Wiki hii
haijamuendea vizuri mwimbaji wa Canada, Justin Bieber ambaye ameripotiwa
kuonekana kwenye video nyingine akitumia maneno yenye ubaguzi wa rangi ikiwa ni
siku moja baada ya kuomba radhi kwa video ya aina hiyo iliyotolewa na TMZ.
Katika video hiyo yenye
dakika 45 iliyotolewa na The Sun ambayo pia ilichukuliwa wakati akiwa na umri
mdogo, Bieber anasemekana kuwa alibadili mashairi ya wimbo wake wa ‘One Less
Lonely Girl’ na kuuita ‘One Less Lonely Nig**’.
Chanzo kimeiambia
NY Dailye News kuwa Bieber alifanya utani kuhusu kutaka kujiunga na kundi la
kibaguzi lilikuwa likiwapiga vita watu weusi la Ku Klux Klan.
“Inabidi watu
walilione hili. Watoto wa kawaida katika jamii hawafanyi utani wa aina hii.
Analindwa na watu wa mitandao lakini kamera hazidanganyi. Huyu ni Justin
halisi.”
0 maoni:
Post a Comment