani”Alisema Mpoto Mpoto akiwa uwanja wa ndege Dar es salaam akirejea toka Dubai


Mpoto akiwa uwanja wa ndege Dar es salaam akirejea toka Dubai
Pia Mrisho ataendelea kufafanua kwanini ataki kubadilika na kuchana na tamaduni ya kutembea mbila kuvaa viatu

“Nataka maisha yasiniendeshe mimi,mimi niyaendeshe maisha, kwasababu unajua speed ya utandawazi yani globalization ni kubwa sana kuliko speed ya mwanadamu kwa Tanzania,ukiangalia watu kama Marekani wamepata uhuru miaka mia mbili iliyopita,sisi tuna miaka mingapi tu ya uhuru na teknologia inakuja kwa kasi sana,ndiyo maana technologia inapokuta Tanzania watu wanaimasta sana,kwamfano facebook,instargam,twetter,whatsapp na mitandao mingine vimekuja kwa kasi sana na watu vimewabadilisha sana,ata Ngugi wa Thiong’o alisema
huwezi kwenda kwa jirani kama ujatokea kwako,mtu kaka mimi ninapoigia kwenye technologia siwezi badilishwa kwasababu nimeshajijua mimi ni nani”Alimalizia Mpoto

MADAKTARI WASHINDWA KUUNGANISHA UUME WA MWANAMUZIKI ALIYE JIKATA MAKUSUDI.

Rapper mwenye uhusiano na kundi la Wu-Tang Clan, Andre Johnson hana tena kiungo kinachomfanya aitwe mwanaume kwakuwa madaktari wameshindwa kuunganisha.

Mtandao wa TMZ uliandika kuwa Johnson aka Christ Bearer aliukata uume wake jana Jumatano na kujirusha kwenye nyumba ya ghorofa mbili anakoishi huko North Hollywood kwa kile kinachodaiwa kutaka kujiua. 
 
Alikimbizwa kwenye hospitali ya Cedars-Sinai Medical Center lakini uume wako umedaiwa kukatika kabisa.

Johnson/Christ Bearer ni member wa kundi liitwalo Northstar, lilioanzishwa na rapper Wu-Tang Clan, RZA. 
 
Kulikuwepo na rappers wengine kwenye tukio hilo waliokanusha kuwepo na madawa ya kulevya kiasi cha kumfanya achukue uamuzi huo.

Lady JayDee - Nasimama (Official Video)

SHAKIRA ANA NDOTO ZA KUWA FISRT LADY WA TIMU YA BARCELONA

Mwimbaji wa Pop, Shakira ambaye ni mpenzi wa mchezaji wa timu ya Barcelona, Gerard Pique ameweka wazi nia na ndoto yake ya kuwa ‘first lady wa timu hiyo’.

Shakira anaamini kuwa siku moja Gerard Pique atakuwa rais wa Barcelona na hiyo itampa yeye nafasi ya kuwa first lady wa timu hiyo.

“Nafikiri siku moja Gerard atakuwa rais wa Barcelona na mimi nitakuwa ‘first lady’ wa Barca.” Shakira ameeiambia jarida la Bocas.

Kauli ya Shakira inaonesha kumuunga mkono mpenzi wake ambaye aliviambia vyombo vya habari vya Hispania kuwa huenda siku moja atakuwa rais wa Barcelona, “nani anajua, huenda siku moja ntakuwa rais wa FC Barcelona.”

Shakira na Gerard wako katika uhusiano wao kwa miaka minne na wamebarikiwa kupata mtoto wa kiume aitwae Milan

IYANYA KULIPWA $4000 NA SUTI MPYA ILI AWEZE KUONEKANA KWENYE VIDEO YA HABIDA.

Muimbaji wa Nigeria, Iyanya ameombwa alipwe kiasi kikubwa cha fedha kutokea kwenye video ya wimbo alioshirikishwa na msanii wa Kenya, Habida.

Habida amedai kuwa uongozi wa Iyanya umedai ulipwe $4000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 6.5 ili kuonekana kwenye video hiyo.

Pia walitaka Habida amnunulie Iyanya suti mpya ya kuvaa kwenye video hiyo.

Kama hiyo haitoshi, walitaka msanii wa mitindo binafsi na ukijumlisha vyote hivyo zaidi ya shilingi milioni 9 ilikuwa inahitajika.

“Sina uhakika kama Iyanya alikuwa anajua kinachoendelea. Sikuweza kutimiza matakwa hayo kwa muda huo na nimeamua kuutoa wimbo huo mapema,”
Habida aliiambia Heads Up ya Kenya.

Ray C Foundation yaandaa kipindi cha TV ‘Pamoja Inawezekana’ kitaelimisha jamii juu ya madawa ya kulevya

Msanii wa muziki Rehema Chalamila ‘Ray C’, kupitia Ray C Foundation ameanza kuandaa kipindi chake cha TV ‘Pamoja Inawezekana” ili kuendelea na jitiada za kuendeleza kuelimisha jamii juu ya madawa ya kulevya.

Ray C kupitia instagram yake amesema:Preparing my TV programme Pamoja Inawezekana,Ray C foundation inawaletea kipindi cha pamoja
inawezekana,stay tuned people more to come.

Kipindi maalum cha ‘Pamoja Inawezekana’ kitakujia hivi karibuni,makubwa mengi yatakuja kupitia Taasisi yetu,kwa walio mikoani tupigie 0658009715 au barua pepe raycfoundation2014@gmail.com,itakuwa na mambo mbalimbali yanayohusu matatizo au athari za madawa ya kulevya,tutawatangazia hivi
karibuni.

Ewe ndugu jamaa rafiki anaesumbuliwa na madawa ya kulevya usisite kuwasiliana na sisi tutakusaidia kwa hali na mali”Alisema Ray C


   

Labels