D-Knob akiwa amembeba mtoto wake wa kwanza ...
Dknob ametoa nyimbo nyingi
tu zenye kuwika sana katika Afrika ya
Mashariki...kama vile Elimu Mitaani.com, Sauti
ya Gharama, Ingewezekana na Kitu Gani.
Dknob alizaliwa mnamo
tarehe 12 Februari ya mwaka wa 1980, katika mkoa wa Tabora, Tanzania.
Amenza kupata elimu yake ya
msingi katika shule ya Mazoezi Ligula Mtwara na kuja kumalizia katika shule ya
msingi ya Kipawa iliyopo Dar es Salaam.
Baada ya kumaliza elimu ya
msingi, baadaye akawa anaendelea na masomo ya sekondari katika shule ya
sekondari ya Pugu kwa kidato cha kwanza mpaka nne na baadaye kidato cha tano na
sita akamalizia katika shule ya sekondari ya Jitegemee ya jiji Dare es Salaam.
Shughuli za
muziki
Dknob alianza rasmi
shughuri za muziki kunako mwaka wa 1998, ni baada ya kuvutiwa sana na albamu ya marehemu Tupac na Big Small
au Notorious Big.
Ilipofika mwaka wa 2000,
Dknob alirekodi nyimbo ya Kibongo Stance ambayo pia ilishirikisha baadhi ya
wasanii mbalimbali akiwemo G-Pozz, Pig Black, Dknob mwenywe na wengine kibao.
Mnamo mwaka wa 2001, Dknob
akabahatika kurekodi nyimbo yake ya kwanza akiwa kama
msanii binafsi na nyimbo ilikwenda kwa jina la usiniache ambayo pia
ilimshirikisha Mez B na ilitayarishwa na matayarishaji mashuhuri Bw.Miikka
Mwamba.
Kurekodiwa kwa nyimbo ya
usiniache, ikawa kama ndiyo mwanzo wa Dknob kupata mafanikio na akabahatika
kukutana na Ruge Mutahaba, ambaye pia ni mkurugenzi wa Smooth Vibe Project,
ambayo iliweka nyimbo ya Dknob katika compilesheni za Bongo Hottest (mkusanyiko
wa nyimbo kali za Bongo Flava).
Mwaka wa 2003, Dknob akatoa
single ya elimumitaani.com ambayo ilifanya vizuri zaidi na kuweza hata kumleta
umaarufu katika medani ya muziki wa kizazi kipya.
Na kibao hiko cha
elimumitaani, nacho kilitayarishwa na mtayarishaji mashuhuri wa muziki Bw.
Miikka Mwamba na ndiyo ikawa mara yake ya mwisho kwa Miikka kumtengenezea Dknob
nyimbo kwa mwaka wa 2003 na 2004 Miikka akarudi kwao nchini Finland.
Baada ya hapo, Dknob
akakutana Dj Steve B wa kituo cha radio cha Clouds FM na akawa kama kiongozi wake na hata kumdhamini katika kukamilisha
albamu ya Dknob na kumfanyia promosheni za nguvu.
Akiwa na meneja Stveve B,
Dknob akafanikiwa kurekodi nyimbo ya Sauti ya Gharama akiwa amemshirikisha tena
mwanamuziki Mez B na nyimbo ilitengenezwa na mtayarishaji maarufu Bw. P Funk
Majani .
Mwaka wa 2005, Dknob
akafanikiwa kutoa albamu yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la
Elimumitaani.com ikiwa chini yake mwenyewe Dknob akiwa pamoja na Steve B na
albamu ikasambazwa na FKW Promoters.
Mnamo tarehe 4 Septemba ya
mwaka wa 2006, Dknob akataoa single yake ya "ingewezeakana" akiwa
amemshirikisha Ray C na Squeezer na single ikaingia katika albamu ya nyimbo
mchanganyiko ya Pamoja Ndani ya Game (mchanganyiko wa nyimbo kali za Bongo
Flava).
Katika mwaka huo huo wa
2006, Miikka akawa amerudi Bongo na akaanza mpango wa kutengeneza albamu ya
Dknob ya "Bomoa Mipango".
Mnamo tarehe 20 Aprili ya
mwaka wa 2007, Dknob akaachia single yake ya "Kitu Gani" ambayo
ilimshirikisha msanii machachali wa Bongo Flava Bw. Q Jay na ilivyofika tarehe
20 Agosti ya mwaka wa 2007, akatoa video ya nyimbo hiyo na kazi hiyo ilifanywa
na kampuni ya kupigia video ya Visual Lab ya Dar es Salaam, Tanzania.
Ifikapo tarehe 1 Julai ya
mwaka wa 2008, Dknob atatoa albamu yake ya pili itakayo kwenda kwa jina la
“Bomoa Mipango” na single ya kutambulisha albamu hiyo itakwenda kwa jina la
“Dear Mtoto”, ambayo pia inategemewa kutoka mnamo tar. 25 Julai ya mwaka wa
2008.
Katika albamu hiyo, pia
kuna nyimbo ya ziada ambayo inaitwa Badamn akiwa amemshirikisha msanii Cannibal
wa kutoka nchini Kenya.
Maisha binafsi
Mnamo tar. 29 Septemba
2008, Dknob alimwoa Bi. Anitha Ramadhani (amezaliwa 9 Septemba, 1983).
Kwa pamoja wana mtoto mmoja
ambaye alizaliwa kabla ya ndoa aitwaye Vivican, aliyezaliwa mnamo tar. 18
Agosti ya mwaka wa 2006.
Vilevile Dknob ni mtu wa
mitungi tangu yungali bwana mdogo, lakini mitungi yake imefikia kikomo
ilivyofika tar. 8 Januari ya mwaka wa 2009, pale alipowekewa sumu kwenye pombe
akiwa Klabu, hapo ndipo ikawa mwanzo na mwisho wa yeye kunywa pombe.
Kwa sasa anaishi yeye na
familia yake iliyopo huko Kiwalani, jijini Dar es Salaam.
Itaendelea wiki lijalo
Itaendelea wiki lijalo
Babu, umekopi yote kama ilivyo kutoka Wikipedia ya Kiswahili. Mimi ndiye niliyeandika hadithi yote kuhusu D-Knob. Tazama: http://sw.wikipedia.org/wiki/Mtumiaji:Muddyb_Blast_Producer historia ya kurasa kwa uhakika: http://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Dknob&action=history
ReplyDeleteNicheki kwenye FB: facebook.com/muddybtz
Twitter.com/muddybtz
Sio mbaya! Angalau nilichofanya watu wanasoma!
Bonge a.k.a Muddyb!