Pages

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Friday, January 18, 2013

KUMI KALI ZA REDIO KITULO FM IJUMAA 18/01/2013

10;-Dear God - kala Jeremaih
09;-Ngoma Moja - Team Racerz
08;-Me & U - Ommy Dimpoz
07;-Utamu - Dully ftn Diamond & ommy Dimpoz
06;-Si kosa Lake - EMG
05;-Kinyulinyuli - Samir
04;-Wazo la Leo - Stamina ftn Fid Q
03;-Bonge la Bwana - Shetta ftn Linnah
02;-Kesho - Diamond Platnumz
01;-2030 - Roma

Suma Mnazaleti Kuja Na "Tuko Wangapi" Hivi Karibuni

      
Hit-Maker wa track ya Chukua Time maarufu kama Suma Mnazaleti sasa yuko mbioni kuachia ngoma yake nyingine inayokwenda kwa jina la Tuko Wangapi huku akiwa amemshirikisha Tundaman.

Suma amesema kuwa ngoma hiyo inazungumzia namna mapenzi ya uongo yalivyo huku wanawake wengi wakiwa na wanaume wengi na mwisho wa siku anaamua kuweka na kuuliza Tuko Wangapi kwa lengo la kutoa utata na kuyakimbiza matatizo yanayoweza kutokea.

Pia aliongeza kwa kusema kuwa wimbo huo pia utakuwa ni fundisho kwa wanaume wengi wanaopenda kuona mwanamke na kutokujua nguo anazovaa zimetoka wapi, badala yake wanafurahi na hawajui kuwa wanaume wengi wanakula tunda. Hivyo basi, mashabiki wa Suma kaeni tayari kwa ujio mwingine kutoka kwake.

UJIO MPYA WA RAPPER CHAMILLIONAIRE.

Rapper Chamillionaire yupo tayari kurudi na Project Mpya ya Elevate. 

Rapper huyu from Houston alitangaza project hii kwenye facebook page yake nakusema, FEB 12th on www.chamillionaire.com. The first 500 copies will be autographed and each autographed copy will be numbered. 

Thursday, January 17, 2013

MSANII RAMA D NAYE AZUSHIWA KIFO


Zile death hoaxes zilizokuwa zikiwakumbuka wasanii wa Marekani zimeanza kuchukua nafasi kwa wasanii wa Tanzania ambapo kumeanza kuzuka mchezo wa watu kuwazushia vifo wasanii wa Bongo.

Baada ya Profesa Jay kuzushiwa kifo wiki hii, Rama Dee naye amesema kuna watu wamezusha kuwa amefariki.Kupitia Facebook, Rama Dee ambaye kwa sasa yupo nchini Australia amelaani kitendo hicho na kuwataka ‘haters’ wasubiri mwenyezi Mungu aamue mwenyewe.

“Huu mchezo wa kuzushia watu wamekufa sio poa kabisa…inaonyesha ni jinsi gani akili yako ilivyo na matope ya ushamba na uchafu wa ulimbukeni….juzi mchizi wangu ametumiwa msg kuwa mimi nimedanja sio inssue subirini siku ikifika nikidanja mtapata habari ya kuandika kwenye page zenu Au blogs ila kwasasa punguzeni mizuka ya kise**e ni hayo tu asante,” ameandika mkali huyo wa R&B nchini.

WASANII 9 KUTUMBUIZA KWENYE UZINDUZI WA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA 2013

Ayanda-Nhlangothi
Wasanii 9 wamepewa shavu la kutumbuiza kwenye sherehe za uzinduzi wa kombe la mataifa 2013 nchini Afrika Kusini.

Wasanii hao ni pamoja na Oumou Sangare wa Mali , Eric Wainana wa Kenya, Judith Sephuma, Lira, Siphokazi, Ayanda Nhlangothi Afurukan, Sipho ‘Hotstix’ Mabuse na Ringo Madlingozi wa Afrika Kusini.

Ufunguzi huo wa The Orange Africa Cup of Nations SOUTH AFRICA 2013 utafanyika Jumamosi hii, 19 January kuanzia saa kumi jioni kwa saa za Afrika Kusini. 

Utafuatiwa na mechi ya Bafana Bafana na Cape Verde.

