Pages

Friday, April 18, 2014

SHAKIRA ANA NDOTO ZA KUWA FISRT LADY WA TIMU YA BARCELONA

Mwimbaji wa Pop, Shakira ambaye ni mpenzi wa mchezaji wa timu ya Barcelona, Gerard Pique ameweka wazi nia na ndoto yake ya kuwa ‘first lady wa timu hiyo’.

Shakira anaamini kuwa siku moja Gerard Pique atakuwa rais wa Barcelona na hiyo itampa yeye nafasi ya kuwa first lady wa timu hiyo.

“Nafikiri siku moja Gerard atakuwa rais wa Barcelona na mimi nitakuwa ‘first lady’ wa Barca.” Shakira ameeiambia jarida la Bocas.

Kauli ya Shakira inaonesha kumuunga mkono mpenzi wake ambaye aliviambia vyombo vya habari vya Hispania kuwa huenda siku moja atakuwa rais wa Barcelona, “nani anajua, huenda siku moja ntakuwa rais wa FC Barcelona.”

Shakira na Gerard wako katika uhusiano wao kwa miaka minne na wamebarikiwa kupata mtoto wa kiume aitwae Milan

0 maoni:

Post a Comment

Labels