Pages

Friday, November 09, 2012

'SUMA MNAZALETI’ MBIONI KUACHIA NGOMA MPYA ‘ASANTE’, AMPA SHAVU MSANII KUTOKA NIGERIA…!!

MSANII wa muziki wa kizazi kipya Suma Mnazaleti, ameuambia mtandao wa DarTalk kuwa baada ya ngoma yeke ya ‘Chukua Time’, kufanya vzuri sasa anatarajia kuachia track mpya inachokwenda kwa jina la ‘Asante’, ambayo amefanya na msanii kutoka nchini Nigeria anayefahamika kwa jina Dan Joh ambaye pia ni ya producer anayeipika ngoma hiyo.

Suma alisema kuwa kujuana na msanii huyo kulikuja wakati alipokuwa Nairobi Kenya, ambapo alitaka kufanya ngoma moja kali ndipo alipoambiwa kuwa kuna jamaa mkali yupo Nigeria anaweza kusimama vizuri, na baada ya hapo wakafanya mazungumzo na huyo jamaa, baada ya makubaliano wakamtumia beat ili aingize Chorus.

Alisema kuwa kuvuka kwake mipaka na kwenda hadi Nigeria anaamini kunaweza kufungua ukarasa mzuri wa yeye kufika mbali kwani, urafiki wake na msanii huyo hautaishia kwenye ngoma moja pekee bali wataendelea kufanya kazi nyingine kibao.

Alisema kuwa hata hivyo kibao hicho kitakuwa funika mbaya kwani mashairi yanayopatikana ndani ya ngoma hiyo ni yale yenye ujumbe mzito, ambapo aliwataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula ili waweze kupata kitu kingine kitakachowafanya wapate burudani zaidi.
 

0 maoni:

Post a Comment

Labels