Pages

Monday, February 03, 2014

Lady Jay Dee kuachia rasmi video ya 'Historia' February 8

Lady Jay Dee kuachia rasmi video ya 'Historia' February 8, mashabiki 20 walio Facebook kuhudhuria party maalum ya kuitambulisha

Mitandao ya kijamii inazidi kuwa njia rahisi na kubwa zaidi kwa wasanii kuwasiliana moja kwa moja na mashabiki wao na hata kufahamu ni kwa jinsi gani wanaelewa na kuwafuatilia kwa karibu, na zaidi kutoa maoni yao moja kwa moja kuhusu kinachofanywa na wasanii hao.
Mwimbaji wa kike wa bongo flava mwenye mafanikio makubwa, Judith Wambura aka Lady Jay Dee amebreak habari njema kwa mashabiki wake wa mitandao ya kijamii ambao wanafikia 225,722 kwa upande wa Facebook na zaidi ya 66, 400 wanaomfuata kwenye Twitter, kuwa ataitoa rasmi video ya wimbo wake wa ‘Historia’, February 8 mwaka huu kupitia party maalum, na watu 20 kati yao watapata nafasi ya kuhudhuria tukio hilo.
Mashabiki wa Facebook wamepewa nafasi zaidi ambapo kigezo ni kujibu maswali yatakayotolewa na mwimbaji huyo wa Joto Hasira.
“Video ya Historia iko tayari na itatoka Jumamosi ya tar 8 february 2014 kwenye party maalum ya kuitambulisha, na kutoka humu facebook nitaalika watu 20 wa kuja kuiangalia kwa mara ya kwanza kabla haijaruka kwenye TV zote.. 
Swali litakuja na 20 wa mwanzo watakaopatia nitajumuika nao. Usicheze mbali.” Ameandika Lady Jay Dee.

0 maoni:

Post a Comment

Labels