Pages

Friday, April 18, 2014

IYANYA KULIPWA $4000 NA SUTI MPYA ILI AWEZE KUONEKANA KWENYE VIDEO YA HABIDA.

Muimbaji wa Nigeria, Iyanya ameombwa alipwe kiasi kikubwa cha fedha kutokea kwenye video ya wimbo alioshirikishwa na msanii wa Kenya, Habida.

Habida amedai kuwa uongozi wa Iyanya umedai ulipwe $4000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 6.5 ili kuonekana kwenye video hiyo.

Pia walitaka Habida amnunulie Iyanya suti mpya ya kuvaa kwenye video hiyo.

Kama hiyo haitoshi, walitaka msanii wa mitindo binafsi na ukijumlisha vyote hivyo zaidi ya shilingi milioni 9 ilikuwa inahitajika.

“Sina uhakika kama Iyanya alikuwa anajua kinachoendelea. Sikuweza kutimiza matakwa hayo kwa muda huo na nimeamua kuutoa wimbo huo mapema,”
Habida aliiambia Heads Up ya Kenya.

0 maoni:

Post a Comment

Labels