Pages

Thursday, June 05, 2014

T.I azungumza Kiswahili Wakati akijibu kuhusu ugomvi wake na Floyd Mayweather Jr




http://img1.wikia.nocookie.net/__cb20130902112547/ladygaga/images/b/bb/Ti.jpg
Wiki kadhaa zilizopita ugomvi kati ya T.I na bondia Floyd Mayweather ulikuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

MayWeather Jr alizungumza katika interiview moja na kuwaomba msamaha mke na watoto wa T.I, lakini T.I alielezea zaidi uvumi kuwa aliumizwa jichoni na kisha kupost picha kuthibitisha.

Wiki hii rapper huyo alinaswa Na TMZ akitembea barabarani na kuhojiwa kuhusu ugomvi kati yake na Mayweather ambapo alikataa kabisa kuzungumzia kilichotokea kati yao.

Baada ya kuendelea kusongwa na muuliza maswali, T.I aliweka msisitizo wa maelezo yake kwa kuongea Kiswahili kueleza kuwa hakuna tatizo kwa upande wake.

“Everything is wonderful men ‘Hakuna Matata’ that means everything is wonderful for the rest of your days.”

Neno Hakuna Matata ni sehemu ya maneno ya Kiswahili yaliyosambaa zaidi duniani.

0 maoni:

Post a Comment

Labels