Pages

Sunday, February 02, 2014

RAIS KIKWETE AONGOZA MATEMBEZI YA MSHIKAMANO YA MIAKA 37 YA CCM JIJINI MBEYA......KUHUTUBIA TAIFA MCHANA HUU

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Rais Jakaya Kikwete  akiwapungia mkono baadhi ya Wananchi (hawapo pichani),walioshirikia matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya SIDO,kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya mapema leo asubuhi,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.

Kushoto kati ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki,Mh.Godfrey Zambi,Katibu Mkuu wa chama hicho,ndugu Kinana pamoja na Katibu wa Uchumi na Fedha,Bi Zakia Meghji wakishiriki matembezii hayo yaliyofana kwa kiasi kikubwa jijini humo.

Rais Kikwete ambaye ndiye mgeni rasmi wa sherehe hizo atahutubia leo  mchana kwenye maadhimisho ya sherehe hizo zitakazofanyika katika uwanja wa Sokoine mkoani humo.
Rais Kikwete akiongoza  matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya SIDO akiwa sambamba na baadhi ya watoto,kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.Kushoto kati ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki,Mh.Godfrey Zambi,Katibu Mkuu wa chama hicho,ndugu Kinana pamoja na Katibu wa Uchumi na Fedha,Bi Zakia Meghji wakishiriki matembezii hayo yaliyofana kwa kiasi kikubwa jijini humo. 
 Baadhi ya vijana wakereketwa na chama cha CCM wakiwa na mabango yao. 
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Rais Jakaya Kikwete  (pilia kulia) akiwa tayari kuongoza wanachana na Wananchi (hawapo pichani) kushiriki matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya SIDO,kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya mapema leo asubuhi,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM,Bwa.Phillip Mangula,wa tatu kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki,Mh.Godfrey Zambi,Katibu Mkuu wa chama hicho,ndugu Kinana pamoja na Katibu wa Uchumi na Fedha,Bi Zakia Meghji pamoja na Waziri Ofisi ya Rais asiye na Wizara maalum,Prof Mark Mwandosya wakiwa tayai kuyaanza matembezi hayo.
 Rais Kikwete akizungumza na baadhi ya watoto waliokuwa miongoni mwa watoto waliojitokeza kushiriki  matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya SIDO mapema leo asubuhi kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.
 Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakishiriki kuchukua matukio yaliyokuwa yakijiri kwenye matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya SIDO mapema leo asubuhi kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Rais Jakaya Kikwete akipokelewa na viongozi wa chama hicho ngazi za juu,pichani akisalimiana na  Katibu Mkuu wa chama hicho,ndugu Kinana na anaeshuhudia pichani kati ni Makamu Mwenyekiti wa CCM,Mh.Phillip Mangula,tayari kwa kuongoza matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya SIDO,kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM. 
 Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya SIDO mapema leo asubuhi kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akifurahi jambo na Waziri Ofisi ya Rais asiye na Wizara maalum,Prof Mark Mwandosya 
 Ndugu Kinana akizunguza jambo na Mwigulu Nchemba kabla ya kuanza matembezi ya mshikamano. 
  Msafara wa Rais ukiwasili sehemu ya kuanza matembezi ya mshikamano. 
 Mambo ya matembezi ya mshikamani yakiwa yameiva
 Rais Kikwete pia aliungana na Watoto katika matembezi hayo. 
 Mwenyekiti wa CCM,Rais Kikwete akiwasili kwenye bustani za uwanja wa Sokoine kufikia kilele cha matembezi ya mshikamano
 Sehemu ya Wananchi na wakereketwa wanachama mbalimbali wa wa CC Mwakiwa wamekusanyika kwa pamoja tayari kumsikiliza Rais Kikwete mara baada ya kumaliza matembezi hayo yalifanikiwa kwa kiasi kikubwa.
 Baada ya kumaliza matembezi ya mshikamano viongozi wa juu wa CCM,wakisiliza utaratibu wa kuadhimisha sherehe za miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho.

Rais Kikwete akizungumza machache mara baada ya kumaliza matembezi ya mshikamano,Rais Kikwete atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hizo zitakazoanza mapema leo mchana ndani ya uwanja wa Sokoine,jijin Mbeya.

-EDDY BLOG

0 maoni:

Post a Comment

Labels