Pages

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Friday, March 08, 2013

TOP TEN TRACKS ZA REDIO KITULO FM [08 MACHI 2013].......BEST OF THE WEEK

10:-Simama Remix - Makomandoo ft Tunda Man,Amini,Barnaba,Banana Zorro.
09:-Niwe Nawe - Jux
08:-Nje ya Box [18] - NickII ft Joh Makini & G- Nako
07:-Dear Gambe - Young Kiler ft Belle 9
06:-Kesho - Diamond
05:-Nishai - Chibwa ft Juru
04:-Dole - Mabeste ft Deddy
03:-Usinibwage - Aika & Nareel
02:-So Crazy - Maua Sama ft Mwana FA
01:-Nikupe nini - Noorah ft Ali kiba

MTV YAMTAJA MC MKALI NAMBA 1 KWENYE GAME(MTV's HOTTEST MC's IN THE GAME 201


Kendric Lamar ametajwa kama Mc namba 1 mkali hivi sasa kwenye game kwa mujibu wa MTV.List hiyo ina wasanii 10 ambao kwa mujibu wa MTV ndo MC's wakali kwenye game hivi sasa.Namba mbili ni 2Chainz
 2Chainz  namba 2.
Rick Ross the big boss namba 3.
4.Nas
5.Drake
6.Big Sean
7.Kanye West
8.A$AP Rocky
9.Future
10.Meek Mill

PICHA ZA CHRIS BROWN AKIWA NA WIZKID WAKIFANYA VITU ON STAGE


Ni mara chache sana kwa wasanii wakubwa wa muziki Marekani wanaotoa ushirikiano mzuri wakati wanapokuja Afrika kupafom, sio tu ushirikiano mzuri bali hata kujichanganya na wasanii wa Afrika wanaokuwepo kupafom nae kwenye stage moja.
Time hii zali limemdondokea staa Wizkid wa Nigeria ambae kwa mara ya pili mfululizo mwimbaji staa Chris Brown amemuita kwenye stage na kupafom pamoja huko Ghana juzi ambapo kwa mara ya kwanza alimuita wakati akipafom kwenye mji wa Lagos Nigeria.
Uhusiano wa wawili hawa unazidi kukua na unatoa nafasi ya wengi kuamini kwamba kolabo au ushirikiano mkubwa zaidikwenye kazi za wawili hawa vinaweza kutokea muda wowote kuanzia sasa.
Ni stori ambayo imechukua headlines sana kwa sababu wasanii wengi wa Marekani wanapokuja Afrika wengine hukataa hata kupiga picha au kukaa sehemu moja backstage na wasanii wa Afrika, wengine pia hawaruhusu kabisa Video Camera iwachukue wakipiga picha na watu manake wanaogopa inaweza kutumika kibiashara.

KANYE WEST ACHUKIA KUWEKWA NAMBA 7 KWENYE LIST YA MTV HOTTEST EMCEES


Manager na C.E.O wa G.O.O.D MUSIC Rapper Kanye West,Amezungumza kwenye Show ya Angie Martinez wa HOT 97 na Kuzungumza na DJ Enuff Kuhusu Alivyojisikia yeye kukamata nafasi ya 7 kwenye orodha ya Mtv Hottest MCs.....
Yeezy Amemueleza Enuff kuwa Anadhani Rapper Lil Wayne ndo MCs Mkali zaidi kwenye game....amefurahi pia kuona Big Sean kuingia kweneye Top 5 but Yeye kama yeye alipaswa kuwepo kwenye Top 5 hiyo na sio namba 7.
Baba Huyo Mtarajiwa wa Kim Kardashian Ameendelea kusema; Hakuna
verse kali Mwaka Huu aliyoimba kwenye Remix ya wimbo wa Rihana
wa Diamonds...!
Pia Amemkumbusha DJ Enuff kuwa ni yeye ndie aliempa SWAY (Mwandaaji
wa MTV Hottest MCs) Kipindi cha kwanza cha Tv na Kisha akakata
Simu....!

