Pages

Saturday, April 28, 2012

Kidumu jukwaa moja na Msechu

MSANII kutoka nchini Burundi aliyefanikiwa kutamba Afrika Mashariki kutokana na nyimbo zake, Kidumu, anatarajia kufanya shoo akiwa pamoja na Peter Msechu kutoka Tanzania.

Shoo hiyo iliyopangwa kufanyika sehemu maarufu ya kiburudani iliyopo jijini Dar es Salaam ijulikanayo kama Mbalamwezi Beach, inatarajia kufanyika Ijumaa ya Mei 4 mwaka huu.

Kidumu ambaye alikuwa kioo kwa msanii Peter Msechu wakati wa shindano la Tusker Project Fame, atasindikizwa na msanii huyo katika nyimbo zake atakazoziimba usiku huo.

Na mwanasporti.

0 maoni:

Post a Comment

Labels