Pages

Friday, November 09, 2012

MWIGIZAJI INI EDO KUTOKA NIGERIA AMEJITOA KATIKA UKURASA WA FACEBOOK

 INI Edo amewaambia mashabiki wake kwamba hayupo kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook na kwamba akaunti zinazoonekana zimetengenezwa.

Msanii huyo ambaye hivi karibuni ilivumishwa kwamba ameachika, amesisitiza kuwa yupo kwenye mtandao wa Twitter tu na wala si vinginevyo.

"Nimeona na kusikia watu sana wanatumia akaunti feki kwenye Facebook kutapeli watu. 

Nataka kuuambia ulimwengu kwamba siko tena kwenye Facebook."

"Wasikubali kutapeliwa na wahuni kupitia jina langu, mimi niko kwenye Twitter tu na si muda mwingi nakuwa hewani," alisisitiza na kukanusha habari za kuachika.

Amezikana habari za magazeti ya udaku ya Nigeria kwamba ameachika. 

"Hiyo stori imetengenezwa na watu wenye mitazamo yao, si ya kweli. 

Hakuna kitu kama hicho kimenitokea,Tuko pamoja na tunazungumza kwa simu kila siku tangu nitoke Marekani, hakuna wa kututenganisha."

0 maoni:

Post a Comment

Labels