Download | Jcb & Steph Waters Ft. Raf Mc - Hamna Shida [Audio]

UJUMBE KUTOKA KWA MSANII DAYNA KUHUSU SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.


Dayna
Naitwa Dayna Nyange. Mwanamuziki wa Bongo Freva. Ni Mwanamke wa KiTanzania. naungana na wanawake wengne duniani kote katika kuadhimisha Siku ya wanawake duniani.  Nawashauri wanawake wenzangu juu ya kujituma kufanya kaz ili kujipatia maendeleo bila kutegemea wanaume. 
 
Naamini  wenyewe tunaweza  tena bila ata ya kuwezeshwa.  Nakupitia siku hii muhimu kwetu naiomba serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kuhakikisha inapambana vilivyo juu ya unyanyasaji wa kijinsia  tunaoupata wanawake. 
 
hasa ubakaji, ukeketaji na  mauaji yanayoendelea zidi  yetu, tunaiomba serikali ihakikishe kwamba wahusika wa matukio kama hayo wanachukuliwa hatua za haraka ili kukomesha maovu hayo. 
 
Pia nijukumu la kila mwanamke na  Niwajibu wetu kina Mama pia na jamii kwa jumla kupambana na majanga haya. tushikamane kujiletea. Tupendandane tushikamane WANAWAKE TUNAWEZA By Dayna Nyange.

PICHA 2: COVER ART YA ALBUM MPYA YA TYGA WA YOUNG MONEY NA LA SNOOP DOGG.

Cover La Album Mpya Ya Rapper Tyga Wa Young Money Hotel California .
Cover La Album Mpya Ya Snoop Dogg `Reincarnated' Inayotoka April 23.

[INTERVIEW]:-MABESTE AKIZUNGUMZIA DHAMIRA YA WIMBO WAKE WA DOLE ALIOMSHIRIKISHA DEDDY


WIMBO ULIOTOKA MAALUM KWAAJILI YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Ni Kina dada watatu kutoka Nyumba ya Vipaji Tanzania, The TRIO, wametoa wimbo wao mpya unaoitwa, ‘PAMBO’ ambao ni maalumu kwa ajili ya kuadhimisha siku ya wanawake duaniani.

Kundi hilo ambalo limekuwa kwenye muziki kwa muda mrefu kidogo, sasa wameamua kutoa wimbo huo ikiwa ni maandalizi ya ujio wao kamili mwishoni mwa mwezi huu.

Pamoja na wimbo huo, The TRIO pia wametoa video ya live performance ya wimbo wao wa ‘FALL IN LOVE’ ambayo ilirushwa kwa mara ya kwanza kwenye vituo vya luninga wakati wa sherehe za Valentine mwaka huu.

Kundi hilo linaundwa na kinadada watatu machachari, Angella Karashani (Malaika), Alice Kibopile (Alice) na Khadija Maige (Kadja)

Wimbo umerekodiwa studio ya Sourround Sound, chini ya mtayarishaji Ema The Boy.

Thursday, March 07, 2013

RAPA GUCCI MANE ABADILI MAWAZO BAADA YA KUTANGAZA JINA JIPYA.!


