Habari zilizotufikia hivi punde zinasema boti ya Kilimanjaro 2 iliyokuwa
ikitoka Pemba kuelekea Ugunja inasemekana imepingwa na dhoruba kali na
kunusurika kuzama, inadaiwa kuna vifo vimetokea.
Ukweli
ni kwamba wimbi kubwa liliipiga boat na kusababisha hali ya
tafrani. Nimetoka kuongea na mamlaka ya bandari sasa hivi na boat iko
njiani inakuja unguja iko maeneo ya Beit ras sasa hivi. Haijazama na
iliondoka na abiria watu wazima 269, watoto 60 na mabaharia 8 wote wako
salama.
Wimbi kubwa liliipiga likachukua mabegi na baadhi ya life jackets. Injini za boat zilizima, ilibidi watulie kwa muda kuona kama wimbi lilichukua na baadhi ya abiria lakini hakuna hata mtu mmoja aliyeachwa.
Nakumbuka mamlaka ya hali ya hewa walitoa tahadhari kuhusu mchafuko wa bahari hizi siku.
CHANZO:-JAMII FORUM NA CLOUDS FM
0 maoni:
Post a Comment