Boti
ya Kilimanjaro II ikitokea Pemba kuelekea Unguja imepigwa na dhoruba
leo Jan 5 2014 kwenye saa nne asubuhi na kuponea kuzama ilipokua kwenye
eneo hatari la Nungwi ambapo ilizama kidogo mbele na kunyanyuka hivyo
watu wa mbele wote wakaachwa lakini pamoja na kuwatupa hao watu kwenye
maji Nahodha akafanya uamuzi mwingine mgumu.
Aliona akisimama ili kuwaokoa wale watu boti yote ingezama pale hivyo
akaamua kuendelea na safari lakini kabla ya kuondoka watu kadhaa ndani
ya boti wakajitolea kuwatupia life jacket wale waliotupwa kwenye maji
ambapo shuhuda anasema kama mtu hajui kuogelea anaweza kupoteza maisha
kwa sababu hawakua wamejiandaa kwenye tukio hili la ghafla na sio wote
wamepata vifaa hivyo vya kujiokoa.
Shuhuda mmoja anasema ‘yani boti ilizama ghafla mbele hivyo watu
wakatupwa kwenye maji kwenye hii sehemu ambayo kuna mkondo wa maji,
upepo ulikua mkali sana yani unaona watu wanajaribu kujiokoa mabegi na
vitu vingine vinaonekana juu ya maji’
0 maoni:
Post a Comment