Pages

This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

Sunday, February 10, 2013

LADY IN RED 2O13....TONIGHT..... MAANDALIZI,SERENA HOTEL....!!


RED CARPET UNAPOKAGULIWA TICKET MPAKA UNAPOINGIA.....
LADY IN RED INAFANYIKA DAR,SERENA HOTEL...!!
HAPA WATENGENEZAJI STAGE NA UKUMBI WAKIWA BUSY KUWEKA
MAMBO SAWA....!!

Rapper LL Cool L amebadilisha Jina na Cover la album yake mpya ya mwaka 2013 Na Kuipa jina la Authentic Hip Hop


Rapper LL Cool L amebadilisha Jina na Cover la album yake mpya ya mwaka 2013 Na Kuipa jina la Authentic Hip Hop na itatoka May 7 2013. Hapo Chini ndio List ya Nyimbo kwenye cd Hio. 
 
1. Something About U (FTW)
2. Where Ya At (BOSS)
3. Take It (feat. Joe)
4. Closer (feat. Monica)
5. Too Late
6. New Love
7. Dream With Me
8. Girl So Bad
9. Ratchet
10. Bartender Please
11. Bath Salt
12. Getting Paper
13. Jump On It
14. Hell Yeah
15. Whaddup

Goldie Kutengeneza Album Itakayogusa Bara La Africa

 
Mwanamuziki kutoka Nigeria, Goldie Harvey famously known as "Goldie" anataraji kutengeneza album ambayo itagusa kila kona ya Africa

Goldie ambae pia alikuwa mshiriki wa shindano la Big Brother Africa la mwaka jana ameyasema hayo katika interview aliyofanya na MTVBase Africa hivi karibuni.
Katika kufanikisha hilo, Goldie anataraji kufanya album hiyo ambayo bado hajaipatia jina na atleast wasanii 10 bora kutoka Africa ambapo mpaka sasa ameshafanya singles tatu ambazo zitatangulia, ikiwemo SKIBOBO featuring AY (@AyTanzania) kutoka Tanzania, MILIKI feat. Navio kutoka Uganda na GIVE IT TO ME akimshirikisha J.Martins kutoka Nigeria.
Goldie amekuwa akifanya vizuri sana kwenye muziki hasa baada ya kutoka kwenye Jumba la BBA-StarGame mwaka jana, ngoma zake zikisikilizwa sana Africa na duniani pia.

RAPPER KUTOKA MBEYA CITY 'IZZO B' AMEPATA SHAVU LA KUTENGENEZEWA NGOMA NA PRODUCER MKONGWE KATIKA MEDANI YA MUZIKI "MASTER J" WA MJ RECORDS

Rapper kutoka Mbeya City anae-hit na ngoma yake ya ''Ball Player'' akimshirikisha Ngwair, Quick Rocka na Ruth amepata shavu la kutengenezewa ngoma na Producer mkongwe katika medani ya muziki, mtu mzima Master J [MJ RECORDS] ikiwa ni kama zawadi kutoka kwa producer huyo.

Mbeya Boy aliandika katika moja ya account zake za mtandaoni akiwa amepiga picha na Producer Master J siku ya Alhamis, "Nakushukuru mwenyezi mungu kwa kuniwezesha kurekodiwa nyimbo na Master J leo tarehe 7/2/2013 siwezi sahau siku hii"  akionekana kuisubiria siku hii ambayo hatimaye imetimia.
 
Izzo Bizness amekuwa akifanya kazi kwa karibu sana na Master J hasa katika masuala ya kimuziki na maisha lakini toka ajiunge na label ya MJ Records mara nyingi ngoma zake zilikuwa produced na Producer Marco Chali ambae pia yupo chini studio hizo, sasa this time Master J anamsukia dundo moja kama offer kwa rapper huyo.

Go Izzo Bizness a.k.a Ball Player, dream just came true, tunasubiria that other hit kutoka kwenye mikono ya Master J himself... MBEYA CITY STAND UUUPPP!!!!

[NEW HIT]:-DAYNA FTN MR BLUE - LEO

Diamond Platnumz Katika Mapenzi Mazito Na VJ Penny... Penny Ana Mimba??!!

 
Ikiwa ni jana tu, Raisi Wa Wasafi, Diamond Platnumz alitupia picha katika moja ya mitandao ya jamii anayotumia, huu ukiwa ni Instagram ya mtangazaji wa kipindi cha Xtreme kituo cha TV cha DTV, Pennyl Mungirwa a.k.a Penny ikiwa na maandishi chini yake yanayoonesha wawili hawa sasa wako katika mahusiano ya kimapenzi.

