Pages

Saturday, February 09, 2013

Venance Mushi achukua fomu Big Brother

MSHINDI wa pili shindano la Maisha Plus 2012, Venance Mushi aliyekuwa akiwakilisha Mkoa wa Dodoma, amechukua fomu ya kushiriki shindano la Big Brother Africa 2013.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Venance alisema kuwa, ameamua kuchukua fomu hiyo ili kujaribu nafasi ya kuiwakilisha Tanzania kwenye shindano hilo, kutokana na uwezo alionao, ikiwemo wa kuzungumza lugha zaidi ya tatu na kipaji chake.

“Tayari nimeishachukua fomu na nimeshaijaza, natarajia kuirudisha muda wowote kuanzia sasa, naomba wadau waniombee ili kuweza kupita katika usaili hapo baadaye,” alisema Venance.

Pia aliongeza kuwa, uwezo alioonesha Maisha Plus 2012, umempa umaarufu mkubwa, huku akiahidi kufanya vizuri endapo atapata nafasi hiyo mwaka huu.

Venance ambaye ni msomi wa elimu ya juu katika masuala ya mipango na maendeleo, aliyosomea Chuo cha Mipango Dodoma, alionesha kiwango cha hali ya juu kwenye shindano la Maisha Plus, ikiwemo kuyazoea maisha ya kijijini na ubunifu ambao ulimfanya kupata mali na fedha nyingi.

Aidha, mbali na Venance, tayari mastaa wengine wameshajitokeza kuchukua fomu za kushiriki shindano hilo akiwemo aliyekuwa Miss Tanzania 2006 na muigizaji wa filamu, Wema Sepetu.

Fomu hizo zimeanza kutolewa katika ofisi za Dstv na kwa njia ya mtandao wa kampuni ya Multichoice Tanzania.

0 maoni:

Post a Comment

Labels