MWANA FA KUJA NA THE FINEST HIVI KARIBUNI

       
Msanii anayefanya poa na kazi yake ya Yalaiti maarufu kama Hamis Mwinjuma aka Mwana Fa sasa yuko mbioni kuachia kitu kipya kitakacho kwenda kwa jina la The Finest.

Mwana Fa amepost picha hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, hivyo mashabiki wake kaeni tayari kwa kitu hicho kipya kutoka kwa rapper huyo.

H BABA SASA KURUDI DAR AKITOKEA MWANZA

NYOTA wa filamu na muziki wa kizazi kipya, Hamisi Ramadhani ‘H.Baba’ anatarajia kurudi toka Mwanza alipokuwa na mpenzi wake Frola Mvungi ambapo walichukuwa mapumziko ya miezi miwili kuja Dar es salaam kwaajili ya kuachia ngoma yake mpya Funga Zipu.

Wednesday, January 16, 2013

BARNABA AZUNGUMZIA MALENGO YAKE KATIKA MUZIKI WA BONGO FLEVE BAADA YA KURUDI


Msanii wa kizazi kipya kutoka THT  naanayefanya poa hapa bongo na nje kupitia kazi zake maarufu kama Barnaba baada ya kumaliza ziara yake huko London sasa pia ana mpango wa kufanya vitu vizuri vipya katika tasnia hii ya muziki soma huu ujumbe aliyoandika kupitia katika ukurasa wake wa twitter.

Nikki Mbishi Ampa Stamina Ubunge Wa Morogoro

       
Rapper kutoka MLab, Nikki Mbishi hivi karibuni alimpa rapper mwenzie Stamina, ubunge wa Morogoro kwa kumfananisha na Mh. Joseph Mbilinyi [SUGU] ambae ni mbunge wa Mbeya Mjini

Nikki Mbishi aliyasema haya hasa kwa kuonekana kukubali anachofanya Stamina kupitia mtandao wa kijamii wa twitter, na kuandika "Stamina is our new SUGU, mbunge wa Morogoro".

      
Hii ni heshima kubwa sana aliyompa Stamina hasa kwa kumfananisha na SUGU, hasa ukizingatia Nikki Mbishi ni msanii mkubwa kuliko Stamina

Hii inaonesha ni jinsi gani Nikki Mbishi anamkubali rapper huyu from Moro Town, Well hii ni nzuri, hasa wasanii kwa wasanii wanapoonekana kusikiliza, kutambua, na kukubali kazi zinazoendelea kwenye industry hii ya muziki wetu.
       
Stamina ni msanii anaefanya miondoko ya Hip-Hop [Kama ilivyo kwa Nikki Mbishi] mwenye chimbuko la Morogoro anaefanya vizuri sana katika muziki huo hapa Tanzania. Punchlines, Bars, Mashairi n.k. ni baadhi ya vitu anavyovimiliki rapper huyu. Kwa sasa, Stamina anatamba na track yake mpya ya WAZO LA LEO akiwa amemshirikisha Fid Q na anatarajia kuachia album yake mpya yenye tracks 22 hivi karibuni.

FID Q: VIDEO YA WAZO LA LEO ITASHUTIWA WIKI IJAYO

Stamina na Fid Q baada ya kuachia ngoma yao mpya inayokwenda kwa jina la Wazo la leo na kupeleka mashabiki wengi wa Hip Hop kuwa kubali wasanii hawa wawili katika tasnia hii ya muziki.
 
Sasa leo fareed kubanda a.k.a Fid Q aliamua kufunguka kupitia katika ukurasa wa twitter baada ya kuulizwa na shabiki wake kuhusu video ya wazo la leo na akamjibu kwamba wanatarajia kufanya shooting ya ngoma hiyo wiki ijayo.
 
Kama wewe ni shabiki wa Stamina au Fid Q kaa tayari kwa ujio huo mpya kutoka kwa wasanii hawa wawili.

NGWEA KUJA NA NGOMA MAALUMU KWA SIKU YA WAPENDANAO



Rapper Albert Mangwea aka Ngwair amesema wapendanao wajiandae kusikiliza ngoma yake special kwaajili ya siku ya yao, Valentine’s Day, February 14.

Ngwair ameiambia Bongo5 kuwa ngoma hiyo aliyoifanya AM Records chini ya producer Manecky inaitwa ‘Alma’.

