Pages

Friday, July 05, 2013

CRISS BROWN AWATAJA MASTAA ALIOWASHIRIKISHA KATIKA ALBUM YAKE "X" ITAKAYOTOKA JULAI 16 2013

Kutoka katika albam yake mpya ya X ambayo inatarajiwa kutoka hivi karibuni, Chris Brown ameamua kuweka wazi kwa mashabiki wake orodha ya wasanii ambao amefanya nao baadhi ya ngoma zilizopo ndani ya Albam.


Kwa wale wapenzi na wadai wanaoisikilizia kwa hamu albam hii, story kubwa kuihusu kwa sasa ni kwamba ndani yake yupo rapper ambaye anatisha sana kwa sasa, Kendrick Lamar, Wiz Khalifa, Kelly Rowland, BoB,Nicki Minaj bila kumsahau wala kumweka kando bibie Rihanna.

Orodha hii imeachiwa na Chris mwenyewe kupitia ukurasa wake wa twitter na kutokana na hii, tayari mitaa inasubiri kwa hamu kabisa kusikia vile Rihanna, Minaj, Kendrick na wengine watafanya katika albam hii ambayo Chris ameahidi itawarudisha watu katika miguso ya Michael Jackson, Quincy Jones na Stevie Wonder.
Hii hapa ndiyo tweet ya Chris kuhusiana na mchongo huu;

0 maoni:

Post a Comment

Labels