Pages

Sunday, December 01, 2013

WASHIRIKI WAWILI KUTOKA NCHINI UGANDA NA RWANDA WASHINDWA KUFIKA FAINALI ZA SHINDANO LA TUSKER PROJECT FAME SEASON SIX

tpfex16
Ikiwa zimebakia siku 7 tu kufikia fainali za shindano la Tusker Project Fame Season Six, weekdn hii shindano hilo liliendelea kama kawa huku washiriki wote washindano hilo walikuwa katika probation/ hatari ya kuondolewa katika kinyanga’nyiro hicho cha kumsaka mshindi wa TPF 6.
Lakini katika probation hiyo washiriki hao walifanikiwa kuokolewa na wapenzi wao ama watazamaji wa shindano hilo kwa kupigiwa kura ili waweze kubakia katika mpambano huo, lakini ilikuwa bahati mbaya kwa washiriki wawili ambao waliyaaga shindano hilo rasmi jana.

Washiirki hao wawili walishindwa kubakia katika shindano hilo kutokana na kuapata kura chache kushinda washiriki wengine, washiriki hao wawili waliyoaga shindao hilo, mmoja ni kutoka Uganda ajulikanaye kwa jina la Kojjo na mwingine kutoka Rwanda mwana dada Phionah.

Ni week moja tu imebakia kufikia Final ya TPF  6, ambapo tuatashuhudia mkali mmoja ambaye atafanikiwa kunyakua ushindi wa shindano hilo mwaka huu.

0 maoni:

Post a Comment

Labels