 Amesema Alma itatoka siku mbili kabla ya Valentine’ Day na itakuwemo kwenye albam yake mpya iitwayo MIMI 3.

Ameongeza kuwa Ngoma hiyo 'Mimi 3 'itatoka mwezi April mwaka huu.

Tuesday, January 15, 2013

VIDEO YA WIMBO WA BELLE 9 "LISTEN" KUACHIWA TAREHE 18 MWEZI HUU

Belle 9 baada ya kutambulisha ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Listen kwa mashabiki wake,sasa leo ameweka siku ya kutoa video yake mpya ya Listen ambayo anatarajia kuichia siku ya tarehe 18 mwezi huu.

WEMA SEPETU AACHIA LOGO YA KAMPUNI YAKE "Endless Fame Film. "

    
 Mwanadada machachari kutokea kwenye Industry ya Filamu Tanzania, Wema Sepetu kwa mara ya kwanza kupitia mtandao wa picha unaoitwa Instagram ameachia picha ambayo inaonesha ni logo ya kampuni yake mpya ya Endless Fame Film

Kampuni ambayo aliitangaza kipindi cha nyuma ambayo itakuwa inajihusisha na maswala ya filamu Tanzania.

 Sambamba na kuachia picha hiyo Wema amewataka Watanzania kumwombea Dua ili kufanikisha adhma yake hiyo ambayo itakuwa na msaada mkubwa kwenye sanaa ya filamu Tanzania na hata kuinua vipato vya Wasanii.

CLOSER YA VANESSA MDEE YAVUKA BODA NA KUTIKISA ANGA ZA MBELE

Mtangazaji wa Choice FM 102.5 maarufu kama Vanessa Mdee baada ya kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Closer,sasa tumefahamu kwamba ngoma hii inazidi kukubali na kuchezwa na ma Deejayz na radio mbalimbali za nchini Kenya.Big up to her!!!!!!!!!!!!

Man Walter Amaliza Beef Yake Na Wasanii Wote Akiwemo 20%.


    
Producer wa muziki maarufu nchini, Man Walter [Pichani, Kushoto] atangaza kumaliza beef zake zote alizokuwa nazo na wasanii. Akizungumza na radio moja maarufi nchini, Man Walter alizungumza kumaliza matatizo yote aliyokuwa nayo na wasanii ikiwemo hata yale ambayo hayajui

 Akizungumzia kuhusu 20%, Man Walter alisema beef yake na 20% ni moja ya matatizo ambayo yalikuwepo na sasa hayataki tena  yuko tayari kufanya kazi na msanii yeyote akiwemo 20%.
     
Akiongelea beef zingine Man Walter alisema wapo wasanii au watu ambao unaweza kuwa na matatizo nao bila kujua, mtu ana beef na wewe ya kichini chini lakini mimi nimeyamaliza yote.

Kipindi fulani nyuma, producer Man Walter aliingia kwenye beef na 20% na kushindwa kuendelea kufanya kazi na msanii huyo ambaye wamefanya kazi nyingi pamoja.

Jay-Z Na Beyonce Wamnunulia Blue Ivy Carter Mdoli Wenye Thamani Ya $80,000

    
Katika kusheherekea tarehe yake ya kuzaliwa... The power couple [Jay-Z & Beyonce] wamnunulia Blue Ivy Carter mdoli wenye thamani ya dola za kimarekani 80,000... Damn!!
    
Mdoli huyo mwenye thamani hiyo, akiwa ametengenezwa na kupambwa sehemu kubwa kwa almasi, alinunuliwa na wanandoa hawa kama zawadi kwa Blue ambaye ametimiza mwaka mmoja jumatatu iliyopita toka kuzaliwa kwake.

Barbie Doll amekuwa ni sehemu tu ya furaha hii, kwani pia Jay-Z na Beyonce wamemuandalia mtoto wao sherehe kubwa Blue Ivy ambayo inagharimu pauni za kiingereza 60,000 na cake yake ya birthday yenye thamani ya pauni 1,500 za kiingereza.

