Habari ya kusikitisha kwa mashabiki wa shindano la Big
Brother Africa, Jumba linalotumika kufanyia shindano hilo lililoko
Johannesburg, Afrika Kusini limeteketea kwa moto September 2.
Kutokana na tukio hilo, M-Net na Endemol South Africa
wameeleza kuwa wamelazimika kubadili ratiba ya shindano hilo msimu huu
lililopewa jina la ‘Big Brother Hotshots’ na halitaanza September 7 kama
ilivyotarajiwa hapo awali.
Chanzo cha moto huo hadi sasa hakijajulikana na makampuni
hayo yameeleza kuwa uchunguzi wa kina utaanza mara moja.
Makampuni hayo yamepata changamoto kubwa kutokana na tatizo
hilo kwa kuwa vifaa vinavyotumika kufanyia uzalishaji ni vya aghali na adimu
sana hivyo wameeleza kuwa ni vigumu kupata vifaa mbadala hivi punde.
“Kila juhudi itafanywa kutafuta ufumbuzi wa tatizo haraka
iwezekanavyo kuhakikisha kuwa reality show hii kubwa zaidi Afrika inaendelea.”
Wameeleza katika tamko lao.
Hakuna mtu aliyejuruhiwa katika tukio hilo.
M-Net and Endemol SA advise that due to a devastating fire at the Big Brother house on 2 September 2014, Big Brother Hotshots will not launch this Sunday (7 September) as schedule.
The cause of the fire at this stage is unknown and investigations will commence as soon as it is safe to do so.
At this stage M-Net and Endemol are urgently looking for an alternative Big Brother house in which to film the production, however as this production has highly technical infrastructure, camera and edit requirements an alternative is not immediately available. Every effort will be made to find a solution as quickly as possible to ensure that Africa’s biggest reality show will continue.
CHANZO:-www.timesfm.co.tz
0 maoni:
Post a Comment