Pages

Wednesday, August 22, 2012

HUENDA NICK MINAJ AKAWA JAJI WA AMERIKAN IDOL




Kuna tetesi kuwa Nicki Minaj ataungana na Mariah Carey kama jaji wa American Idol.

Kwenye mahojiano mahsusi mtandao wa Us Weekly umeripoti kuwa vyanzo vimethibitisha kuwa Nicki Minaj atakuwa jaji mpya wa shindano hilo.

Chanzo kimoja kimesema "Sina uhakika kama deal imekamilika tayari lakini ndio kuna uhakika kuwa atafanya. Kuna mambo kidogo ya kusaini na itakuwa hivyo.”

Chanzo kingine kimesema muimbaji huyo wa "Super Bass" ana asilimia 100 za kuwa jaji wa American Idol.

Mpaka sasa hakuna uthibitisho kutoka Fox Network wala kwa Nicki Minaj, lakini vyanzo vinasema wapo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha mikataba.

Msanii mwingine ambaye amekuwa akisemwa kujiunga na show hiyo kama jaji ni Pharrell Williams.

0 maoni:

Post a Comment

Labels