Pages

Sunday, May 06, 2012

Beyonce apewa tuzo ya uandishi wa habari!

 


Beyonce Knowles – mwanamke mrembo zaidi duniani  (kwa mujibu wa People Magazine) mke wa rapper wa pili kwa hela duniani, Mama wa mtoto mrembo na mshindi wa tuzo kibao za Grammy na sasa ameongeza heshima nyingine ambayo si rahisi kuifikiria .

















Mwanamuziki huyo ameshinda tuzo kutoka kwenye umoja wa waandishi wa habari weusi wa New York kwa makala yake aliyoiandika kwenye jarida la Essence iitwayo "Eat, Play, Love”.

Katika makala hiyo Beyonce anahalalisha uamuzi wake wa kuchukua miezi tisa nje ya shughuli za muziki kwa kusafiri na kujitambua. Sentesi zilizoshinda ni pamoja na ile aliyoandika “, “In Capri I ate pizza and drank red wine every Sunday. I discovered I love artichokes and that a salad and fresh fish are not only healthy choices but incredibly delicious.”

Hata hivyo uamuzi wa Beyonce kupewa tuzo ya uandishi wa habari umekosolewa vikali.

“Tuzo kama hizi huwasahau wana habari wa kweli ambao huandika mada za maana na za hatari” alikosoa mwandishi mmoja wa Mused Magazine.

Ripoti ya mwandishi huyo ilionesha mashaka iwapo kweli Beyonce aliandika kipande hicho mwenyewe. Hata hivyo mhariri wa burudani wa Essence Cori Murray ameliambia gazeti la New York Daily News, “Ni mwandishi wa kweli. Tulihariri alichokiandika lakini kila mmoja huhaririwa isipokuwa Toni Morrison”.

Wakati Beyonce akijiongezea heshima nyingine ya uandishi wa habari, ameamua kuuonesha uzuri wake kiduchu akiwa bila nguo kwa kusambaza picha hii!










Damn!!!
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Na daily entertainment

0 maoni:

Post a Comment

Labels