Pages

Sunday, May 06, 2012

Lady Jaydee apanga kutengenezewa beat na Dr Dre!

 


Ameshafanya kazi na wasanii wakubwa Afrika kama Oliver Mtukuzi na wengine lakini kwake Judith Wambura aka Lady Jaydee anaona haitoshi.

Sasa anatamani kufanya kazi na producer mkubwa kabisa duniani na ambaye kwa mujibu wa orodha ya wafalme wa Hip Hop wenye mshiko zaidi duniani (Forbes) mwaka huu amekamata nafasi ya tatu, Andre Romelle Young ama Dr Dre, whaaaaaat! Jaydee you must be kidding right?

Mapema Jumapili hii Jaydee ametweeet, "Mwaka huu unaisha tena kabla Dr.Dre hajanitengenezea Beat, inabidi nijipange upya"

Anaposema mwaka huu unaisha bila kupata mdundo mzito kutoka kwa mchawi huyo wa beats Dr Dre anamaanisha kuwa amejiwekea mpango huo kwa muda mrefu bila shaka!

Bad news kwa Jaydee ni kwamba kama akitaka kufanikisha mpango huo ni lazima akusanye kuanzia dola 100,000 hivi kwa beat moja ambazo ni karibu shilingi milioni 150 za Tanzania! Kama akifanikisha atakuwa msanii wa kwanza anayeishi Afrika bila shaka kuwahi kufanya kazi na Dr Dre!

All the best Jide japo kwa gharama hiyo ni kweli huna budi kujipanga upya!
 
Na daily entertainment take away

0 maoni:

Post a Comment

Labels