Diamond anaetamba sana kwa sasa na wimbo wake wa Kesho uliofanyika MJ Records chini ya Marco Chali na video yake kufanywa Nairobi, Kenya ali-post picha hiyo ikiwa na maandishi au Hashtags "#MaBabyMama De'MumOfMyBlood #MamaYounDiamond #YounPlatnumz #YounPrezident" yaliyozidi kuweka wazi kuwa wawili hawa wako pamoja kimapenzi.
Check picha hapa chini:
 
Katika hali iliyozua maswali zaidi, moja ya Hastags hizo, zilionesha VJ Penny ana ujauzito wa Diamond Platnumz... Je ni kweli??  Maandishi hayo yalisomeka, "#MaBabyMama De'MumOfMyBlood"
Wawili hawa wamekuwa wakishukiwa kuwa kwenye mapenzi kutokana na picha tofauti ziliwaweka katika mapozi yaliyoonesha hivyo lakini muda mwingi hawakutaka kuyaongelea haya na mara mara walionekana kukanusha kabisa habari hizo.

[OFFICIAL RELEASE DATE] Steve RnB Kuachia "MUSIC" Hivi Karibuni.

Steve RnB have something special for Valentine's Day. Muimbaji mahiri wa single ya Jambo JamboMUSIC [Its All Bout Music]. inayofanya vizuri sana redioni yuko mbioni kuachia track nyingine itayojulikana kama
Steve RnB ataachia wimbo huo siku mbili kabla ya Valentine's Day, yaani Tarehe 12 mwezi huu ikiwa ni zawadi maalum kwa ajili ya sikukuu hiyo ya wapendanao.
Wasanii kutoka TZ wameendelea kutu-bless na nyimbo mpya kwa ajili ya siku hii ambapo pia wiki kadhaa zilizopita mwanadada Diva [Loveness Love] aliachia track yake pia, inayofahamika kama Mgonjwa Kwa Raha Zako akimshirikisha Mr.Blue ikiwa pia ni special gift ya Valentine's Day...
Tusubirie na hii ya Steve RnB tuone inakuwaje...

Wasanii kutoka Kigoma wakifanya Shooting ya Tangazo la shirika la Hifadhi Ya Jamii ya [NSSF

 
Wasanii kutoka Kigoma wakifanya Shooting ya Tangazo la shirika la Hifadhi Ya Jamii ya [NSSF]... Pichani anaonekana Diamond Platnumz, Queen Darleen, Chege na wengineo.

Kundi hili kwa pamoja ni wasanii kutoka mkoa wa kigoma wakifanya vizuri kimuziki wakijulikana kama Kigoma All Stars wakitamba kwa ngoma zao kama LEKA DUTIGITE na mpya iliyotoka hivi karibuni, NYUMBANI...

SIZE 8 AMETOLEA NJE OFA YA KUPIGA SHOW KATIKA KAMPENI ZA UCHAGUZI NCHINI KENYA

KENYA:
MAMITO mwenye Mpunga wa kutosha Nchini Kenya, namzungumzia Size 8 (Pichani) ametolea Nje ofa za kutumika kupiga show katika Kampeni za Uchaguzi zinazochukua kasi Nchini humo

Kwa mujibu wa mwanamama huyo ambaye hajui ni kiasi gani cha fedha alicho nacho sasa hivi na wala hajasumbuka kupiga mahesabu, amedai kuwa amekuwa licha ya wasanii wengi wa Kenya kushirika katika kupiga kunako kampeni mbali mbali za Uchaguzi nchini humo, yeye ameamua kupiga chini ofa ambazo amekuwa akipewa mara kadhaa na wanasiasa mbali mbali wanaoshiriki uchaguzi nchini humo, huku sababu yake kuu ikawa ni kutaka nchi yake iwe na amani na hawezi kujihusisha na suala hilo

HIZI NDIZO TOP 20 ZA REDIO KITULO FM JUMAPILI HII [10 FEBRUARI 2013]

20:-Nikupe nini - Noorah ftn Ali Kiba
19:-Butterfly - Q Chiller
18:-Kelele - Baucha ftn Ali Kiba
17:-Si Kosa Lake - EMG
16:-Narudi Kazini - Beka Ibrozama
15:-Kidela - Abdul kiba
14:-Nawatangazia Msamaha - Baghdad ftn Amin
13:-Hasira - Chibau ftn Rich Mavoko
12:-Sina noma nae - Mc Koba
11:-Dear God - Kala Jeremiah
10:-Wazo la Leo - Stamina ftn Fid Q
09:-Utamu - Dully ftn Diamond & Dimpoz
08:-Mama Yeyo - Gnako ftn Ben Pol
07:-My Everythin' - Ali Kiba
06:-Bonge la Bwana - Shetta tfn Linnah
05:-2030 - Roma ftn Story
04:-One Time - Rich Mavoko
03:-Me & U - Ommy Dimpoz ftn Vanessa Mdee
02:-Kesho - Diamond
Bonus Track:-Nyumbani - Kigoma All Stars
01:-Jambo jambo - Steve RnB

Kwa Ushauri/Maoni:-ergonsanga@yahoo.com au 0755 894 663.
Jumapili Njema!!!