    
Jay-Z na Beyonce wameripotiwa kutokuwa na tatizo katika kumfanyia mtoto wao huyo chochote kitakachoweka alama katika maisha yake yote ambapo kwa sasa wanatambulika duniani kama ma-star wanaolipwa hela nyingi pamoja katika mahusiano yao. Jay-Z Na Beyonce wanalipwa dola za kimarekani 78 milioni kwa mwaka.
Jay-Z na Beyonce wamekuwa kwenye maandalizi haya ya kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa mtoto wao kwa wiki kadhaa sasa... just to make the best of it.

Monday, January 14, 2013

Team Racers - Ngoma Moja (Official HD Video)

Q CHILLAH: WALIO NICHUKIA NDIO WAMENIFANYA KUINGIA KWENYE MADAWA YA KULEVYA


Q Chilla amesema kuingia kwake kwenye matumizi ya madawa ya kulevya ilisababishwa na baadhi ya watu kuchangia kumrudisha chini na kujikuta yuko peke yake katika mitihani aliyokuwa akipitia.  

Huku akikataa kuwataja kwa majina alisema watu hao walihakikisha kila anachokifanya hakifanikiwi na kujikuta katika wakati mgumu.  Qchilla amesema alishindwa kujua amemkosea nani au nani amuombe msamaha.
Hata hivyo anasema anawashukuru watu wake karibu waliokuwa wakisikitishwa na hali aliyokuwa nayo na kuamua kumshauri aache kutumia madawa hayo.

Alipoulizwa anawashauri vipi wasanii ambao wametumbukia kwenye matumizi hayo alisema njia pekee ni kukubali kuwa wana tatizo na kuishika dini.
Pia aliipongeza hatua ya rais Kikwete kumsaidia Ray C ambaye pia alikuwa aliingia katika wimbi hilo akitolea mfano wa rais Nelson Mandela aliejaribu kumsaidia mwanamuziki Brenda Fassie na Rais Obama aliemsaidia marehemu Whitney Houston na kusisitiza wasanii wote ambao ni waathirika wa madawa ya kulevya kujitokeza ili wasaidiwe na jamii.
QChilla amesema kwa sasa anafanya muziki akilenga soko la kimatafifa zaidi akiwatolea mfano PSquare na kusema tatizo la wanamuziki wengi kuishia kusikika nchini tu ni kujiwekea mipaka na kulenga soko la ndani tu na kumalizia hana mpango wa kutoa album badala yake ataendelea kutoa nyimbo kali.


kwa Hisani ya Clouds fm

WABABA WA EBSS-2012 AKABILIWA NA KESI YA KUTEMBEA NA MWANAFUNZI

 Mapenzi yao yalianza tangu binti akiwa kidaato cha tatu lakini halikuwa penzi lenye mashamu shamu kwa kuwa wababa alikuwa bado hajamiliki pesa na heshima katika jamii inayomzunguka kama sasa mara tuu baada ya kuchukua kifuta jasho cha EBSS na vijihela alivyopewa na mapapaa waliokubali kazi aliioifanya EBSS hivyo kuwa na
kiburi kilichomfanya amtie mimba mwananfunzi ambae aligundulika kuwa ametoa mimba mara taarifa za mahusiano ya wababa na mwanafunzi huyo kufikishwa kwa mama mzazi wa binti huyo. 
Wababa aliwekwa ndani kwa muda wa siku mbili na kesi bado ipo mahakamani na wazazi wa binti wameapa kumweka ndani wababa na kumfanya kama Babu Sea huku binti akiwa hajaonekana siku ya 4 sasa na kutokujulikana alipo kwa madai anampenda wababa na wakimfunga tu nae anakunywa sumu.

Hatimaye Lady Jaydee Amaliza Ziara Yake Ya Kupanda Mlima Kilimanjaro.

        

Msanii Lady Jaydee hatimaye jana ndio amaliza ziara yake ya siku sita ya kihistoria ya kupanda mlima wa Kilimanjaro.

Ziara hiyo ambayo alianza siu ya January 8 akiwa na lengo la kutangaza utalii wa ndani ya Nchi ya Tanzania huku akiwa ameongozana na mumewe Gadner G Habash ambae pia ndio msimamizi mkuu wa kazi zake zote.

Msafara wa Lady Jaydee uliwasili jana katika lango kuu la Marangu saa kumi na Mbili Jioni na kupokelewa na mhifadhi mkuu wa Hifandi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Bw. Erastus Lufungilo.

Labels