Professor Jay ameiambia Bongo5 kuwa wamesaini
mkataba wa mfupi na tayari wameshaanza majukumu ya kazi ya kuhamasisha vijana
kufanya kilimo mkoani Iringa.
“Watu waliotuteua wanaitwa Ansaf lakini wawakilishi
wa serikali ya United States
of America ambayo inaitwa ‘One’ kwahiyo hapo
kuna Ansaf na One ndio wanetuteua sisi kuwa mabalozi,” amesema Jay.
“Wamesema tuanze kuifanya kwasababu inatakiwa
ifanyike kwa wakati huu na hatujasaini mkataba mrefu, tumesaini mkataba tu wa
kuwaambia kazi zao walizotaka tufanye Iringa, tumeenda na kuzifanya kwa utiifu
kabisa, kwa uaminifu kabisa na kwa uaminifu kabisa na tumewajulisha watu wetu
waweze kufanya lakini wametuambia tunaweza kufanya vitu kwa mkataba muda mrefu
kidogo.”
0 maoni:
Post a Comment