Pages

Sunday, May 06, 2012

Simu za Jose Chameleone zawa kimbilio la wanyonge

 


Wanasema ukiwa na hela unaweza kufanya lolote utakalo! Yaweza yasiwe mambo yote katika dunia hii kama vile kununua pumzi, lakini wazo la biashara lolote linaweza kutekelezwa kama pesa ikiwepo.

Kibongobongo wazo rahisi kabisa la msanii wa muziki apatapo vijisenti ni duka la nguo? Hakuna idea zingine? 

Ni tofauti kidogo kwa nguli wa muziki nchini Uganda Jose Chameleone.

Yeye anafikiria mambo makubwa zaidi! Tayari wiki iliyopita amezindua simu zake za mkononi ziitwazo Chameleone Mobile!

Katika uzinduzi huo wa nguvu watu maarufu, wawakilishi wa makampuni ya simu na wadau wa mawasiliano ya simu nchini Uganda walihudhuria.

Bobi Wine alikuwepo kwenye uzinduzi kumpa shavu mwenzie
Simu hizo za bei bwelele kabisa zitakuwa na rangi mbalimbali za “Kinyonga”.  Pamoja na bei yake kuwa ndogo jambo ambalo litazifanya zinunuliwe kama njugu na hasa wananchi wa kawaida, simu hizo zina memory card, flashlight, FM radio,MP4 player na vingine.

Zilianza kuuzwa muda mfupi tu baada ya kuzinduliwa huku zingine zikitolewa bure kwa wageni waalikwa. 

Simu hizi za Chameleone zinauzwa kwa shilingi 60, 000 ya Uganda sawa na shilingi 35,000 hivi za Tanzania.

Chameleone atatumia duka la kaka yake Humphrey Mayanja lililipo Ivory Plaza jijini Kampala kama makao makuu ya simu hizo.

Uhakika ni mkubwa kuwa maelfu ya watumiaji wa simu nchini Uganda watataka kuimiliki kutokana na bei yake ndogo na jina la mwanamuziki huyo.  Hiyo ni sababu makampuni mengi ya simu yamekuwa karibu naye yakitaka kuingia ubia wa kibiashara naye.


Nini kilitokea kwa maji ya Lady Jaydee aliyekuwa na mawazo makubwa kama ya Chameleone!!!!
Na daily entertainment take away.

0 maoni:

Post a Comment

Labels