Pages

Monday, February 24, 2014

Meneja wa Tip Top Connection Babu Tale amesema kuna uwezekano wa kuja kufanya kazi tena na MB Dogg

Meneja wa Tip Top Connection Babu Tale amesema kuna uwezekano wa kuja kufanya kazi tena na msanii aliyewahi kuwa chini ya kampuni yake kipindi cha nyuma MB Dogg, lakini sasa itakuwa ni kibiashara zaidi tofauti na zamani walipokuwa wanafanya kazi kindugu.

MBDogg
MB Dogg

Akizungumza na Millardayo.com Tale amesema, wapo wasanii kadhaa ambao walitoka Tip Top wanaotaka kufanya naye kazi akiwemo Keisha na Spack, lakini yeye anampango wa kufanya kazi na MB Dogg ambaye pia ametoa wimbo mpya wiki iliyopita uitwao ‘Umenuna’.

“lakini kwa sasa nataka tumuangalie Mb Dogg kwa macho mawili” Alisema Tale. “Mb dogg ana kipaji watu wanaujua uwezo wa Mb Dogg, Mb Dogg sio kama amepotea hapana ila hana uongozi anahitaji promo ya nguvu tu
Babu Tale
akipata hiyo anarudi kupiga hela kama zamani”.
Babu Tale

Akifafanua utaratibu wake wa sasa wa kufanya kazi na wasanii, Tale ambaye ndiye meneja wa Diamond Platnumz kwa sasa, amesema zamani alikuwa akiishi nao kama ndugu lakini sasa hivi anaagalia biashara zaidi.

“Kwa sasa mimi ni mfanyabiashara tofauti na zamani nilipokuwa naishi na wasanii tulikuwa tunaishi kama kaka kwamba matatizo yapo kila mmoja ana matatizo yake mimi nina matatazo na wasanii nao wana matatzio hizo ni sehemu za maisha”.

Tale aliongeza, “wasanii wengi wanaokuja kwangu wanasema wanataka tufanye biashara na
mimi ni mfanyabiashara kama wao, tunabaki kwenye biashara kwa sababu kama naweza kumsimamia msanii ambaye sijatoka nae toka mwanzo kwanini yule niliekuwa nae mwanzo nishindwe kumsimamia na akaleta heshima nchini
akapata mkate wake wa kila siku na mimi nikapata hela”.

Source: Millardayo.com

0 maoni:

Post a Comment

Labels