Pages

Wednesday, November 13, 2013

TIMBULO:-BAADA YA IMEKATIKA HIKI NDICHO KINACHOFUATA.




The Hit Maker wa Nyimbo kama Waleo wakesho,Bado Kijana,Domo langu na Anayefanya Vizuri na Kazi yake mpya ya IMEKATIKA aliyowashirikisha X Maleya Kutoka Cameroon si mwingine ni TIMBULO amefunguka kuhusu mpango mzima jinsi Video ya Wimbo Huo itakavyofanyika.

Timbulo amesema Kuwa Endapo Ratiba zao (Timbulo na X Maleya) Zikikaa Vizuri basi kunaoption tatu ambazo wamezipanga ikiwa ni moja Kukutana na X Maleya London Uingereza au Ufaransa Au Timbulo Kusafiri mpaka Comeroon na Kufanya Video Hiyo na Chaguo la Tatu ni X Maleya Kufanya Clip za Video ambozo zinawahusu na Kuzituma Tanzania kama ilivyokuwa Audio yake na Kisha Director atakaye Husika Kushoot Video ya Wimbo Huo Kuzifanyia kazi Clip Hizo kwa Kuziunganisha.

Ameyasema Hayo wakati akifanya Mahojiano na Ergon Elly katika kipindi Cha 970 SHOW kinachorushwa Kupitia Redio Kitulo Fm wilayani Makete Mkoani Njombe na Kuongeza kuwa Mipango Imeshaanza.

Awali wakati Timbulo akizungumzia Ujio wa Wimbo wake Mpya ambao Leo Unaitwa IMEKATIKA alisema kuwa utaitwa ELASTIC YA PENDO lakini Mara baada ya Wimbo Huo kukamilika alichukua Jukumu la Kuwasikilizisha Baadhi ya Watu wake wa Karibu na Kumshauri Kazi Hiyo iitwe IMEKAIKA na Kuongeza Kuwa mpango wa Kufanya Version Mbili uliota mbawa Kutokana na X Maleya Kuwa Busy na Kazi…..Kama Ulikuwa haufahamu ni kwamba Ilitakiwa Kazi Hiyo Itengenezwe Tanzania Kwa Producer  Man Walter na Cameroon na Wao X Maleya na Ichaguliwe moja ambayo itafaa kuachiwa Rasmi kwenye Vituo Vya Redio.

IMEKATIKA sasa Iko katika Vituo vya Redio vya Tanzania na Cameroon na Ni Mali Halali ya Timbulo na X Maleya kwa Maana kila Mmoja anahaki ya Kuitumia Kokote Duniani….Alisema Timbulo.

‘’Namshukuru Mungu Mipango yote ambayo niliitangaza mwanzoni mwa mwaka huu Imekamilika kwa Kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na kufanya Collabo kubwa na ya kwanza Tangu kuanza kwa Muziki na Wasanii Kutoka Cameroon X Maleya….Pia kuikamilisha Albam ambayo ni vitu vichache tu vimesalia’’….Alisema Timbulo

hHuHHHHhhhhhhhhhhkl;f eya;TPHHHHHHH

0 maoni:

Post a Comment

Labels