Pages

Tuesday, September 02, 2014

Kim Kardashian kuitosa familia yake kwa ajili ya Kanye West



Mwanamitindo Kim Kardashian anaripotiwa kufikiria kuchukua uamuzi mgumu ili kumfurahisha mumewe Kanye West, uamuzi ambao utaiangusha biashara kubwa ya familia yake ‘The Kardashians’.

Kwa mujibu wa The Sunday People, Kim Kardashian anapanga kuitosa reality show ya familia yake ‘Keeping Up With the Kardashians’ kwa sababu Kanye West hapendi kabisa jinsi ambavyo anayaanika maisha yake kwenye kipindi cha runinga.

Kanye West anataka maisha yake na mkewe kuwa ‘binafsi’ kwa kuwa hivi sasa ni tofauti na alivyokuwa awali.

Endapo Kim K atafuata matakwa ya Kanye West, ni dhahiri kuwa Keeping Up With The Kardashian itashuka sana umaarufu kwa kuwa uwepo wake una mchango mkubwa kutokana na umaarufu alionao.

“Lakini ni vigumu kwake kwa sababu kwa kiasi kikubwa familia yake inamtegemea awe pale kuuza maisha yake kwenye kamera. Inawezekana akajitoa hivi karibuni, japokuwa series bado ina hit sana.” Chanzo kiliieleza The Sunday People.

Huenda Kim Kardashian akajikita katika masuala ya mitindo kwa sababu tayari alizindua ‘The Kardashian Kollection’ akiwa na ndugu zake Khole Kardashian na Koutney Kardashian.

0 maoni:

Post a Comment

Labels