Pages

Friday, December 28, 2012

VANESSA MDEE a.k.a V KUUTAMBULISHA WIMBO WAKE MPYA MWAKANI 2013

Baada ya kufanya vizuri katika collabo mbili kati ya A.Y na Ommy Dimpoz aliweza kufahamika  na kupelekea mashabiki wengi kumkubali katika muziki wa Bongo Fleva,Sasa kama unakumbuka siku ziliyopita alifunguka katika ukurasa wake wa twitter na akasema kwamba anatarajia kuachia ngoma yake mpya siku ya tarehe 26 mwezi huu lakini mpaka sasa kimya ni tatizo.

  
Leo kupitia Double XXL aliamua kufunguka na kusema kwamba amekuwa na mambo mengi sana na ndiyo maana akuwa na time ya kuitambulisha lakini ameamua kuchukua uamuzi wa kuitambulisha ngoma yake mpya siku ya tarehe 12 mwakani.Kwa hiyo kama wewe ni shabiki wa Vanessa Mdee kaa tayari kwa ujio mpya kutoka kwake.
 

0 maoni:

Post a Comment

Labels