Pages

Saturday, February 01, 2014

PRODUCER LAMAR ADAI KUWA NA MPANGO WA KUNUNUA NDEGE BINAFSI

IMG_8021

Kila mmoja ana ndoto zake za kuwa na kitu cha thamani maishani lakini ndoto aliyonayo producer Lamar, kwa wengi inaweza kuonekana kama kubwa mno kwake. 

Lamar ameiambia East Africa Radio kuwa ana mpango wa kununua ndege yake binafsi atakayoitumia kuzunguka popote anapotaka.

Kuonesha kwamba anataka kuanza kuishi ndoto hiyo mapema iwezekanavyo, Lamar ameshaanza kufanya mazungumzo na wauzaji wa ndege hizo ili ajipatie yake mapema.

Lamar si mtu pekee mwenye ndoto ya kumiliki ndege binafsi. 

AY pia ameamua kujifunza urubani kwa kuamini kuwa siku moja anaweza naye anaweza kumiliki yake mwenyewe.

“Wanakuambia dream big, thing big. Fikiria kitu ambacho ni kikubwa zaidi
ya uwezo wako. 

Kwahiyo naweza kusema kuwa kila kitu kinawezekana kwasababu hata wale wenye private jet wakati wakiwa wadogo au wakati hawawezi kuafford walikuwa wanafikiria kuwa kuna siku nao wanaweza kuwa na private jet, so vyote viwili vinawezekana,” AY aliiambia Bongo5.

0 maoni:

Post a Comment

Labels