Pages

Friday, April 20, 2012

KOFFI OLOMIDE APATA KIBALI CHA KUIMBA NYIMBO ZA TABU LEY



Baada ya Concert yake iliyofana ya Koffi Chante Tabu Ley na Koffi chante Lutumba mwanamuziki nguli Koffi Olomide ameomba ruhusa kwa watoto na familia ya marehemu Franko Luambo Luanzo Makiadi ili aweze kupiga Concert na huku akiimba nyimbo za mwanamuziki huyo mahiri aliyetamba na bendi ya T.P Ok Jazz

Koffi amesema kuwa kutokana na Matukio yaliyojiri kwa wanamuziki wa Congo waliokuwa wakim support Rais Kabila huko Europe ameamua kuongeza show zake nchini Congo na anataka awaridhishe mashabiki wake kwa kuwapa ladha na kile kitu roho inapenda.

Akiongea na Digital Congo Koffi amesema kuwa anajiimarisha kwenye ziara za Africa zaidi kwa mwaka huu ambapo amepanga kufanya maonyesho kadhaa.
Kwa mujibu wa habari ambazo zimetolewa na Koffi mwenyewe anasema kuwa amepanga onyesho hilo la kumuenzi Luambo limepangwa kufanyika July 7, 2012, kwenye bwawa la kuogelea la Hoteli maarufu ya The Grand huko Kinshasa.

Koffi amesema kuwa mazungumzo yameshafanywa ya awali na tayari familia ya marehemu iliwakilishwa na Emongo ambaye anasema kuwa alimuandikia yeye binafsi na kumuomba aziimbe hizo nyimbo za marehemu baba yao na mazungumzo yakaanzia hapo.

Haikuwa jitihada zangu bali ni wanafamilia ya Mareemu hasa baada ya kuona picha na video za show ya Simaro Lutumba na Tabu Ley.

“Nisingeweza kukataa nafasi hiyo adhimu ya kuiimba sauti ya yule mzee kwakweli hata ungekuwa wewe ndio mwenye kipaji kama changu usingekataa aliongeza Koffi”...

KWA HISANI YA PRO 24.

0 maoni:

Post a Comment

Labels