Baada ya kutambulisha jina lake jipya kupitia mtandao
 wa kijamii wa twitter, Gucci Mane ameamua kubadili mawazo
 hayo muda mfupi na kuamua kurudia jina lake hilo hilo.
Gucci Mane alitangaza kubadili jina na kujiita "Guwop" mapema leo
 hii, lakini baada ya muda mfupi alibadilisha mawazo na kuamua 
kubaki na jina lake.
rapa huyo kutoka atlanta, Georgia,aliandika kupitia twitter leo hii 
kutangaza jina hilo jipya, ambapo aliandika  kuwa rasmi ataanza
 kujulikana kama Guwop itakapofika tarehe 2 july
"July 2nd I'm officially changing my rap name to Guwop and
 retiring the great GucciMane Thanks Fans, for 8 years as Gucci 
now it's Wop turn," aliandika
lakini muda mfupi baada ya kubadili jina lake, alirudi na kuandika
 tena kuwa atabaki kuwa na jina hili hilo Gucci Mane kwasababu
 mashabiki wake wameamua hivyo.
 "I am officially NOT changing my name to Guwop it will 
officially stay Gucci Mane due to my Fans' response.. Trap 
House 3 & Juug House July 2" aliandika 
Gucci angekuwa mmoja wa ma MC walioamua kubadili majina yao
 publicly kama angebaki na wazo hilo, kama unakumbuka Snoop
 Dogg aliamua kubadili na sasa anajiita Snoop Lion, Mos Def hivi
 karibuni kawa Yasiin Bey na N.O.R.E. amekuwa P.A.P.I.
 Gucci kwa sasa ameachia mixtape yake mpya Trap God 2 na
 Free Bricks 2 akiwa na Young Scooter

[NEW HIT]:YOUNG SUMA FT NYEMO - DON'T GIVE UP

KARIBU DAR - UJIO MPYA WA KALA JEREMIAH

Kala Jeremiah ambae anafanya fresh sana kwenye Game ya Muziki wa Hip Hop amefunguka mapema leo kuhusu ujuio wake mpya na project yake na Roma ambayo ilianza mwaka 2011 na kusimama kwa muda, Kala alisema.

"mWAKA 2011 MIMI KWA KUSHIRIKIANA NA ROMA TULIANZISHA TOUR YENYE LENGO LA KUWAFIKIA WATANZANIA KOTE NCHINI HASA WAKULIMA, WAFUGAJI, WAVUVI, WACHIMBAJI WADOGOWADOGO WA MADINI,NA WATU WENGINE WA AINA HIYO. LENGO LA SISI KUFANYA HIVYO ILIKUWA NI SISI KUONGEA NA WATU KUJUA CHANGAMOTO WANAZOKUTANA NAZO KATIKA MAISHA YA KILA SIKU,PIA KUJUA UMASKINI HALISI WA MTANZANIA.KUJUA HISIA ZAO, MAONI YAO, NA NINI WANGEPENDA KIFANYIKE,.

PROJECT HII ILIKUWA NA MAMBO MENGI SANA.TULIFANIKIWA KUANZA NA KANDA YA ZIWA AMBAKO TULIFANIKIWA KUKUTANA NA WAVUVI, WACHIMBAJI WADOGOWADOGO WA MADINI,NA WATU WAISHIO KARIBU NA MIGODI. KWA KUWA ILIKUWA NI MWANZO TULIISHIA HAPO KWANZA NA TULISITISHA KUTOKANA NA KUBANWA NA MAJUKUMU MENGINE YA KIKAZI LAKINI IKIWA NI PAMOJA NA UFINYU WA BAJETI KWA KUWA TULIKUWA TUNATUMIA HELA ZETU NA HATUKUWA NA MDHAMINI.

PROJECT HII IKO HAI NA ITAENDELEA TENA MWAKA HUU KWA KISHINDO. 

LAKINI WAKATI TUNAFANYA PROJECT HII NILIGUNDUA PIA KUWA VIJANA WENGI WAISHIO MAENEO TULIYOYATEMBELEA WANAAMINI KUWA ILI WAFANIKIWE NI LAZIMA WAJE DAR YANI WANAAMINI DAR ES SALAM NDO SEHEMU YA KUTOKEA KI MAISHA, HILO MIMI BINAFSI SIKULIPENDA HATA KIDOGO NA KWA KUWA MIMI NAISHI DAR NA NAJUA KUWA DAR KUNA WATU WANAMAISHA MAGUMU SANA. KWA HIYO NILIPORUDI DAR NILIFANYA UCHUNGUZI USIO RASMI WA MAISHA HALISI YA MTU WA KAWAIDA WA DAR NILIYOYAGUNDUA KWENYE UCHUNGUZI HUO NILIYAANDIKA YOOTE NA KUYATENGENEZEA WIMBO UNAOITWA KARIBU DAR. 

