Siku
moja baada ya kundi la G- Unit kuungana jukwani katika show ya Summer Jam
iliyoandiwa na Hot 97, wasanii wote wanne walioiunda G-Unit ya awali wamekutana
kwenye wimbo mmoja ikiwa ni baada ya miaka sita.
50
Cent, Lloyd Banks, Young Buck na Tony Yayo wameweka kando tofauti zao na
wameamua kupiga kazi kama zamani, ‘Nah
I’m Talking Bout ni wimbo unaoirudisha ladha ya G-Unit kwa mashabiki.
Hii
ni remix wimbo wa Hit-Boy na HS87 “Grinding’ My Whole Life” na wamempa
shavu pia Kidd Kidd.
Swali ni Je, ndo
kurudi kabisa kwa kundi lile la zamani au ni ushirikiano wa wimbo mmoja?
“Everything
cool here till trip.” Amesema 50 Cent kwa utani.
Leo
(June 3) ni siku ambayo albam ya 50 Cent ‘Animal Ambition’ inatoka rasmi.
0 maoni:
Post a Comment