Staa wa filamu za Bongowood, Rose Ndauka
ambaye ni mjamzito anadaiwa kuwa atazaa kabla ndoa mwezi Aprili,
mwakani.
Akizungumza na mwanahabari wetu, mchumbaa’ke, Malick Bandawe
ambaye ni memba wa kundi la muziki la TNG alianika aya za Kurani kuwa
katika Dini ya Kiislamu si ruhusa kufunga ndoa na mwanamke ambaye ni
mjamzito kwani ni sawa na kufunga ndoa na watu wawili hivyo anamsubiri
ajifungue kwanza.
“Ni kweli mchumbaa’ngu hivi sasa ni mjamzito na
anatarajia kujifungua mapema mwezi wanne, mwakani.
“Kuhusu kufunga naye
ndoa kwa sasa ni ngumu hadi ajifungue kwani kwa dini yetu (Uislam) si
ruhusa kufanya hivyo lakini atakapojifungua tu tutafunga ndoa,” alisema
Malick.
Malick ambaye hivi sasa anatamba na Wimbo wa ‘Crazy Man’ alisema
kuwa ana furaha kubwa kuitwa baba mtarajiwa na anamuomba Mwenyezi Mungu
Rose ajifungue salama kwani anampenda kupita maelezo.
Baada ya
kuzungumza na Malick, gazeti hili lilimtafuta mama wa Rose Ndauka,
Batuli kufungukia ishu ya mwanaye kubeba ujauzito kabla ya ndoa ambapo
aligoma kuzungumza kwani hakubaliani na suala hilo.
0 maoni:
Post a Comment