KARIBU DAR NIMEJITAHIDI KUONGEA UKWELI WA MAISHA HALISI YA WATU WA KAWAIDA WA DAR. LENGO LA KUFANYA WIMBO HUU NI KUTAKA KUMJULISHA MTU ALIYEKO SEHEMU NYINGINE NA ANAAMINI KUWA DAR NDO SEHEMU PEKEE ATAKAYOTOKEA KI MAISHA.KWA KIFUPI KARIBU DAR NI WIMBO UNAOELEZEA MAISHA MAGUMU YA WATU WA KAWAIDA WA DAR LENGO LA KUFANYA WIMBO HUU NI KUHAMASISHA VIJANA WAKAE WALIPO NA WAZITUMIE VIZURI FURSA WALIZONAZO KULIKO KUKAA NA KUOTA KUWA DAR NDO KUNA MAISHA MAZURI.

WIMBO HUU NIMESHIRIKIANA NA MKALI WA RNB BEN POL NA WIMBO UKO TAYARI NA UMEFANYIKA KWENYE STUDIO ZA SMART MUSSIC CHINI YA MUANDAAJI PRODUCER MBEZI NA VIDEO YAKE IMEFANYIKA NEXT LEVEL CHINI YA DIRECTOR ADAM JUMA KILA KITU KIKO SAWA SO KAA MKAO WA KULA KUANZIA WIKI IJAYO KINANUKA.NAOMBA MAPOKEZI YAKO. ASANTE SANA"

[COMING SOON tRACK]:I 2the Y - IMANI YA MOYO

Baada ya kuachia Track yake inayoenda kwa jina 'USINIACHE' Msanii I 2The Y [Emma B] amesema yupo kwenye hatua za awali za kuaanda Hit yake nyingine mpya ambayo itafanyika katika Studio za Suma Records kwa Yule yule producer wa Ngoma yake ya kwanza na ngoma hiyo inaenda kwa jina la 'IMANI YA MOYO',Joint hiyo inatarajiwa kuachiwa mwezi wa tano mwanzoni kwa mashabiki wa I 2The Y kaeni mkao wa Burudani zaiiiiidi.

[NEW HIT....VERY HOT]:LADY JAYDEE ft pROF JAY - JOTO HASIRA


Monday, March 04, 2013

[PICHA]- UTENGENEZWAJI WA VIDEO YA YOUNG KILLER FT BELLE 9 - DEAR GAMBE.











Sunday, March 03, 2013

[MICHEZO]:-WEKUNDU WA MSIMBAZI "SIMBA SC YATOLEWA KLABU BINGWA"

Wawakilishi wengine wa Bara katika michuano hiyo, Simba SC wametolewa baada ya kufungwa mabao 4-0 na Recreativo de Libolo ya Angola kwenye Uwanja wa Manispaa mjini Calulo, Angola.

Matokeo hayo, yanaifanya Simba itolewe kwa jumla ya mabao 5-0, baada ya awali kufungwa bao 1-0 Dar es
Salaam.

Hadi mapumziko, Libolo walikuwa mbele kwa bao 1-0, lakini kipindi cha pili ndipo hali ikawa mbaya zaidi kwa Wekundu wa Msimbazi baada ya kutandikwa mabao hayo matatu na kuwa 4-0.


Simba ilicheza vizuri kipindi cha kwanza, lakini Recreativo walitumia zaidi upande wa kushoto kushambulia, ambako walimzidi beki Amir Maftah na kumgeuza uchochoro.

Na hata bao hilo la kwanza lilitokana na Maftah kuzembea kuokoa mpira hadi mfungaji akaingiza mguu kutokea nyuma yake na kufunga.


