Pages

Tuesday, August 12, 2014

DIRECTOR KHALFANI BAMUSHKA AACHANA NA NISHER ENTERTAINMENT



C.E.O and President wa NISHER ENTERTAINMENT NISHER ameandika hivi kupitia Account yake ya Facebook

 Nisher Entertainment Inasikitika kuwataarifu Wadau wake wote na Mashabiki wote wa kazi zetu Kua Khalfani Bamushka hatakua Akifanya kazi pamoja nasi Tena! 

Ni kama mwaka na Nusu sasa NISHER (C.E.O and President wa NISHER ENTERTAINMENT) Ali-gundua Kipaji Cha khalfani kwa njia ya facebook.. na baada ya hapo walikutana na kuanza kufanya kazi pamoja... 

Khalfani amejifunza Mengi Kuhusu Video Production Kutoka kwa Mshindi wa Tuzo Za watu 2014 Director Nisher, katika kipindi chote alichokaa kwa karibu sana na Nisher. 

Khalfani aliweza pia kupata nafasi ya kufanya videos alizozioongoza yeye mwenyewe Chini ya Nisher Entertainment kama "LET ME KNOW" ya Chin Bees iliyo pata kuchezwa Channel O...., pamoja na Video Mpya Ya Baby Madaha, Pamoja na Kazi Nyinginezo Nyingi ambazo zilimwezesha Kupata Jina na Kujiweka vizuri zaidi katika Uongozaji na Uandaaji wa Videos.

Nisher Entertainment Pamoja na C.E.O. wake Tunatambua Juhudi na Bidii aliyokua nayo Khalfani na Tunamshukuru Kwa Mchango wake Katika Kufanikisha Shughuli zote za Nisher Entertainment.

Mwisho....Nisher Entertainment inaendelea kufanya Msako wa Vipaji mbali mbali ili kuwapa Ajira vijana wetu kupitia Mitandao ya kijamii... hivyo wadau wote na wote wale wanao penda kazi zao zionekane Msiache kuzituma kwenye inbox yetu....Tunawashukuru kwa kuendelea ku-Support kazi zetu! Ahsanteni.

NISHER ENTERTAINMENT

0 maoni:

Post a Comment

Labels