Pages

Saturday, February 01, 2014

OGOPA DEEJAYS YA KENYA YASITISHA MIKATABA YA WASANII WAKE

Jina la Ogopa Deejays limekuwa zaidi katika miaka ya karibuni nchini Tanzania kutokana na wasanii wengi wa Bongo kufanya video na kampuni hiyo, ambayo ilianzishwa miaka 1990 ikiwa studio ya kurekodi audio pekee
kwa wakati huo.


ogopa3
Kwa mujibu wa mtandao wa GHAFLA, Ogopa deejays imesitisha mikataba ya baadhi ya wasanii ambao ilikuwa ikiwasimamia kwa miaka kadhaa iliyopita.
Avril
Wasanii waliopitiwa na panga hilo ni pamoja na mwimbaji mrembo Avril ambaye taarifa za hivi karibuni zinasema anategemea kuhamishia makazi
yake Afrika Kuisni, yaliko makazi ya mchumba wake wanaetarajia kufunga ndoa hivi karibuni.
marya
Marya
Wasanii wengine ambao mikataba yao imesitishwa na Ogopa ni Marya,
Colonel Moustapha na Kenzo.
Mustafa
Colonel Moustapha

Mmiliki wa studio ya Ogopa Lucas Bikedo, ametoa maelezo kuhusu taarifa zilizoenea za kusitishwa kwa mikataba ya baadhi ya wasanii wake,

“Kila mara mashirika hufanya mapitio ya ndani kutathmini utendaji dhidi ya matarajio. 

Wakati wa mapitio, maamuzi magumu hutakiwa
kufanyika”.

Ilisema taarifa kutoka kwa Lucas baada ya GHAFLA kutaka kupata ufafanuzi.

“Sehemu ya matarajio yetu imekuwa ni kutafuta na kutoa vipaji ambavyo vinaweza kushindana nje ya Afrika Mashariki. 

Katika siku za nyuma mfumo huu umeweza kufanya kazi vizuri sana. 

Hata hivyo, sekta ya burudani imebadilika kwa haraka na uwekezaji uliohusika kuleta mafanikio unakuwa kila siku.

Kama biashara, uwekezaji ni lazima ulete faida ndani ya wakati uliokusudiwa. 

Hii itaruhusu uwekezaji mpya ili uchumi ukue. Na hii inawezekana tu katika mazingira ambapo vipaji vinavyohusika vinapotambua kuwa hata kama kuna kushinda ama kushindwa ni lazima uendele kujitahidi kadri ya uwezo katika kazi iliyo mbele. 

Hakuna mbadala wa kufanya kazi kwa bidii, malengo na nidhamu.

Mtindo wa biashara wa sasa wa kusaini vipaji ni hatari sana na una assumptions nyingi mno.

Sehemu ya tathmini inayoendelea inahusisha na
kuangalia mtindo huu na umuhimu wake katika hali ya sasa.”

Hata hivyo Lucas hakutoa majibu ya moja kwa moja kuhusu wasanii wanaodaiwa kupoteza nafasi zao Ogopa deejays.

*Source: GHALFA*


0 maoni:

Post a Comment

Labels