Kipindi cha pili, Simba ilifanya mabadiliko, ikiwatoa Amir Maftah na kumuingiza Kiggi Makassy kwenda kucheza beki ya kushoto, wakati Mrisho Ngassa alikwenda kuchukua nafasi ya Chanongo.


Mabadiliko hayo hayakuisaidia Simba SC, kwani Kiggi alikwenda kuwa uchochoro zaidi kuliko Maftah na Libolo wakapitia huko kutengeneza mabao yao, waliyoyapata dakika 15 za mwishoni.


Hata mabeki wa kati nao, waliwaruhusu wachezaji wa Angola kuruka peke yao kwenye mipira mingi ya juu, hivyo kufunga kwa urahisi.

Kikosi cha Simba kilikuwa; Abbel Dhaira, Nassor Massoud ‘Chollo’, Amir Maftah/Kiggi Makassy, Komabil Keita, Juma Nyosso, Shomary Kapombe, Amri Kiemba, Abdallah Seseme, Haroun Chanongo/Mrisho Ngasa, Felix Sunzu na Salim Kinje.

BAUCHA RECORDS KUTIMIZA MIAKA KUMI MWEZI HUU

Mwezi huu [Machi] 2013 Baucha Records Inatimiza miaka kumi sasa tangu kuanza kwake na Inampango wa kurudisha Talent Show itakayoanza Lindi na Mtwara mwezi Huu Then Mikoa ya Iringa na Mbeya mwezi Ujao yaani mwezi wa Aprili na mikoa mingine itafuata na washindi wataondokanao mpaka Dar es salaam kwaajili ya kufanyanao kazi na kazi hizo zitasambazwa Redioni.

Akipiga Stori kwanjia ya simu Leo asubuhi na Ergon Elly wa Kitulo Fm na Mmiliki wa Mtandao Huu Producer Mkongwe katika Industry Hii ya muziki wa kizazi kipya ALLY BAUCHA amesema katika pitapita huko wasanii kibao watapiga show akiwepo mwenyewe Baucha, K-One,Baghdad watapiga Show huko mikoani kwa Kijana mwenye kipaji jipange kwa wakati ndio huu wa kutoka kwao.

Na kama itawezekana Producer huyo na Msanii ambaye amenanya poa na Track yake ya Kelele aliyomshirikisha Ali Kiba atatambulisha ngoma katika Msimu huo wa kuadhimisha siku ya kuanzishwa kwa Baucha Records

[TOP 20]:-REDIO KITULO FM MACHI 2013

20;-Nje ya Box - Nick ii ft Joh Makini & G-nako [Ingizo Jipya]
19:-So Crazy - Maua Sama ft Mwana Fa [Ingizo Jipya]
18:-Mahakama ya Mapenzi - Linex [20]
17:-Sina noma nae - Mc koba [13]
16:-Bonge la Bwana - Shetta ft Linna[05]
15:-Narudi kazini - Beka Ibrozama [For 2 weeks]
14:-Dear God - Kara Jeremiah [12]
13:-Dole - Mabeste ft Deddy [For 2 weeks]
12:-Always - Country Boy ft T.I.D [18]
11:-Mama yeyo G-nako ft Ben Pol [09]
10:-Money - AY ft Vanessa [For 2 weeks]
09:-My Everythin' - Ali kiba [09]
08:-Me & U - Ommy Dimpoz ft Vanessa [08]
07:-Nikupe nini - Noorah ft Ali kiba [14]
06:-Listen - Belle 9 [16]
05:-Dear Gambe - Youn' Killer ft Belle 9 [06]
04:-Nishike Mkono - Darasa ft Winnie [-]
03:-Wazo la leo - Stamina ft Fid Q [For 2 weeks]
02:-Jambo Jambo - Steve RnB [For 2 weeks]
BONUS TRK:-Sio Mimi - Madee
01:-Kesho - Diamond Platinumz [For 2 weeks]

Kwa Ushauri/Maoni:-ergonsanga@yahoo.com au 0755 894 663.
Jumapili Njema!!!

Labels