Shirika la TUNAJALI
linatarajia kuzindua mradi wa zero Vvu katika mkoa Njombe na Iringa ili kutokomeza
maambukizi mpya ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Hayo yamebainika mapema hii leo
mjini Makambako mkoani Njombe kwenye kikao cha wadau na wanahabari wa vyombo vya habari vya mkoa
wa Njombe na Iringa ambapo wanahabari hao wametakiwa kuwa chachu ya kutumia vyombo vyao vya
habari katika kutoa elimu kuhusu tiba ya ART kwa maisha yote kwa wajawazito na
wanaonyonyesha wenye maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Katika kikao hicho imebainika kuwa Tanzania
imepiga hatua kubwa katika kupunguza viwango vya maambukizi ya virusi vya UKIMWI
kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
Tanzania imelenga kutokomeza maambukizi mapya ya virusi
vya Ukimwi miongoni mwa watoto na kuwafanya akina mama waishi kwa muda mrefu
zaidi.
Mpango huu umezinduliwa na
mh. Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania DR.Jakaya Mrisho Kikwete mkoani
Lindi siku ya Ukimwi duniani mwaka 2012 na umeadhimia kufikia malengo ya kutokomeza
maambukizi hayo kutoka asilimia 26 mwaka 2011 hadi asilimia 4 ifikapo mwaka2015.
0 maoni:
Post a Comment