Rais
wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela amefariki dunia.
Mandela
anaejulikana kama mpigania uhuru, usawa na haki za binadamu atakumbukwa
kwa kujitoa kwake katika kuhakikisha watu weusi wanapata haki sawa
katika ardhi yao toka kwa utawala wa makaburu kitu kilichofanya atumikie
kifungo cha miaka 27 gerezani na hatimaye kuachiwa huru na kuwa rais wa
kwanza mweusi nchini Afrika Kusini.
Dunia nzima imepokea kwa mshituko
taarifa za
kifo cha Mandela huku Rais Jakaya Kikwette akiamuru siku 3 za
maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti. Pumzika kwa amani
Tata Madiba.
0 maoni:
Post a Comment