Pages

Wednesday, January 01, 2014

MSANII M.I.A HAYUPO TENA ROCK NATION RECORD LEBEL YA JAY Z

Unakumbuka Mstari Wa Jay z "I Dont Get Dropt, I Drop The Lebel" Inaonekana M.I.A kautumia hapa. 
Mwaka 2014 ameanza tofauti kwa lebel ya Rapper Jay Z kwa kupoteza mmoja ya wasanii wakali kwenye himaya yake.

Huyu M.I.A ni msanii mwenye kipaji tofauti na wasanii wengine na kama hufuatili vitu adimu kwenye game basi kazi zake zimekupita. 

M.I.A Alikuwa chini ya usimamizi wa Rock Nation na alikuwa akisimamiwa kama msanii na kazi zake. 
Msanii huyu alitangaza kupitia kurasa yake ya Twitter kuwa " Anaondoka Rock Nation na anatoa shukrani zake kwa wote waliompa nguvu kupitia kazi yake ya MATANGI "
M.I.A Mwenye miaka 38 alianza kufanya kazi na Jay-Z mwezi May mwaka 2012 na kujiunga na wasanii kama Rihanna, J. Cole, Meek Mill na Wale.

0 maoni:

Post a Comment

Labels