Saturday, February 09, 2013

[NEW HIT] MUPAGE - RAMA ZINGA


The Making Of Wanasahau wimbo Mpya Ya Conscious Akimshirikisha Belle Nine Katika Studio Za DIGITAL VIBES MOROGORO



The Making Of Wanasahau Wimbo Mpya Ya Conscious Akimshirikisha Belle Nine Katika Studio Za DIGITAL VIBES MOROGORO
   
Song Produced By GQ

Motion Picture By GQ

Special Thanx To SAB Multimedia & Belle 9

Maturationatoka hospitali

  Na Elizabeth John

MUIGIZAJI wa filamu za kibongo na mchekeshaji, Tumaini Martin ‘Matumaini’ ameruhusiwa kutoka Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam ambako anatarajiwa kurejea tena baada ya kumaliza dozi ya dawa alizopewa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, rafiki wa karibu wa msanii huyo, Robert Kiwewe ‘Kiwewe’ alisema kuwa, Matumaini alilazwa hospitalini hapo kwa siku tatu akiwa anasumbuliwa na miguu, ambako juzi aliruhusiwa kurudi nyumbani.

“Hivi nimetoka nyumbani kwao Yombo kumuangalia, bado hali yake sio nzuri, daktari kampa dawa, kamwambia arudi hospitali baada ya kumaliza kumeza dawa hizo, Watanzania tunatakiwa kumuombea mwenzetu ili arudi katika hali yake ya kawaida,” alisema Kiwewe.

Alisema hali yake sio nzuri, kwani hadi sasa hajui ugonjwa unaomsumbua, taarifa walizozipata mwanzo ni kwamba alianza kusumbuliwa miguu, ikafuata na mikono na sasa maumivu yamesambaa sehemu mbalimbali za mwili wake.

Kiwewe alisema kuwa, kutokana na kushindwa kugundua ugonjwa unaomsumbua, daktari ameamua kumpa dawa za kupunguza maumivu.

Alisema kwa sasa hawana utaratibu mwingine ambao wameweza kuufanya hadi amalize kumeza dawa hizo na kurejea tena hospitali.

Matumaini alikwenda kuishi nchini Msumbiji na kuripotiwa kusumbuliwa na maradhi, lakini alishindwa kutibiwa akiwa huko ambako Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla akishirikiana na baadhi ya wasanii, alichukua jukumu la kutoa nauli ya kumrudisha nchini.

Venance Mushi achukua fomu Big Brother

MSHINDI wa pili shindano la Maisha Plus 2012, Venance Mushi aliyekuwa akiwakilisha Mkoa wa Dodoma, amechukua fomu ya kushiriki shindano la Big Brother Africa 2013.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Venance alisema kuwa, ameamua kuchukua fomu hiyo ili kujaribu nafasi ya kuiwakilisha Tanzania kwenye shindano hilo, kutokana na uwezo alionao, ikiwemo wa kuzungumza lugha zaidi ya tatu na kipaji chake.

“Tayari nimeishachukua fomu na nimeshaijaza, natarajia kuirudisha muda wowote kuanzia sasa, naomba wadau waniombee ili kuweza kupita katika usaili hapo baadaye,” alisema Venance.

Pia aliongeza kuwa, uwezo alioonesha Maisha Plus 2012, umempa umaarufu mkubwa, huku akiahidi kufanya vizuri endapo atapata nafasi hiyo mwaka huu.

Venance ambaye ni msomi wa elimu ya juu katika masuala ya mipango na maendeleo, aliyosomea Chuo cha Mipango Dodoma, alionesha kiwango cha hali ya juu kwenye shindano la Maisha Plus, ikiwemo kuyazoea maisha ya kijijini na ubunifu ambao ulimfanya kupata mali na fedha nyingi.

Aidha, mbali na Venance, tayari mastaa wengine wameshajitokeza kuchukua fomu za kushiriki shindano hilo akiwemo aliyekuwa Miss Tanzania 2006 na muigizaji wa filamu, Wema Sepetu.

