Pages

Sunday, May 06, 2012

Mayweather awapa raha wana Hiphop!

 


Ukimtoa Mike Tyson, hakuna boxer mwingine duniani kipenzi cha wanamuziki hasa wa Hiphop kama Floyd Mayweather Jr.

Usiku wa kuamkia leo amedhihirisha kuwa hatakuja kushindwa ulingoni na boxer yoyote wa uzito wake kwa kumshinda Miguel Cotto kwa pointi na kuchukua mkanda wa WBA junior middleweight.





















Boxer pekee aliyebakia na ambaye anadhaniwa pengine anaweza kuivunja rekodi yake ya kutopigwa ni Manny Pacquiao wa Ufilipino.

Baada ya ushindi huo, wanamuziki na watu wengine maarufu duniani waliushambulia mtandao wa twitter kuonesha furaha yao juu ya ushindi huo uliompa dola milioni 32 za kuweka benki ama kula bata!


0 maoni:

Post a Comment

Labels