Pages

Thursday, December 05, 2013

11 DESEMBA 2013 DJ CHOKA KUACHIA NGOMA MPYA

dj

Ukiwa mfuatiliaji mzuri wa burudani ya muziki, haswa muziki wa hapa nyumbani Tanzania basi jina la Dj Choka halitokuwa geni kwako, kwa kuwa huyu ni mmoja wa ma Dj ambao wanafanya kazi nzuri sana hapa nchini kwa kugawa burudani safi kwa wale wapenzi wa burudani ya muziki wa hapa nchini.

Kupita website ya Dj huyu mahiri, imeripotiwa kuwa Dj huyu anatarajia kuachia ngoma yake mpya siku ya Tarehe 11, December mwaka huu. Dj choka amabaye yupo katika record company ya B’Hitz, ataachia ngoma hiyo mpya iitwayo Stinga Li… ambapo ngoma hii itakuwa ya pili kwa mwaka 2013 baada ya kutamba na wimbo uitwao Press Play.

Wimbo huu mpya umefanyikia katika studio ya B’Hitz chini ya producer mkali, maarufu kama Pancho Latino… kwa hiyo kwa wale wapenzi wa kazi za Dj Choka wakae tayari kwa ajili ya ujio mpya wa Dj huyu amabapo pia atashirikiana na vichwa vipya kabisa katika game, wasanii kama wakina  MIS RIZZY, PLUTO na wengineo.

0 maoni:

Post a Comment

Labels