kwa wakati huo.
Wasanii waliopitiwa na panga hilo ni pamoja na mwimbaji mrembo Avril ambaye taarifa za hivi karibuni zinasema anategemea kuhamishia makazi
yake Afrika Kuisni, yaliko makazi ya mchumba wake wanaetarajia kufunga ndoa hivi karibuni.
Colonel Moustapha na Kenzo.
“Kila mara mashirika hufanya mapitio ya ndani kutathmini utendaji dhidi ya matarajio.
Wakati wa mapitio, maamuzi magumu hutakiwa
kufanyika”.
Ilisema taarifa kutoka kwa Lucas baada ya GHAFLA kutaka kupata ufafanuzi.
“Sehemu ya matarajio yetu imekuwa ni kutafuta na kutoa vipaji ambavyo vinaweza kushindana nje ya Afrika Mashariki.
Katika siku za nyuma mfumo huu umeweza kufanya kazi vizuri sana.
Hata hivyo, sekta ya burudani imebadilika kwa haraka na uwekezaji uliohusika kuleta mafanikio unakuwa kila siku.
Kama biashara, uwekezaji ni lazima ulete faida ndani ya wakati uliokusudiwa.
Hii itaruhusu uwekezaji mpya ili uchumi ukue. Na hii inawezekana tu katika mazingira ambapo vipaji vinavyohusika vinapotambua kuwa hata kama kuna kushinda ama kushindwa ni lazima uendele kujitahidi kadri ya uwezo katika kazi iliyo mbele.
Hakuna mbadala wa kufanya kazi kwa bidii, malengo na nidhamu.
Mtindo wa biashara wa sasa wa kusaini vipaji ni hatari sana na una assumptions nyingi mno.
Sehemu ya tathmini inayoendelea inahusisha na
kuangalia mtindo huu na umuhimu wake katika hali ya sasa.”
Hata hivyo Lucas hakutoa majibu ya moja kwa moja kuhusu wasanii wanaodaiwa kupoteza nafasi zao Ogopa deejays.
*Source: GHALFA*




























