Pages

Saturday, April 28, 2012

KITABU: Chuo Kikuu cha Hiphop!

 

 
 
Hiki ni kitabu kuhusu Hip Hop kimeandikwa na M.S. HANZI "MALLE" ni denti wa Chuo Cha Ustawi wa jamii Dar es salaam.

Dhumuni la kuandika kitabu hiki ni kutoa mwanga kwa jamii kuhusu Hip Hop na ukweli uliopo kuondoa mtazamo hasi kwamba Hip Hop ni uhuni, ni ya rika fulani tu, kutokana na makosa maarifa utamaduni wa Hip Hop, vijana wengi duniani wanakosea kwa kufikiri vitu/ vitendo kama kuvuta bangi, kunywa vileo, kuvaa mavazi ya wabunifu, kujibandika plasta zenye alama za x, kubeba bastola (gun) au kwenda kujirusha club ndo "Hip Hop" .

Hip Hop inafanywa kimakosa sana na wasanii wengi ambao wanafanya kazi katika nguzo ya ughanaji (uchenguaji). 

Na haya makosa yote kwa kawaida huhamasishwa na kupewa promo na kiwanda cha muziki na washirika wengine ambao hudumaza utamaduni huu kwa kuteka ufahamu wa vijana na maadili yao. 
Kupata kitabu hiki piga simu 0715 076 444 upate copy yako ili uweze kusoma mambo kibao kuhusu Hip Hop.

Na, Darhotwire

0 maoni:

Post a Comment

Labels