Pages

Sunday, July 29, 2012

Keko asainishwa na Sony BMG Africa



Tuliliona hili linakuja mapema mno kutokana na uwezo wa rapper huyu. Hatimaye kweli imekuwa hivyo. Rapper wa kwanza wa kike nchini Uganda kupenya kwenye mainstream, Keko amekula mkataba na record label ya Sony BMG Africa.

Keko amekuwa akiwasiliana na Sony BMG Africa na amekuwa akifunga safari za hapa na pale kwenda Afrika Kusini kuzungumzia mchongo huo. Habari njema ni kuwa rapper huyo anayetamba sasa na ngoma ‘Make You Dance’ amechukuliwa rasmi.

Kwa sasa Keko anajiandaa kufanya collabo na msanii wa Afrika Kusini Toya Delazy ambaye naye yupo chini ya Sony.

Keko anaungana na mkenya Xtatic aliyesainishwa hivi karibuni na label hiyo pamoja na Rose Muhando ambaye alichukuliwa mwaka jana.
 
Habari na LEOTAINMENT.

0 maoni:

Post a Comment

Labels