Fomu hizo zimeanza kutolewa katika ofisi za Dstv na kwa njia ya mtandao wa kampuni ya Multichoice Tanzania.

Friday, February 08, 2013

HEMEDY SULEIMAN a.k.a PHD:-MKUBWA WA FREEMASON ANANISHAWISHI NIJIUNGE UANACHAMA


Kupitia ukurasa wake wa Facebook muimbaji wa R&B na muigizaji wa filamu nchini Hemedy Suleiman aka PHD (Pretty Huge Dude) amesema mkubwa wa Freemason (hajamtaja jina) amekuwa akimshawishi ajiunge na chama hicho.

“Mkubwa wa freemason ananishawishi nijiunge katka chama hicho ila nimemuombea dua Mungu amlani ishallah“na hakika mwenye kujiunga na chama hicho mwisho wake ni kufa napia huenda motoni,” alisema Hemed.


BEER PARTY Saturday 9th Feb - HOLLAND


[PHOTO] Tiwa Savage Avishishwa Pete Ya Uchumba...

Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria, mwanadada Tiwa Savage ambae anatamba na baadhi ya track zake kama Love Me Love Me, Kele Kele na nyingine nyingi amevishwa ''Pete'' na mchumba wake.

Tiwa amevishwa pete hiyo na mchumba wake ambae pia ni meneja wake kimuziki aitwae Tee Billz ambae amekua nae kwenye mapenzi mazito ya siri kwa kipindi kirefu sasa.

Tee Billz amemvisha pete msanii huyo katika siku yake ya kuzaliwa ambapo kwa taarifa nyingine kutoka kwa wawili hao ni kuwa watafunga ndoa kabla ya mwaka huu kuisha.

Ona picha za tukio hilo hapa chini:

[COOMIN' SOON TRACK] - LEO BY DAYNA FTN MR BLUE


Msanii maarufu wa kizazi kipya kutoka Mji kasoro maji ya bluu Moro Town na aliyewahi kufanya poa na kazi zake za muziki kama vile Mafungu Ya Nyanya, Nivute Kwako na Unataka nini si mwingine ni Dayna Nyange a.k.a MKALI WAO sasa yuko kwenye hatua ya mwisho ya kuachia track yake nyingine mpya ambayo inakwenda kwa jina la ''LEO''.

Leo ni track mpya ambayo amempa shavu Mr. Blue a.k.a Kabyser, star wa muziki huu wa Bongo Flava anaefanya vizuri pia katika tasnia hii ya muziki.

Fans wa Dayna kaeni tayari kwa ujio mpya kutoka kwa msanii huyo.

[VIDEO] Check Trailer Ya "IDENTITY THIEF" - Movie Mpya Ya T.I.

Rapper kutoka Atlanta, America si mwingine ni Tip Harris famously known as T.I anatarajia kuachia movie yake nyingine hivi karibuni ambayo inakwenda kwa jina la ''Identity Thief''.

Movie hiyo iliyo katika mtindo wa vichekesho [Comedy] ambayo pia wameaigiza baadhi ya mastar kutoka Hollywood kama Melisa McCarthy, John Cho na Genesis Rodriguez.

T.I. ameshaigiza movie kadhaa ikiwemo ile ya ATL aliyofanya na Big Boi [Outkast], Lauren London na zinginezo.

Angalia hapa chini mzigo wenyewe

Hatimaye ile ndoa ambayo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu ya mwanamuziki wa muda mrefu kutoka Nigeria, 2Face Idibia na mchumba wake Annie Macaulay Idibia sasa inatarajiwa kufungwa Tarehe 23 March mwaka huu.

Hatimaye ile ndoa ambayo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu ya mwanamuziki wa muda mrefu kutoka Nigeria, 2Face Idibia na mchumba wake Annie Macaulay Idibia sasa inatarajiwa kufungwa Tarehe 23 March mwaka huu.

Masaa machache yaliyopita, Annie aliandika kupitia ukurasa wake wa Facebook na kusema kuwa ndoa hiyo itafungwa Dubai.


Annie na mumewe mtarajiwa walikwenda Dubai kuangalia ukumbi ambao watakaofanyia harusi hiyo.

Pia wawili hao wamepanga kusafiri baadhi ya ndugu,jamaa na marafiki wao wa karibu wa kuweza kuhudhuria harusi hiyo ambapo mpaka sasa 2face ameshazuia vyumba kadhaa katika hotel ya Bur Al Arab, Dubai.

Baadhi ya mastar kutoka Nigeria ambao watahudhuria harusi hiyo ni Don Jazzy, D'banj, Banky W, P-Square  na wengine wengi.

Labels